Mke wangu aniamsha, usiku saa sita,
Machozi aomboleza, simu anonyesha,
Habari mbaya napata, usingizi unakata,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa.
Tarehe kumi na tano, ndoto ninaota,
Aniijia Raila Amolo, machozi analia,
Dola toa tangazo, tarehe kumi na saba,
Akili yangu kataa, Magufuli amekufa...