15 November ...snowhite alizaliwa!

15 November ...snowhite alizaliwa!

rafiki na wapendwa wangu!leo ni siku yangu ya kuzaliwa

Namshukuru sana MUUMBA kwa baraka na baraka tele alizonijalia na pumzi anazonijaalia toka nilipozaliwa mpaka sasa

HAKIKA SIFA NA UTUKUFU NI WAKE

Namshukuru sana mama yangu kwa kunizaa na kunilea toka nikiwa tumboni mpaka aliponiacha na kurudi kwa Muumba wake,natamani sana angepata heri ya kuniona nikiwa sasa mama, mke najua na naamini angejivunia sana mimi

HAKIKA NAKUPENDA NA KUKUMBUKA SANA MAMA YANGU

Namshukuru sana baba yangu kwa kunileta duniani na kunilea, yeye amekuwa nguzo yangu na amani yangu mpaka aliponiacha naye kumrudi kwa Muumba wake, naye natamani sana angenishuhudia leo nikiwa ni mwanamke jasiri na shupavu kama alivopenda niwe

HAKIKA I MISS YU daddy,(mwenyewe alikuwa ananiita mama yangu coz nilipewa jina la bibi yangu)

Namshukuru sana mume wangu, amekuwa ni rafiki mpenzi kwa maisha yangu miaka 17 pamoja naye haikuwahi kuwa majuto kwenye maisha yangu!

HAKIKA NAKUPENDA UPEO MAISHA YANGU!(mie humwita NAFSI YANGU MIMI)

Nawashukuru sana watoto wangu, wamekuwa furaha na faraja ya pekee sana kwa maisha yangu wamekuwa zaidi ya watoto wangu, infanct ni mashosti zangu, nawapenda sana na hawajanidissappoint as a mother! I'm very proud of them

HAKIKA NAMASHUKURU MUNGU KWA AJILI YAO

Nawashukuru sana dada zangu,kaka zangu
najua nilivyokuwa mtundu na wa kudeka enzi hizo

MUNGU AWABARIKI SANA KWA KUNIFUNDISHA YOTE!tatizo tu hesabu ndo zilikataa kupanda!

JF friends!
You guys sijui niseme nini kuonyesha kuwa nawapenda sana kila mmoja kwa nafasi na upekee wake FP we unajua ni dada mkubwa, thank you very much for being one gfsonwin weye mwali hata sina maneno ya kukwambia, thank yu very much The Boss we ni big brother si unajua? Ahsante sana kwa kuwa hivyo Ciello wewe ni mamduchu enh? Yap i love you dogo BAK hujawahi kunidisappoint kwenye upande wa miburudiko ahsante brother Boflo ah we mtu sijui nisemeje, jua tu unanipa cheko na bashasha kwa post zako, af nakumbushia ile offer yangu ya massage treat! cacico mke mwenza we wajua vile u remind of those days! SnowBall mtoto wa kiume wa mama yangu thank yu pacha watu8 ahahahahhahhaha ahsante sana kwa mambo yetu yaleeee! Hujawahi kuniangusha si unajua? Kaizer na Asprin mimi proud being ur mwalimu bana lara 1 kino gal, hujawahi kunibore kwa uandishi wako, I like ur style girl!
MJ'r partner shukrani sana kwa kushare nami interest kwenye ushairi Kongosho bi harusi wangu, mimi love you kwa kweli, na ahid ya glambox lazima niitimize Zinduna Madame B , mwaJ na King'asti ndani ya chama letu kubwa nawapenda sana mashosti Mtambuzi mume ya mama ngina wewe lol!ahahahhahhhha love yu sana bana Dark City,HORSE POWER na Mkusa hongera sana kwa mawazo yenu

Well idadi ni kubwa saaaan nashindwa kuimaliza. Wengine woote NAWAPENDA SANA SANA SANA SANA!

Hongera sana kwa kusherehekea siku ya kuzaliwa kwetu! Kumbe tumezaliwa tarehe moja! Hongera sana!
 
Last edited by a moderator:
Kitendo cha cacico kupigwa ban kime7bisha babu Asprin atokwe machozi.

crying-man-11.jpg
 
Last edited by a moderator:
Last edited by a moderator:
Ooh dear, hii imenitoa machozi. This far God has brought you, and He will take you higher than the clouds. Miaka 17? Ndo maana una mauzoefu eeh, ntakuja kwa ushauri nasaha manake nimewaza kumpiga chini Paw nihamie chimbo lingine, kumbe yanawezekana.

Love you gal, hongera na furahia one more year of wisdom
Ahsante mwaya nimefurahi kwa kukugusa!usimoige chuni Paw gangamala nae mwenyewe utaona raha shosti wangu!
love yu sana gal!sana!
 
Last edited by a moderator:
Heri ya kuzaliwa mwalimu wangu snowhite! Una kila sababu ya kisherekea hii siku. Mi ntakuja na kreti mbili za biya Asprin atabeba konyagi tusherekeeeeeee!

Love u mwalimu! Uishi miaka mia nane!!
 
Last edited by a moderator:
Na maanisha ndoa itumike wakati wote kama ulikuwa utumii ipasavyo inabidi uongeze! Unaweza usitumie chakula lakini usipotumia ndoa ipasavyo ni case!
WA KUACHA KUITUMIA NDOA IPASAVYO NANI HAPA!?mie huyu?ahahahhahahhaha we nna njaa sifai !labda unipe case nyingine lakini hilo la kuitumia ndoa!lol natiii kiu yangu barabara!
shikamoo kwake mheshimiwa mume wangu!
 
Heri ya kuzaliwa mwalimu wangu snowhite! Una kila sababu ya kisherekea hii siku. Mi ntakuja na kreti mbili za biya Asprin atabeba konyagi tusherekeeeeeee!

Love u mwalimu! Uishi miaka mia nane!!
ahsante sana mwanafunzi wangu!
mimi love yu sana jamani,proud being ur mwalimu si wajua!
sema Asprin tu ndo anapiga kelele darasani vinginevyo ah!tushamaliza syllabus siku nyiingi!
akija na hizo nyagi uhakikishe umekuja na fimbo kabisa ili akileta tu fujo!tunatema mate tunamchapa
 
Last edited by a moderator:
May you live a 100 years with the same fun and attitude as you do now. Happy Birthday!
baby-beer-drinking.jpg unakumbuka enzi zako??
 
ahahahahhahhahaa nilikuwa noumer weh!najikumbuka sana!kuna watu leo wakioniona nilivyo hubaki kucheka tu eti na ni nimekuwa mkubwa nina watot kabisa lol!

aahh kweli mi siamini kama mvi zimeanza kuota, maisha yanakwenda kasi mno.. natamani kweli nirudi niwe na miaka 18 nianze bata upyaa
 
aahh kweli mi siamini kama mvi zimeanza kuota, maisha yanakwenda kasi mno.. natamani kweli nirudi niwe na miaka 18 nianze bata upyaa

wala si utani wangu!
hamna age naitamani kama nilivokuwa FORM SIX LEAVER!dah!
 
happy birthday 'mdogo wangu' wa kabila moja, ingawa mi ni wa kumbinga
 
Back
Top Bottom