Chama cha ACT Wazalendo kimepokea kwa masikitiko makubwa na kulaani vikali kutekwa kwa wananchi wawili Dar es Salaam na Kigoma katika mazingira yanayotia shaka, huku Jeshi la Polisi likionyesha uzembe wa hali ya juu katika kushughulikia matukio haya. Matukio haya yanatoa picha ya wazi kwamba ama...
Mtu mmoja ambaye hajafahamika jina lake amechukuliwa kwa nguvu na Watu wasiojulikana ambao walikuwa wamebeba silaha na ripoti zinadai tukio hilo limetokea February 20,2025 saa saba mchana katika Kituo cha Mafuta cha Puma kilichopo Kibaha Mkoani Pwani.
Kwa mujibu wa ripoti za Mashuhuda Kijana...
Mbunge wa Iringa Mjini Jesca Msambatavangu ameiuliza Serikali kuwa imejipanga vipi kudhibiti kile alichokiita kuwa wizi wa binadamu (utekaji) nchini Tanzania. Swali hilo lilielekezwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi na lilitakiwa kujibiwa na Naibu Waziri Daniel Sillo. Lakini Spika wa Bunge Dkt...
Wakuu,
Hii kesi naona mauzauza, inaenda kama haiendi inakuja kama haiji. Yaani wanafanya kusudi kabisa ili iishie juu kwa juu. Ngoja tuone nini kitajiri hiyo kesho wakati CHADEMA wakiuamua mbivu na mbichi.
=====
Kwa mara nyingine tena Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni, iliyopo Kinondoni...
Godbless Lema amesema kuwa hana taarifa zozote kuhusu Soka, lakini hisia zake zinaonyesha kuwa Soka hayuko hai. Alisema:
"Sina taarifa zozote lakini hisia zangu zina nambia Deus Soka hayuko hai, ni bahati mbaya sana kuwa na hisia hizi, hakuna Serikali inaweza kumshikilia mtuhumiwa mtoto kama...
Mwenyekiti wa ngome ya vijana akizungumza na waandishi wa habari leo January 9,2025 amesema kuwa
“Naomba niwaambie watanzania suala la ulinzi na usalama ni jambo ambalo tunapaswa tuungane kwa pamoja kupaza sauti zetu kupinga kukemea haya matendo. Na wala tusiseme kwamba haya matukio yanatokea...
Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya ACT Wazalendo, Abdul Nondo, anatoa tamko muda huu kuhusu kutekwa kwake Stendi ya Magufuli.
Fuatilia hapa akitoa tamko lake
https://www.youtube.com/live/LyTw1PpXT4I?si=Ze8FhWkwx-7UfKkb
"Baada ya kutekwa katika stendi ya Magufuli mashuhuda waliotoa taarifa ndio...
Jeshi la Polisi limetoa taarifa ya kupatikana kwa Mtangazaji wa TV 3, Gwamaka Francis Gehas maarufu kama 'Boiboi Mkali' mkazi wa Mbezi Beach Africana, Dar es Salaam, aliyedaiwa kupotea tarehe 3 Januari, 2025 amepatikana akiwa kwa shangazi yake Kitunda, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ya...
Wakuu,
Hivi karibuni kama mmefatilia kwenye matukio haya ya kupotea/kutekwa na watu wasiyojulikana mtagundua kuna kitu, kuna pattern inatengezwa kuisafisha serikali na vyombo vya ulinzi, kwa kufanya kuwa wote waliotekwa wameamua kujificha wao wenyewe kutokana na sababu mbalimbali. Wakienda...
Mwandishi wa Habari Eugen Peter anatafutwa na Familia yake pamoja na Ofisi yake ya Ayo TV Dar es salaam baada ya kutoweka bila kujulikana alipo leo ikiwa ni siku ya tisa.
Mara ya mwisho Eugene alionekana mazingira ya nyumbani kwake Jumapili December 29,2024 majira ya saa mbili usiku.
Familia...
Nimepokea taarifa usiku huu kutoka kijijini Kishanje, Bugabo Bukoba, akitaarifu kutekwa kwa kijana Danstan Daudi Mutajura (pichani juu) anayefanya kazi Jijini Dar es Salaam.
Dastan ametekwa jana majira ya saa 4 asubuhi maeneo ya Sigara, TANESCO, Buza Jijini Dar es Salaam wakati akienda kazini...
Wakuu,
Kama mnavyojua watuhumiwa wa tukio la utekaji wa Talimo kule Kilivya, Benki na wenzake 5 walikamatwa Disemba 4 na kufikishwa mahakamani Disemba 6.
Ikumbukwe kuwa dhamana yao ilikuwa wazi kwa masharati ya kulipa Bondi ya Shilingi Milioni 10 na wadhamini wawili kwa Kila mmoja, pamoja na...
Leo Disemba 16, 2024, zinatimia siku 100 tangu aliyekuwa mwanasiasa mwandamizi wa chama cha upinzani cha CHADEMA, Ali Mohamed Kibao, alipotekwa Septemba 6, 2024, na mwili wake kupatikana Ununio, Dar es Salaam, Septemba 7, 2024, akiwa ameuwawa huku mwili wake ukiwa umeharibiwa vibaya.
Tukio hilo...
Mwili wa Mfanyabiashara aliyeripotiwa kupotea tangu December 11,2024 Jijini Dar es salaaam, Daisle Simon Ulomi, umekutwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwanyamala huku Uongozi wa Hospitali hiyo ukisema Ulomi afikishwa Hospitalini hapo December 11,2024 majira ya jioni akiwa ameshafariki na...
Mfanyabiashara Daisle Simon Ulomi, aliyepotea tangu Desemba 11, 2024 amekutwa amekufa na mwili wake kukutwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam.
Ulomi aliyekuwa akifanya biashara za fedha za mitandao ya simu maeneo yaa Sinza Kijiweni na Mwenge alipotea tangu 11...
Jeshi la Polisi limetoa ushahidi wa awali kuhusu kupitea Kwa bwana harasi mara baada ya kumaliza harusi.
Polisi wanadai ushahidi wa awali unaonesha bwana Masawe aliyepotea Aliuza gari aliyokodi Ili Kulipa Madeni na kwamba Polisi wanaendelea kukusanya taarifa Ili Kubaini kama bwana Masawe...
Elizabeth Munisi ambaye ni Mke wa Mfanyabiashara aliyepotea tangu December 11,2024 Jijini Dar es salaaam, Daisle Simon Ulomi, ameiomba Serikali kupitia Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuendelea na uchunguzi huku pia akiwasihi Wadau wa Haki za Binadamu na Watanzania wote kuendelea kupaza sauti ili...
Baada ya taarifa za kupotea kwa Mfanyabiashara Daisle Simon Ulomi ambaye hakurudi nyumbani kwake toka alipoingia kazini December 11, 2024 Jijini Dar es salaam, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema haihusiki na swala la kupotea kwa Mfanyabiashara huyo.
Taarifa hii ya TRA inakuja baada ya...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.