Tatizo la matumizi na biashara ya dawa za kulevya limeendelea kuiathiri nchi yetu. Bangi imeendelea kuwa ni dawa ya kulevya inayotumika zaidi na ikizalishwa katika mikoa yote ya Tanzania Bara hususani katika mikoa ya Mara, Morogoro, Arusha, Tanga, Mbeya, Kagera, Ruvuma, Iringa na Njombe...