soko la kariakoo

Soko la Kariakoo (Kariakoo Sokoni)
Soko la Kariakoo ni soko kuu jijini Dar es Salaam na Tanzania ambapo kunafanyika biashara za aina zote za mahitaji muhimu ya kila siku ya binadamu. Biashara katika soko hili zinafanyika kwa jumla na rejareja.

Soko hili linajumuisha majengo mawili makuu (soko kubwa na soko dogo) pamoja na maeneo yanazunguka majengo hayo. Soko la Kariakoo lipo katikati ya jiji la Dar es Salaam na ndiyo chanzo cha eneo zima la Kariakoo kujulikana kwa jina hilo.

Jengo la Soko Kuu la Kariakoo lipo katika kiwanja namba 32 mtaani Kariakoo, katikati ya makutano ya mtaa wa Mkunguni na mtaa wa Nyamwezi na limezungukwa na mitaa ya Nyamwezi, Mkunguni, Sikukuu na Tandamti.

Mwaka 2021 soko hilo liliungua na moto jambo lililofanya shughuli sokoni hapo kusitishwa ili kupisha uchunguzi na badaye ukarabati, na mpaka kufikia April 2024 ukarabati wa soko hilo ulikuwa umefika 93%
  1. Rubawa

    Ijue historia ya soko kuu la Kariakoo

    Neno ‘KARIAKOO‘, asili yake ni neno la Kiingereza la ‘Carrier Corps’, likiwa na maana ya kwamba mahala hapo ndipo inapomalizikia misafara iliyokuwa ikiwasili kutokea nje ya hapa mjini, wakati huo wa utawala wa Wajerumani na Waiingereza. Misafara hiyo ilihusisha askari pamoja na wapagazi...
  2. Mohamed Said

    Soko la Kariakoo na harakati za TANU

    SOKO LA KARIAKOO NA HARAKATI ZA TANU Hii makala nimemwandikia ndugu yangu Kheri Chomba mwenyeji wa Kariakoo kumfariji kuwa asihuzunike pale inapotokea watu wakatucheza shere kwa kujifanya kuwa wao wanaujua mji kutushinda sisi wenyewe. "Kheri siku moja katika miaka ya 1970s soko jipya...
  3. Nyendo

    Kariakoo, Dar: Mabadiliko ya vituo vya daladala kufuatia ujenzi wa soko la Kariakoo

    Mabadiliko ya vituo vya daladala kufuatia ujenzi wa soko la Kariakoo
  4. Swahili AI

    Wafanyabiashara tujifunze kupitia haya majanga ya moto

    Habarini wana JF, Kwanza kabisa nitoe pole kwa wafanyabiashara wote wa Soko la Karume, pamoja na Kariakoo (hawa sijawahi kuwapa kutokana na janga la moto walilopata). Kuna suala moja ningependa tujifunze kupitia majanga kama haya ambapo yakitokea yanasababisha hasara kubwa kutokana na upotevu...
  5. Erythrocyte

    Kwanini wananchi wengi wanadai Masoko yanayoungua hayaungui kwa bahati mbaya bali yanachomwa?

    Dhana hii ndiyo inayozungumzwa na Watu wengi mno, kutokana na mazingira yalivyo inaaminika kwamba masoko haya yanapigwa kiberiti, japo haijatajwa hasa ni yupi anayefanya unyama huo. Lengo langu si kufanya uchochezi, nilichozingatia ni ile methali isemayo MFICHA UCHI HAZAI au MFICHA MARADHI...
  6. Erythrocyte

    Soko la Kariakoo lateketea kwa moto

    Soko Kuu la Kariakoo jijini Dar es Salaam linaungua moto usiku huu huku jitihada za kuuzima zikiendelea. Akizungumza na Mwananchi kwa simu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amethibitisha tukio hilo. Makalla ambaye yuko kwenye eneo la tukio, amesema; “Ni kweli soko linaungua na tuko...
  7. Informer

    Historia ya Soko la Kariakoo na Mchora ramani Beda Amuli

    Historia ya jina la Kariakoo na soko la Kariakoo inaanzia tangu enzi za ukoloni wa Mjerumani wakati Tanzania Bara ikiitwa Tanganyika. Mahala lilipo soko hilo palijengwa jengo la utawala wa Wajerumani ambalo lilikusudiwa litumike kama ukumbi wa kuadhimisha sherehe za kutawazwa kwa Mfalme Kaiser...
Back
Top Bottom