15 Julai, 2021; Hayati Magufuli atakumbukwa kwa kasi sana na watu wa kada zote

15 Julai, 2021; Hayati Magufuli atakumbukwa kwa kasi sana na watu wa kada zote

Kuna mbunge mpumbavu alijisifu bungeni akisema bajeti yake kwa mwezi kwa ajili ya vocha ni 50k lakini mimi mwananchi wa kawaida bajeti yangu ya mwezi kwa ajili ya vocha ni 1k, nikipata sms za mwezi ndo imetoka hiyooooooo mpaka mwezi ujao na bado nikatwe kodi

Kmmke yule mbunge.
Hapo kwenye 50k na 1k. Unamaanisha nini au shilingi ngapi?
 
Kwa kweli nisiwe mnafiki. Niliacha kupenda siasa toka baadhi ya wapinzani kuanza kuunga mkono juhudi za JPM. Marufuku ya siasa ikachangia pia. Utendaji wa hayati nao nikaupenda.

Kilichonifanya nisimpende Magufuli baadae ni hali ya mgawanyiko uliokuwa unaendelea nchini.

Haya ni Rais wetu JPM katangulia wapo waliofurahi na wapo waliosikitika pia.

Baada ya serikali ya awamu ya sita kuchukua hatamu na kuanza kufungulia mambo mengi yalifungwa na kurekebisha uhusiano na majirani, wapinzani, wafanyabishara na wafanyakazi kuongezewa mishahara,nchi ilikuwa kama umepata uhuru toka kwa mkoloni mweusi. Mama akapendwa na watu wote bila kuangalia itikadi yao.

Mara baada ya siku 100 kufika kauli yake kuhusu wapinzani na katiba mpya ikawatisha baadhi ya wananchi. Lakini bado hakupoteza mvuto.

BAJETI MPYA YA 2021-2022 YAMWARIBIA
Hapa ni lazima Hayati Magufuli akumbukwe na wote sababu alidaiwa kuwajali wanyonge zaidi kuliko matajiri. Bajeti iliyopitishwa na waziri wa fedha Mwigulu Lameck Nchemba ndio mtihani wa pili kwa Rais SSH baada ya dai la katiba mpya.

Huenda akaponzwa na waziri wa fedha lakini atabeba lawama yeye sababu yeye ndie alimteua na anaweza pia kumuwajibisha.

Je, kwa mabadiliko haya 2025 atatoboa?

USHAURI WANGU KWAKE
Pamoja na miradi mikubwa aliyokuwa amefanya mtangulizi wake haya maisha hayakuepo? Je kweli serikali imekosa chanzo kingine cha kuongeza mapata badala ya huduma zinazotumiwa zaidi na wananchi wa kawaida? Kwanini wasingebana kwenye vitu vya anasa kama alivyofanya Magufuli?

Je, ni Serikali kukamua wananchi kama njia ya kujiongezea mapato? Hakuna rasilimali zinazoweza kutumiwa kuiongezea serikali mapato?
Jasmoni Tegga kazi imeanza
 
Hapo kwenye 50k na 1k. Unamaanisha nini au shilingi ngapi?
Mkuu hujasoma shule nini? Hilo neno ni common sana sikuhizi! K ni kiwakilishi cha kiwango cha elfu 1 ama 1000! Utakapoona namba yeyote ikifuatiwa na neno k basi zidisha hio namba mara 1000 ndipo utapata jibu halisi!
Kwa minajili hio 50k ni sawa na 50x1000=50,000
1k ni sawa na 1x1000=1,000
 
Alimuua nani kwenye familia yako?
Dhalimu mwendakuzimu ndiye alikuwa kamanda mkuu wa jeshi la wasiojulikana lililoteka, kutesa, kumiminia risasi na kuwapoteza Watanzania ambao hawakumuunga mkono na kwa uovu wake huo akapewa adhabu stahiki ya kupelekwa jehanum anakoteseka kama alivyowatesa wengine.
 
Mkuu hujasoma shule nini? Hilo neno ni common sana sikuhizi! K ni kiwakilishi cha kiwango cha elfu 1 ama 1000! Utakapoona namba yeyote ikifuatiwa na neno k basi zidisha hio namba mara 1000 ndipo utapata jibu halisi!
Kwa minajili hio 50k ni sawa na 50x1000=50,000
1k ni sawa na 1x1000=1,000
Atakuwa aliielewa kivingine, labda; kaharibiwa na mitandao huyu 🙂 🙂 🙂
 
Atakumbukwa kwa
1) Kuwanyima watumishi nyongeza ya mishahara na madaraja kwa miaka kibao
2) Kuwanyima watumishi wa umma haki ya kuhama
3) Kuwakatalia wanufaika wa bodi ya mikopo kuwaondolea VRF
4) Kwa ukabila aliokuwa anaanza kupandikiza
5) Kwa chuki za kisiasa zilizokuwa zimeanza kushamiri. Apumzike kwa amani Magufuli.
=Kwa hayo hatuta msahau
Mh Samia ni zaidi ya kijito cha maji jangwani, ametufuta machozi na kuanza kutuondolea makovu mioyoni.
Pole sana najua alimpiga chini mjomba wako Bungara na wewe mwenye vyeti feki!
 
Dhalimu mwendakuzimu ndiye alikuwa kamanda mkuu wa jeshi la wasiojulikana lililoteka, kutesa, kumiminia risasi na kuwapoteza Watanzania ambao hawakumuunga mkono na kwa uovu wake huo akapewa adhabu stahiki ya kupelekwa jehanum anakoteseka kama alivyowatesa wengine.
Sawa vyeti feki ulitegemea utadumu kwa nguvu za ndumba ofisini😂???
 
Kuna mbunge mpumbavu alijisifu bungeni akisema bajeti yake kwa mwezi kwa ajili ya vocha ni 50k lakini mimi mwananchi wa kawaida bajeti yangu ya mwezi kwa ajili ya vocha ni 1k, nikipata sms za mwezi ndo imetoka hiyooooooo mpaka mwezi ujao na bado nikatwe kodi

Kmmke yule mbunge.
Mbunge si fisadi namba moja😅😅😅 halafu wanajiona wapo sahihi mno!
 
Back
Top Bottom