Vijana nchi zote huwa na tamaa ya kutaka kutoka, ni jambo la kawaida, hata Bongo kuna madogo mamilioni wanatamani sana kwenda Marekani wakaishi huko na akina Jay Z, Nick Minaj n.k.
Hata mimi enzi nikiwa kijana nlitamani sana kwenda majuu maana movie zilikua zinatupa picha nzuri nzuri, lakini ukikua ndio unatambua umuhimu wa kubaki nyumbani na kuijenga nchi yako.
Leo hii mimi hata hapa jirani nchi kama ya Tanzania nikienda huwa naharakisha shughuli zangu nirudi mara moja kwa familia yangu, watu wetu na nchi yangu, nihusike kuijenga bati kwa bati, tofali kwa tofali, hatua kwa hatua, iwe kwa mifoleni ya magari, iwe kwa mvua au jua kali, tutaijenga nchi na haitokuja siku niikimbie, humu humu tu kitaeleweka, bendera yangu na wimbo wa taifa letu tukufu na nyama choma, kachumbari, matembele, mabamia, sukuma wiki na ugali, mke mmoja mrembo anayefahamika!!!!, watoto wenye akili na uwezo mkubwa, lugha yangu ya asili ya Kikikuyu, lugha nne za asili Kiluhya, Kijaluo, Kikamba, Kikisii lugha za kuja kama Kiswahili, Kingereza ndio zangu mbele kwa mbele, sababu kibao za kumshukuru Mungu kwa baraka zote hizi.
Na kila wikendi nakutana na washkaji kwenye bendi tunaambizana mbili tatu huku tukicheza zilizopendwa...... Afrika tamu, Kenya haitokuja siku niiache.