Mahakama Kuu Kenya imesitisha kutekelezwa kwa mfumo wa usajili wa wananchi kwa njia ya alama za vidole hadi hapo sheria ya kulinda taarifa itakapopitishwa.
Mbali na kuzuia utekelezaji huo, mahakama imesema kuwa kukusanya taarifa za eneo (GPS) na vinasaba (DNA) ni kinyume na katiba ya nchi...