Mbinguni kuna hukumu,amewaita manani
Malaika walo zamu,aridhi na samawini
Idadi wameshatimu,walo watu na majini
Umeonewa shetani?
Mikao ni kwa kaumu,watu wa zama fulani
mitume yao hashimu,ilotumwa duniani
Wamekaa kwa nidhamu,kikao kiso amani
Umeonewa shetani?
Mkuu wa mahakimu,aliyeketi enzini...