Kwa mujibu wa katiba ya JMT suala la rasilimali za Taifa limejengewa wigo mpana wa ulinzi wake kupitia ibara ya
27.-(1) Kila mtu ana wajibu wa kulinda maliasili ya Jamhuri ya Muungano, mali ya mamlaka ya nchi, mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na pia kuheshimu mali ya mtu...