Ripoti hii ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu huko nchini Kenya imebaini dosari kubwa za kifedha katika ajenda ya Rais Wiilliam Ruto ya "Hustlers Fund"
Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka wa fedha 2023/2024, Hustler Fund imetoa hadi KSh 31 milioni (Tshs Milioni 628) kwa jumla ya wateja 253,717...
Wakati Tanzania ikizozana kuhusu uwajibikaji wa matumizi ya fedha za umma, hebu tutazame hali katika mataifa yanayodai kuwa vinara wa uwazi na utawala bora. Ripoti za hivi karibuni kutoka Marekani zinaonyesha kuwa Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) inashindwa kupitisha ukaguzi wa hesabu...
Utangulizi
Ripoti za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) zimekuwa zikionyesha matukio mbalimbali ya ubadhirifu wa fedha za umma na utawala mbovu katika taasisi za serikali. Hali hii inazorotesha maendeleo na kuathiri ustawi wa wananchi. Ili kujenga “Tanzania Tuitakayo,” ni...
Nini maana ya UBADHIRIFU? Ubadhirifu ni hali ya kukosa uwezo wa kujizuia au kujidhibiti, katika matumizi ya Fedha au Rasilimali mbalimbali, na hii hutokea kwa wale waliopewa mamlaka za kuongoza Serikali ama Taasisi mbalimbali katika jamii zetu.
Je, nini kifanyike ili kuchochea Uwajibikaji dhidi...
Hakika huu ni usanii mkubwa na very calculated.
CCM ambayo ndio ina dhamana ya kuongoza serikali inatumia ujinga wetu kutuhadaa ili tuone wanastahili kuendelea kushika dhamana hiyo pamoja na madudu yao ya kutisha.
Kwa mujibu wa sheria Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali CAG ni mtu...
Ikiwa Bunge linajadili taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG), kisha hakuna azimio linalotekelezwa?
Ni sababu zipi kisheria na Kikatiba zinaruhusu ripoti hiyo kusomwa Bungeni? Je Bunge linapitisha Bajeti wasiyoweza kusimamia na kuamua matumizi yake au lina kazi gani haswa...
Ni takribani miaka mitatu sasa CAG amekuwa akitoa taarifa zilizojaa madudu ya ufisadi na rushwa pasi na mamlaka ikiwemo serikali kuchukua hatua yeyeote kukabiliana na tuhuma hizo kwa kipindi chote hicho.
Imefikia hatua sasa wananchi wamepoteza kabisa imani ya kuendelea kusikiliza ripoti...
Maeneo kumi (10) muhimu katika Uchambuzi wa Ripoti ya CAG mwaka 2022/23.
Kama ambavyo tumekuwa tukifanya kila mwaka, uchambuzi wetu mwaka huu utajikita kwenye mambo kumi (10) ambayo tunaona ni muhimu Watanzania kuyatambua na tutayatolea mapendekezo ili yaweze kuchukuliwa hatua.
Katika...
Kibonzo cha msanii Massoud Kipanya kinafumbua fumbo lisilojadilika.
Nani mwenye uthubutu?
Hata Rais mwenyewe anaonekana kuvuta miguu kwenye kuwachukulia hatua wabadhirifu waliotajwa kuhusika na ukwapuaji wa fedha za umma.
Tutafakari pamoja.....
Je, tunajadili kama wananchi kwa lengo gani...
Kitu kikubwa nilichogundua ni kuwa, Namna pekee ya Kuyaokoa mashirika ya serikali yanayo andamwa na hasara kubwa ni namna ya kupata waendeshaji wawajibikaji.
Imekuwa ni kawaida sana Kipindi hiki cha Uongozi wa Rais Samia Watu kubadilishiwa vitengo tu badala ya kuwajibishwa.
Utakuta Kiongozi...
Madudu na mawashawasha ya ripoti za CAG nyingi tunasikia ubazilifu mkubwa kila kona pesa ambazo zimetumika vibaya ila cha kushangaza huku mtaani hakuna mwenye pesa kwa wale mimi na wewe.
Kipindi cha jakaya angalau tumeona pesa ilikuwepo na maisha kwenye mzunguko ukilinganisha JPM na Samia...
Ibaki kuwa siri ya Rais na watu wake baasi, maana kiukweli pamoja na madudu yote yanayoanikwa lakini hakuna hata mmoja aliyechukuliwa hatua.
Zaidi ya kuleta manung'uniko na hasira kwa wananchi, hakuna lolote linalofanyika , kuna haja gani sasa ya kutupotezea muda kuangalia na kusikiliza ripoti...
MKUTANO wa Bunge la Bajeti umepangwa kufanyika kuanzia Jumanne ya juma lijalo. Pamoja na mambo mengine, ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Mwaka 2022/23 itawasilishwa kwa mujibu wa sheria.
Ibara ya 143 ya...
Mfanyabiashara maarufu nchini, Mzee Azim Dewji amezungumza na vyombo vya habari kumpongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuruhusu mjadala wa ripoti ya CAG unaoendelea bungeni kuwa mjadala wa wazi, amesema uwazi huo utasaisia wezi wa pesa za miradi kuacha tabia hiyo
Kwa upande mwingine...
Huu ni Ushauri wa Bure kwa Rais Samia kwenye mabadiliko tarajiwa ya cabinet kufuatia Ripoti ya CAG, namshauri Rais Samia, asibabaike sana na kuangalia ma vyeti ya usomi kwenye uteuzi wa cabinet yake, atumie watu wenye uzoefu, mfano Waziri wa Fedha wa sasa Dr. Mwigulu Mnchemba ni msomi mzuri wa...
Kwa siku kadhaa, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Spika Dkt. Tulia Ackson limejadili Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG).
Kimsingi, Wabunge wengi wameuona, wameusemea na kuukaripia ufisadi na ubadhirifu mkubwa ulioainishwa kwenye Ripoti ya CAG. Wabunge...
Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson amesema kutokana na mjadala wa Wabunge kuonesha Halmashauri nyingi zina Ubadhirifu mkubwa, anapata wakati mgumu kusikia kauli za Mawaziri wakisema Wabunge wanasema uongo wakati taarifa za Kamati zinaonesha kuna ubadhirifu katika Halmashauri hizo.
Akitolea...
Luhanga Mpina akitoa mchango wake amesema, amesoma taarifa ya CAG mwaka 2021, amesoma majumuisho ya majibu ya serikali na mpango wa utekelezaji wa taarifa ya CAG, hakuna sehemu kwenye majumuisho ya mpango wa utekelezaji wa taarifa ya CAG inayoonesha hatua mahususi zilizochukuliwa mpaka sasa toka...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.