Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 1,117
- 3,153
Wakristo wa Ulaya walitusamehe nusu ya deni la taifa mwaka 2000, ila hivi sasa tunaelekea kuvunja rekodi ya kukopa kama vile nchi inaisha kesho.
Tukumbuke tuna watoto na wajukuu watakaohitaji kuishi katika nchi hii. Mikopo tunayokopa leo huku Waziri wa Fedha akitabasamu akiwa na afya tele, italeta balaa kwa nchi yetu hapo kesho. Mjomba mzungu aliyetusamehe mwaka 2000 hayupo tena.
Sasa hivi tunakopa kwa Mchina na Mwarabu. Hatari, Mwarabu asivyo na adabu ataomba taarabu. Swali ni hili: huyu dalali anayetudalalia usiku na mchana tuchukue mikopo ni nani?
Na ile ten percent ya hiyo mikopo anachukua nani hata kama rate ya mikopo si rafiki kwa ustawi wa nchi yetu?