Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda amesababisha kuahirishwa mara mbili mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Kilimanjaro(KNCU) kwa sababu zake binafsi mkutano uliopangwa kufanyika jana ukasogezwa mpaka leo lakini mkutano huo umefutwa tena leo na kusogezwa mpaka Jumatatu...