Wapo watu ambao hufurahi wanaposifiwa kwa kila jema na zuri watendalo. Hili ni jambo zuri tu. Pia, wapo ambao huwa hawapendi sifa hata kama wakifanya mambo makubwa na mazuri. Hawa ni wachache. Kwa wenye busara, unaposifiwa sana lazima ujiulize. Ya kweli haya? Maana, ngoma ikivuma sana hupasuka...