1. Nipomaliza la saba, litorokea mjini,
Mguuni nina raba, na kibegi mgongoni,
Nauli ninayo haba, nimeweka mfukoni,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.
2. Gari zuri tukapanda, kuelekea mjini,
Shauku ilinipanda, kuondoka kijijini,
Nauli nikailinda, nisiibiwe mjini,
Penzi la mwana wa bosi...