03/03/2018 Dunia itasimama kupisha pambano hili la Deontay Wilder (BronzeBomber) na Luis Ortiz lipite

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189

Tarehe 03/03/2018 ndio tarehe rasmi ambapo ule ubishani pamoja na tambo zinazoendelea kwa kila kati ya Deontay Wilder (BronzeBomber) na Luis Ortiz (King Kong).
Hili pambano lilibidi lipigwe tangu mwaka jana kabla ya Wilder hajapanda ulingoni kuzichapa na Stivern 2 ila ilishindikana kutokana na shutuma zilizomkabili King Kong kipindi hicho kwamba anatumia madawa ya kuongeza nguvu na King Kong almanusura afungiwe kucheza boxing kwa kipindi kirefu hata hivyo hizo shutuma baadaye zilikuja kuonekana hazina ukweli na pambano la Wilder na King Kong likaandaliwa upya ambalo hatimaye vigongo hawa wawili watakutana tarehe 03/03 kuonesahana nani ni mbabe kuliko mwenzake.

Kwa ujumla wote wana rekodi ya undefeated , Wilder ana 39 -0-0(38kos) na King Kong ana 27-0-0(23kos) sasa je nani ataendelea kushika rekodi ya kuwa undefeated???????

Majibu yote tutayapata 03/03/2018 katika ukumbi wa Barcalys center Ney York city.

Deontay Wilder inabidi ashinde pambano hili ili asubirie pambano kati yake na Anthony Joshua ila kwa kigezo cha Joshua na yeye ashinde pambano lake dhidi ya Parker .

Wilder katika mapambano yake yote aliyocheza , ukimtoa Stiverne hakuna mpinzani wake yoyote aliyefanikiwa kumaliza hata round 03 za mchezo wapinzani wake wote wakijitahidi sana wanakwamia kwenye dakika 3.00 na 90% ya waliobaki hawakuweza kumaliza hata dakika moja .

Stiverne katika pambano la kwanza alifanikiwa kucheza round zote 12 ila alipigwa kwa Unanimous decision na pambano la marudiano hakuweza kufikisha hata round 3

Wilder pia amekuwa akilalamika kwa miaka mitatu sasa kwamba AJ anamuogopa ndio maana anatafuta visingizio vingi ili akwepe kupanda naye ulingoni.
 
.sio fair kupambanisha bondia wa 40 yrs na 30 yrs aliye kwenye kiwango cha juu tena master wa style ya orthodox? ..otriz atapigwa hapa ili watu watengeneze pesa kwa kuwakutanisha wilder na joshua
 
.sio fair kupambanisha bondia wa 40 yrs na 30 yrs aliye kwenye kiwango cha juu tena master wa style ya orthodox? ..otriz atapigwa hapa ili watu watengeneze pesa kwa kuwakutanisha king kong na joshua
Ortiz ndio huyohuyo King kong
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…