Kocha mkuu wa Simba, Robertinho amewataka mabosi wa klabu hiyo kusajili wachezaji watano muhimu ambao ni mshambuliaji, kiungo mkabaji, beki wa kati, winga na beki wa pembeni mmoja ili waweze kutoboa kwenye michuano mbalimbali inayowakabili msimu ujao.