Majeruhi watano kati ya sita wa ajali iliyohusisha bodaboda, bajaji na gari dogo aina ya IST wamefariki dunia leo wakati wakipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.
Majeruhi hao walipata ajali jana Aprili 25, 2023 katika eneo la TRM, Kihesa Kilolo, Manispaa ya Iringa...