soko la kariakoo

Soko la Kariakoo (Kariakoo Sokoni)
Soko la Kariakoo ni soko kuu jijini Dar es Salaam na Tanzania ambapo kunafanyika biashara za aina zote za mahitaji muhimu ya kila siku ya binadamu. Biashara katika soko hili zinafanyika kwa jumla na rejareja.

Soko hili linajumuisha majengo mawili makuu (soko kubwa na soko dogo) pamoja na maeneo yanazunguka majengo hayo. Soko la Kariakoo lipo katikati ya jiji la Dar es Salaam na ndiyo chanzo cha eneo zima la Kariakoo kujulikana kwa jina hilo.

Jengo la Soko Kuu la Kariakoo lipo katika kiwanja namba 32 mtaani Kariakoo, katikati ya makutano ya mtaa wa Mkunguni na mtaa wa Nyamwezi na limezungukwa na mitaa ya Nyamwezi, Mkunguni, Sikukuu na Tandamti.

Mwaka 2021 soko hilo liliungua na moto jambo lililofanya shughuli sokoni hapo kusitishwa ili kupisha uchunguzi na badaye ukarabati, na mpaka kufikia April 2024 ukarabati wa soko hilo ulikuwa umefika 93%
  1. danhoport

    Barabara ya mtaa wa swahili karibia soko la Kariakoo inamwagwa lami kwa kasi sababu kuna msafara unapita hivi karibuni kwenda kuzindua soko

    Nimeshtushwa na huu utendaji wa haraka wa kuziba viraka kwenye ichi kipande cha barabara kinachoanzia kwenye mataa ya fire mpaka kwenye mataa ya msimbazi kupitia mtaa wa swahili. Nilichokuja kugundua kumbe kuna msafara wa rais unapita hivi karibuni kwenda kuzindua soko la Kariakoo
  2. Lord denning

    Kamera za ulinzi kufungwa Kariakoo kwa gharama ya Tsh Milioni 514

    Katika kuhakikisha biashara zinafanyika saa 24, Jiji la Dar es Salaam limeingia mkataba na Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) unaogharimu jumla ya shilingi milioni 514 wa usimikaji wa mifumo ya kamera za ulinzi katika barabara na maeneo ya Kariakoo ambapo jumla ya kamera 40...
  3. upupu255

    Pre GE2025 Mkurugenzi wa Jiji Dar asema Jiji halitawavumilia wakandarasi wanaochelewesha miradi, Ufungaji wa kamera za CCTV katika Soko la Kariakoo kuanza

    Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Elihuruma Mabelya, amesisitiza kuwa jiji hilo halitawavumilia wakandarasi wanaochelewesha miradi. Tamko hilo amelitoa katika Viwanja vya Karimjee kwenye hafla ya utiaji saini wa miradi mitano muhimu inayolenga kuboresha huduma za jamii na...
  4. Mindyou

    Kamati iliyoundwa na Waziri Jafo kuchunguza wafanyabiashara wa kigeni Kariakoo yaitisha press kuonesha wamefikia asilimia 50 ya Uchunguzi wao

    Wakuu, Hivi kulikuwa na haja ya watu kuitisha press kutuambia kuwa wamefikia asilimia 50 ya majukumu ya kazi yao? Kwanini wasingetupa majibu baada ya kupata majibu kamili? =============================================== Baada ya Rais Samia kutoa agizo la kuanzishwa kwa tume ya siku 30...
  5. Cute Wife

    Rais Samia: Wafanyabiashara mlichoma moto Soko Kariakoo sababu nilizisema changamoto za uongozi uliokuwepo

    Wakuu, Alaaaah, kumbe wafanyabiashara walichoma soko la Kariakoo wenyewe? Hii ndio sababu hatujui ndani ya kilichokuwemo kwenye ripoti rya tukio la moto ule? ====== Moja ya mambo aliyosema mwenyekiti wa kariakoo katika risala yake ni kuhusu ziara ya Samia Kariakoo, ambako alisema Rais Samia...
  6. Mindyou

    Wafanyabiashara soko la Kariakoo kuanza kurejeshwa Februari 2025, 336 wanadaiwa

    Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema zoezi la kuwarejesha wafanyabiashara kwenye soko la Kariakoo lililopata ajali ya moto Julai 10, 2021 na kusababisha wafanyabiashara hao kuondolewa na shughuli kusimama, linatarajiwa kuanza mapema Februari mwaka huu. Akizungumza na waandishi wa...
  7. Waufukweni

    Rais Samia: Serikali kujenga Soko kubwa kama la Kariakoo eneo la Jangwani

    Rais Samia amesema Serikali imejipanga kujenga Soko kubwa kama la Kariakoo eneo la Jangwani kupitia pesa za utekelezaji wa mradi ya DMDP ambapo baadhi ya wafanyabiashara (Machinga) watahamishiwa huko pindi litakapokamili. Soma: Ninachokijua kuhusu Miradi ya DMDP na Ujenzi wa Miundombinu Mkoani...
  8. milele amina

    Soko la Kariakoo: Vipaumbele anavyoviomba Bwana Mushi hadi leo hamna au mnatania?

    Bwana Mushi; 1. Una elimu gani 2. Umri wako 3. Uzoefu wako kwenye biashara 4. Unafanya biashara Gani? 5. Utafanyaje ukichaguliwa, kutokuingiza siasa kwenye biashara? 6. Ni nini msimamo wako, kuhusu migomo ya wafanya biashara? 7. Saa100 ameruhusu raia wa kichina kufanya biashara za umachinga...
  9. J

    Soko la Kariakoo limebaki asilima chache kukamilika, zaidi ya billioni 30 zatumika

    SOKO LA KARIAKOO IMEBAKI ASILIMA CHACHE KUKAMILIKA ZAIDI YA BILLIONI 30 ZATUMIKA Ukarabati wa soko la Kariakoo umegharimu zaidi ya Bilioni 30 na zimebaki asilima chache kukamilika Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ataenda kukagua baada ya kukamilika pia ametoa fedha kwaajili ya ujenzi wa masoko...
  10. Pdidy

    Mkuu wa Mkoa Dar wapige chini baadhi ya Viongozi wa mashirika Soko la Kariakoo

    Gazeti za jana zimesikitisha sana kwa yanayoendelea pale Kariakoo. RC wangu, wakati doll ikikagua yale majina, nikujuze tu kuwa mamlaka yako inaruhusiwa kuwaondoa viongozi wa Shirika la Masoko Kariakoo mapema. Kumekuwa na kama dili za ajabu, soko likiungua viongozi wanafikiri ndio sehemu ya...
  11. Erythrocyte

    Waliokatwa vizimba soko la Kariakoo waandamana kwenda ofisi za CCM Lumumba!

    Hii ndio Taarifa ya sasa kutoka Dar es Salaam. Kwamba Wale waliokuwa wafanyabiashara wa soko hilo kabla halijaungua na ambao majina yao hayapo kwenye mkeka mpya, wameandamana kuelekea CCM Lumumba! Pia soma: Mgomo wa Wafanyabiashara: Biashara zafungwa Kariakoo leo Juni 24, 2024 Sasa sijajua...
  12. OR TAMISEMI

    Orodha kamili ya majina ya wafanyabiashara wenye sifa na vigezo vya kurejeshwa sokoni Kariakoo yatolewa

    Shirika la Masoko ya Kariakoo linautangazia umma orodha kamili ya majina ya wafanyabiashara wenye sifa na vigezo vya kurejeshwa sokoni Kariakoo baada ya ujenzi wa soko jipya na ukarabati wa soko kuu kukamilika. Taarifa hii inapatikana katika tovuti ya Ofisi ya Rais –TAMISEMI www.tamisemi.go.tz...
  13. Lady Whistledown

    Taka zimemwagwa Mtaani Msimbazi B, hii ni hatari sana kwa Watumiaji wa Soko la Kariakoo

    Hali halisi ya Mtaani wa Msimbazi B Kariakoo Kwa hali hii watu tutaacha kupata magonjwa ya tumbo, kuhara au hata kipindupindu? Uongozi wa Soko hauoni hii hali na kushughulikia?
  14. ThisisDenis

    Nini kimejiri soko la Kariakoo Dar es Salaam?

    Sina habari za mwisho wa ugomvi kati ya wafanyabiashara wa Kariakoo na Wachina. Najua kwamba kulikuwa na mvutano kati yao kuhusu masuala ya biashara na ushindani. Inaweza kuwa kwamba pande zote mbili zimefikia mwafaka na zimepata suluhisho la matatizo yao, au pengine mazungumzo yanaendelea...
  15. P

    SoC03 Je, mgomo katika soko la Kariakoo unaweza vipi kukomeshwa usijirudie tena miaka ijayo?

    Ili kuzuia hali kama hiyo isijirudie tena katika Soko la Kariakoo, hatua kadhaa zinaweza kuchukuliwa. Hapa kuna baadhi ya mawazo ambayo yanaweza kusaidia: Mazungumzo na taasisi husika: Wafanyabiashara na wawakilishi wao wanaweza kushiriki mazungumzo na taasisi ya TRA (Mamlaka ya Mapato...
  16. Nyendo

    TRA matopeni, watuhumiwa kukithiri kwa rushwa soko la Kariakoo

    Kwenye kikao cha wafanyabiasha na Waziri Mkuu kilichoitishwa ili kutatua changamoto zao kufuatia mgomo wa wafanyabiara ulioanza tar. 15.05.2022. Wafanyabiasha wawatuhumu maafisa wa TRA kuwaomba rushwa wafanyabiashara. Wafanyabiashara walalamika kufuatwa mpaka nyumbani na maafisa wa TRA ili...
  17. R

    Kwanini tusiwe na maduka ya hadhi nchini ili mawaziri na viongozi wakubwa wasiagize kutoka nje ya nchi?

    Biashara zinaendeshwa Kariakoo kwa sasa hazina tofauti na biashara zilizokuwa zinafanyika miaka ya 1990 za ulanguzi. Soko linazidi kudorora, maduka yenye hadhi yanazidi kupotea na kuzaliwa vibanda vidogo vidogo visivyo kidhi. Mpangilio wa biashara nao unachangia soko kukosa mvuto huku bidhaa...
  18. FRANCIS DA DON

    Je, ni sahihi kwa soko la Kariakoo kuhamishiwa Ubungo?

    Kuna tetesi nimesikia kwamba Soko kuu la Kariakoo linataka kuhamishiwa Ubungo, kwamba watu badala ya kwenda hadi Kariakoo wataishia tu Ubungo. Je, hii imekaaje kaaje, nini mtizamo juu ya hili? Video chini ina maelezo ya ziada. ========================...
  19. C

    Hivi ile tume iliyoundwa kuchunguza kisa cha moto wa soko la kariakoo ilifikia wapi?

    Siyo mara ya kwanza kuundwa tume ya uchunguzi kufuatia majanga yanayotokea, mbaya sasa hakuna majibu yanayotolewa kama matokeo ya uchunguzi wao. Ni kwamba hatupaswi kujua? Zinaundwa za nini, kujua nini na zinafanya kazi kweli? hatuoni kujifunza kutokana na makosa hivyo inatia wasiwasi juu ya...
  20. Mohamed Said

    Soko la Kariakoo Kuanzia Upya Wake 1900s

    SOKO LA KARIAKOO KUANZIA UPYA WAKE MWANZONI MWA MIAKA YA 1900 Sisi tuliozaliwa miaka ya 1950 tumelikuta Soko la Kariakoo kama linavyoonekana katika picha ya tatu na ya nne. Nikiangalia picha ya mwanzo ya Kariakoo akili yangu inanipeleka katika nyumba ambazo nyingine mimi zinanihusu na nyingine...
Back
Top Bottom