uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. T

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 LGE2024 Hivi inakuwaje CCM imara kabisa itumie njia za gizani gizani kushinda uchaguzi!?

    Machawa humu ndani wanasifia kila kukicha kwamba ccm ni chama imara sana, ni kwa nini wanatumia mipango myeusi myeusi kushinda chaguzi!? Maana walisema yaliyotokea 2019 hayatatokea tena. Hawa wanaokiri kwamba 2019 hali haikuwa sawa ndio haohao walikuwa wanasifia sana wakati huo ila leo...
  2. JamiiForums Tanzania Makonda ajibu tuhuma za kumpiga risasi Tundu Lissu. Asema Lissu ana matatizo ya akili, aende Milembe

    Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, leo akiwa anawasilisha ripoti yake ya miezi 6 ya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Makoa ameamua kujibu mapigo. Kama mtakumbuka, wiki chache nyuma Lissu alimtuhumu Makonda kuhusika na jaribio la kumuua lililofanyika mwaka 2017. Akiongea na wanahabari leo...
  3. JamiiForums Tanzania LGE2024 Lindi: Msimamizi wa Uchaguzi kwenye Manispaa asisitiza wagombea kufanya kampeni za kistaarabu

    Wakuu, Mbona maelekezo yameanza kuwa mengi na hata kampeni hazijaanza? Msimamizi wa uchaguzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Juma Mnwele amevihimiza vyama vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 kuhakikisha kampeni zao zinafanyika kwa kistaarabu na kwa kufuata...
  4. JamiiForums Tanzania LGE2024 CHADEMA na ACT Wazalendo nendeni mahakamani mkausimamishe Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

    Kwakua mmekubali kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa na kujiingiza kwenye mtego wa kuhalalisha haramu ya CCM, basi nawashauri tumieni mbinu zote halali kudai haki yenu. Nendeni mahakani mkaiombe mahakama mambo yafuatayo. 1. Uchaguzi usimamishwe mpaka kasoro kubwa zilizojitokeza zitatuliwe...
  5. JamiiForums Tanzania LGE2024 Wananchi Dodoma: Tunataka kupita katika uchaguzi wa haki na huru

    Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Dodoma wameviasa vyama vya siasa nchini kudumisha amani wakati wa kukamilisha michakato ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024 Pia, Soma: Yanayojiri kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma 2024 Kadhalika, wameishukuru...
  6. JamiiForums Tanzania LGE2024 Shinyanga wakimbiza kuku kuhamasisha ushiriki wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

    Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga imeanzisha kampeni ya kuhamasisha wananchi kushiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024, kwa kutumia michezo mbalimbali. Bonanza la michezo lililofanyika katika kata ya Tinde limejumuisha mbio za baiskeli kwa wanawake...
  7. R

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Hakuna kitakachobadirika katika uchaguzi huu, ni replica ya 2019/2020

    Mchengerwa: 1. Unaona kabisa anajiamini kusema analolisema. Unaona kabisa kuwa ana mamlaka Kuu inampa kiburi na arrogance! 2. Hakuna kitakachobadirika. 3. Kama alisema Lisu, uchaguzi umeisha ni kujipanga upya! Unajipangaje kwenye mapolisi/risasi/Kangaroo mahakama/Bunge kibudu! 4. Suggest...
  8. JamiiForums Tanzania LGE2024 ACT Wazalendo kufungua kesi Mahakamani kupinga Wagombea wao kuenguliwa, ili uchaguzi urudiwe

  9. J

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Mjadala JamiiForums & Star TV: Nafasi ya Vyombo vya Habari kuelekea Uchaguzi wa Seriali za Mtaa

    JamiiForums kwa kushirikiana na Kituo cha Runinga cha StarTV, itaendesha Mjadala kuhusu Nafasi ya Vyombo vya Habari na Waandishi kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024 Mjadala huo utakaoongozwa na Mtangazaji Edwin Odema 'Chief Odemba', utahusisha...
  10. JamiiForums Tanzania LGE2024 Askofu Fredrick Shoo alia na rafu zinazoendelea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Ataja mbinu zinazotumika kuengua Wagombea!

    Dkt. Fredrick Shoo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), hivi leo amezungumza na waandishi wa habari kuhusiana na zoezi la Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa linaloendelea nchini. Dkt Shoo amesema kumekuwa na makosa mengi katika Ucahguzi huu ikiwemo kuenguliwa kwa wagombea wa upinzani...
  11. JamiiForums Tanzania PreGE2025 Ni mbinu ya kupata kura?, Utekelezaji wa miradi na miundombinu kipindi cha Uchaguzi: Je, Usalama wa Mazingira na Uendelevu unazingatiwa?

    Muda wa uchaguzi ni kipindi cha kipekee katika mchakato wa kisiasa, ambapo wagombea na vyama vya siasa hutumia kila mbinu kujiweka katika nafasi nzuri ya kushinda kura. Katika mazingira ya Tanzania, utekelezaji wa miradi ya miundombinu na maendeleo wakati wa uchaguzi umejikita kama sehemu muhimu...
  12. JamiiForums Tanzania LGE2024 TAKUKURU Iringa kuanzisha uchunguzi kuhusu wagombea wa serikali za mitaa kujitoa baada ya rushwa

    Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoa wa Iringa Imeanzisha Uchunguzi wa Madai ya Uwepo Baadhi ya Wagombea wa Serikali za Mitaa kujitoa Kugombea Baada ya kupewa Rushwa. Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Iringa, Domina Mkama ametoa Kauli Hiyo wakati akizungumzia Utendaji Kazi wa Taasisi...
  13. JamiiForums Tanzania LGE2024 Geita: Wagombea walioenguliwa watuhumiwa kutoa vitisho kwa wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

    Wakuu Kumbe CCM wakiwatishia wapinzani ni sawa tu lakini Waoinzani wakiwatishia CCM, viongozi wake wanaenda hadi kwenye vyombo vya habari kulialia Hivi karibuni nimemuona Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Yefred Myenzi, akieleza kuwa baadhi ya wagombea ambao majina yao yalikatwa...
  14. JamiiForums Tanzania LGE2024 Benson Kigaila: Yeyote akisema hatukujiandaa na uchaguzi anafanya kazi ya CCM

    "Yeyote akisema hatukujiandaa na uchaguzi, awe Mwanachadema, awe MwanaCCM, awe hana Chama ana shida kati ya hizi mbili mosi; hakuwepo wakati wote wa zoezi hili hivyo hajui anachokizungumza au pili; anafanya kazi ya CCM kwa makusudi kabisa." Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu Bara. Kupata...
  15. JamiiForums Tanzania LGE2024 Mkuu wa mkoa Tanga: Wasimamizi wa uchaguzi Tumieni 4R za Rais Samia

    Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian Batilda Burian amewataka viongozi wote ambao wana nafasi za kusimamia michakato ya uchaguzi,kusimamia agizo la kutumia 4R za Rais Samia katika kufanya kazi zao za uchaguzi. Amesema hayo wakati akitoa taarifa za michakato ya uchaguzi ulipofikia kwa...
  16. JamiiForums Tanzania LGE2024 Hujuma Uchaguzi: Mwakajoka atuhumu kuenguliwa kwa Wagombea wa CHADEMA Mikoani

    Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyasa Frank George Mwakajoka, amesema wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wamekiuka kanuni za uchaguzi kwa kuwaondoa wagombea wa chama hicho bila sababu za msingi. Mwakajoka amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa...
  17. JamiiForums Tanzania LGE2024 Msimamizi wa Uchaguzi akanusha wagombea CHADEMA kuwa na ulemavu

    Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai na Msimamizi wa Uchaguzi, Dionis Myinga amekanusha malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya wanaotajwa kuwa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti kwa baadhi ya vijiji katika wilaya hiyo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa wameenguliwa baada...
  18. JamiiForums Tanzania LGE2024 Mara waridhishwa na mchakato wa Uchaguzi Serikali za Mitaa, waomba mamlaka ziendelee kufanya kazi nzuri ili haki ipatikane kwa kila mgombea

    Wakuu, Hawa wanamvua nguo Nchimbi aliyesema demokrasia yetu bado changa na hivyo OR TAMISEMI ilegeze kamba kidogo! Watu maefurahia zoezi yeye anataka waonekane wanoko! ==== Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa mkoani Mara wameeleza kuridhishwa na mchakato wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu...
  19. JamiiForums Tanzania LGE2024 Kubenea: Hakuna uchaguzi, kuna uchafuzi. Vyama kuendelea kushiriki ni kuhalalisha uhuni, madhara yake yataonekana 2025

    Kupitia andiko hilo la leo, Jumanne Novemba 12.2024 Kubenea ambaye ni mwanahabari nguli nchini na Mkurugenzi wa kampuni ya habari ya Mwanahalisi amedai kuwa kitendo cha vyama vya upinzani nchini kuendelea kushiriki uchaguzi huo ni sawa na kuhalalisha 'uhuni' unaoendelea, na hivyo kutahadharisha...
  20. JamiiForums Tanzania LGE2024 ACT Wazalendo: Wagombea wetu 51,423 wameenguliwa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

    Chama cha ACT Wazalendo kinatoa Taarifa kwa Umma kuwa wagombea wake 51423 katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji wameenguliwa kwa sababu ya udhamini wa chama ngazi ya Kata. Wagombea wetu waliogongewa mihuri ya Kata ambayo ndio ngazi ya udhamini ya ACT Wazalendo wameenguliwa...
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…