uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. State Propaganda

    Pre GE2025 Kuelekea Uchaguzi mkuu : Wapinzani bado wamezubaa sana

    Wakati CHADEMA ikikomaa na NO REFORM, NO ELECTION, ACT WAZALENDO nao wamekuja na mpya kususia vikao vya umoja wa vyama vya siasa kwa madai kama ya CHADEMA. CCM wao wako busy kubuni mbinu za kunasa makundi mengi ya wananchi waisapoti na kuipa kura nyingi uchaguzi mkuu. Wanabuni vikundi vya...
  2. Waufukweni

    Pre GE2025 Alex Msama atangaza Tamasha la kuombea Uchaguzi Mkuu, litafanyika Aprili 20, 2025

    Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Kuombea uchaguzi mkuu 2025, Alex Msama leo ameongea na wandishi wa habari kuwa Maandalizi ya Tamasha la kuombea uchaguzi yanaendelea vizuri na kuwa Tamasha hilo lipo na litafanyika Tarehe 20, Aprili 2025 katika jiji la Dar es Salaam na baadae...
  3. Mkalukungone mwamba

    Pre GE2025 TCRA yataka Vyombo vya Habari kuripotiwa uchaguzi bila upendeleo

    MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imevitaka vyombo vya habari nchini katika kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu kuvipatia vyama vya siasa nafasi sawa katika kuripotiwa habari bila upendeleo ili kuondoa malalamiko. Meneja wa Kitengo cha Utangazaji TCRA...
  4. J

    ✳️ NI ZAMU YETU DAR ES SALAAM, TUKAJIANDIKISHE TUWEZE KUPIGA KURA UCHAGUZI MKUU

    ✳️ NI ZAMU YETU DAR ES SALAAM, TUKAJIANDIKISHE TUWEZE KUPIGA KURA UCHAGUZI MKUU Zoezi la kuboresha taarifa na kujiandishika katika Daftari la kudumu la Mpiga Kura litaendelea kwa mkoa wa Dar es Salaam kuanzia Machi 17 hadi 23, 2025. Issa Rajabu Risasi mkazi wa Kawe amewaomba watu wenye sifa za...
  5. JamiiCheck

    Jifunze kuthibitisha maudhui ya Akili Mnemba kwani yanaweza kutumika upotosha kuhusu Wanasiasa wakati wa Uchaguzi

    Ni muhimu kutambua mbinu zitakazokuwezesha kubaini maudhui ya picha, video ama sauti, yaliyotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya AkiliMnemba kwani yanaweza kutumiwa kupotosha uhalisia wa Taarifa nyakati za uchaguzi hivyo kusababisha wananchi kushindwa kufanya maamuzi sahihi. Shikamana na Jukwaa...
  6. Cute Wife

    Pre GE2025 Joseph Selasini: Hatususii uchaguzi, muda uliobaki hautoshi kufanya mabadiliko

    Wakuu, Panazidi kuchangamka huko, Baadhi ya vyama vya siasa nchini vimesema haviko tayari kususia uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu kwa kigezo cha marekebisho ya katiba mpya. Haya yamebainishwa mkoani Morogoro na Makamu Mwenyekiti Taifa Chama cha NCCR Mageuzi Joseph...
  7. Roving Journalist

    Pre GE2025 Wanachama wa ACT Wazalendo wakamatwa kwa kufanya fujo kwenye Vituo vya Uandikishaji Zanzibar

    Kama ambavyo niliwapa habari awali juu ya zoezi la Uandikishaji kwenye Daftari la wapiga kura Mkoa wa Kusini Unguja kuanzia tarehe 08/03/2025 hadi tarehe 13/03/2025; zoezi ambalo Jeshi la Polisi lilikuwa na dhamana ya ulinzi na Usalama wa vifaa, watendaji wa Tume, mawakala wa vyama, wananchi...
  8. milele amina

    Kilio Cha Wananchi : Changamoto za kukosekana kwa usalama wa Raia na Mali zao, Kuelekea uchaguzi mkuu, Njia panda ya Himo Wilaya ya Moshi- Kiliman

    Utangulizi Katika eneo la Njiapanda ya Himo, Wilaya ya Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro, wananchi wanakabiliwa na changamoto kubwa zinazohusiana na usalama. Kilio hiki kimekuwa kikubwa, kwani vibaka, wezi, na wanyang’anyi wamekuwa kero ya kimataifa. Hali hii imesababisha wananchi kutokuwa na amani...
  9. Lord denning

    Kwa dhana ya Kuharakisha Maendeleo ya Wananchi ni heri tuanzishe Utawala wa Majimbo (States) kugawa Majimbo ya Uchaguzi kutengenezeana Ulaji binafsi

    Mwaka 2020 katika Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge, nikiwa nimevutiwa na Sera ya CHADEMA kuhusu kuanzisha utawala wa majimbo nchini Tanzania niliandika uzi kuonesha namna gani utawala huu utafanikiwa katika kuharakisha maendeleo ya Tanzania Uzi wenyewe huu hapa👇...
  10. The Watchman

    LGE2024 Uchaguzi serikali za mitaa 2024 vyombo vya habari havikuripoti kufeli na kufanikiwa kwa wagombea waliokuwa madarakani

    Chuo kikuu cha Dar es Salaam kupitia shule kuu ya uandishi wa habari na mawasiliano kwa umma (SJMC) kwa miaka kadhaa kimekuwa kikitekeleza mradi unaojulikana kama 'Yearbook' ukiwa ni utafiti kuhusu “Ubora wa Maudhui ya Vyombo vya Habari Tanzania. Katika mwaka 2024 utafiti huo ulichunguza uripoti...
  11. A

    Kuhairishwa kwa debi ya kariakoo yachukua mlengo WA uchaguzi wa 2025 Zanzibar leo

    Bodi ya ligi yaangalia kuhairishwa kwa debi ya kariakoo
  12. R

    Kauli mbiu ya CCM Uchaguzi 2025: Kazi na Utu, Tunasonga Mbele

    Maswali yangu: 1. Kazi gani? 2. Utu gani? 3. Kusonga wapi? 4. Mbele wapi? 1. Ali Kibao 2. Soka et al 3. Ben saa nani 4. Kangoye na wengineo. 5. Katiba mpya iko wapi 6. Tume huru iko wapi? etc etc etc UTU UKO WAPI? KAZI IKO WAPI? TUNASONGA WAPI...kaburini/
  13. F

    Mheshimiwa rais usitumie mabilioni ya maskini Watanzania kushinda uchaguzi au kujitetea pale unapokosea

    Tafadhali mheshimiwa rais tunaomba sana usitumie fedha nyingi za walipa kodi maskini kwa ajili ya kushinda uchaguzi. Watanzania wanahitaji maji ya kunywa, barabara angalau za vumbi, vituo vya afya, elimu ya msingi, nk. Inasikitisha mno kuona mabilioni ya fedha ambazo zingetumika kuwasaidia...
  14. P

    Tukiwa Tunaelekea Uchaguzi Mkuu: Ni Yapi Majukumu ya Mbunge?

    October mwaka huu watanzania watawachagua viongozi watakao pewa dhamana ya kuongoza nchi hii kwa miaka mitano (2025 - 2030). Wale wataochaguliwa watakuwa wataunda mihimili ya serikali na bunge na wana influence kubwa pia kwenye mahakama. Kuyafahamu majukumu ya Mbunge huenda itasaidia vyama...
  15. U

    Mkutano wa uchaguzi wa askofu dayosisi ya mwanga Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania kufanyika machi 10, 2025, mrithi wa sendoro kupatikana

    Wadau hamjamboni nyote? Taarifa kamili hapo chini kwa kiswahili: Mwanga. Dayosisi ya Mwanga ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) inatarajia kufanya mkutano mkuu maalumu wa uchaguzi, Machi 10, 2025, ili kumpata mrithi wa aliyekuwa askofu wa Dayosisi hiyo, Chediel Sendoro...
  16. U

    Pre GE2025 Mara: Jimbo la uchaguzi Serengeti kugawanywa kuwa majimbo mawili, Serengeti Mashariki na Serengeti magharibi

    Wajumbe wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mara (RCC) wamepitisha Jimbo la Uchaguzi la Serengeti kugawanywa na kupata majimbo mawili ya uchaguzi ambapo majina ya majimbo yanayopendekezwa ni Serengeti Mashariki na Serengeti Magharibi. Mkuu wa Mkoa wa Mara Evans Mtambi aliongoza kikao...
  17. Papaa Mobimba

    Pre GE2025 RC Kunenge awataka TANROADS na TARURA kumaliza miradi ya barabara iliyoahidiwa na CCM 2020

    Kunenge alitoa agizo hilo katika mkutano wa Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Pwani uliofanyika Kibaha, ukiwahusisha wadau wa maendeleo na wataalamu wa sekta hiyo. Alisisitiza umuhimu wa kuwa na mpango wa utekelezaji wa ujenzi wa barabara, hasa zile zilizokuwa sehemu ya ahadi za uchaguzi. Pia...
  18. The Watchman

    Pre GE2025 Mradi wa uboreshaji wa miji Tanzania (TACTIC) Geita Mjini, Mbunge alalama ubabaishaji wa mkandarasi, Tuliahidi mradi kukamilika kabla ya uchaguzi

    Mbunge wa Geita Mjini, Constantine Kanyasu, amemshutumu mkandarasi anayetekeleza mradi wa uboreshaji wa miji Tanzania (TACTIC) mjini Geita, akimtaja kuwa hana uwezo, hana mtaji, na anakosa wataalamu wa kutekeleza mradi huo kwa ufanisi. Kauli hiyo ya Kanyasu imekuja siku moja baada ya Mkuu wa...
  19. D

    Maono: Mpaka uchaguzi ninaziona kama bilioni 5 hivi zikikusanywa; 2 'zitatumika' katika uchaguzi; 3 zitawezesha safari ya Ulaya na Marekani!

    Siasa achana nayo tu jamani.......siasa ni nyoko. Kila nikiwasikiliza na kuwaona na kurejea taarifa ya 'kusanyaji' kadhaa huko nyuma, naona kabisa hapa hii miamba inatafuta au imelenga bilioni kama tano Hadi sita hivi kufikia uchaguzi. Hiyo ni kutoka kwa tone-tone na wafadhili wengine. Mbili...
  20. K

    Pre GE2025 Ushauri kwa CCM na CHADEMA kukaa meza moja kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao

    Kama Mwananchi na Raia wa Tanzania ninawashauri CCM na CHADEMA wakae meza moja na wajadiliane kuangalia yale mapungufu yanayoonekana kuelekea Uchaguzi Mkuu ili yafanyiwe marekebisho kama itawezekana. Pamoja na kusema kuwa uchaguzi utafanyika kama ilivyopangwa ni sawa lakini CHADEMA wanaweza...
Back
Top Bottom