Salamu waja.
Waraka huu utumike kama mashitaka kwa binadamu kwa kushindwa kuishi kwenye daraja la ustaarabu wake, kushindwa kuwajibika na kutumia vyema vipawa alivyozawadiwa na asili. Namtuhumu binadamu kwa kuwa kiumbe mbaya sio tu kwa wanyama wengine na mazingira, bali hata kwa binadamu...