Aliyekuwa Naibu Rais wa Jamhuri ya Kenya Rigathi Gachagua, amesema kuwa kuna kitengo cha siri ambacho kinapanga utekaji nyara wa vijana ambao umekua ukiripotiwa nchini humo, ambapo watu 7 wakiwa wameripotiwa kutekwa na watu wanaoaminika kuwa maafisa wa Usalama siku za hivi huko nchini Kenya.