Katika hotuba ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kuhusu mapitio ya serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya waziri mkuu na ofisi ya bunge kwa mwaka 2023/2024 amesema mikopo inayotolewa na benki ya maendeleo ya kilimo imetoa shilingi bilioni 78.54 kwa wakulima 119,797...