16 Wauwawa kwa Kucharangwa Mapanga Usiku wa Manane-Musoma


Mshamalizana usiongelee siasa hii ni mambo ya watu binafsi...Kuua koo ingine tena watu wengi mpaka na watoto...huwezi kuandika kwa maneno mekundu humu...kitendo hiki hakikubaliki hata kama kimeshatokea.
 


Kila mkoa unavituko wala msitake kuwa undermine wananchi wa mara ndani ya tz labda muwa undermine nje ya tz.
Na hata hivyo sisemi kwamba ni sawa wanachofanya, nakipinga kwa nguvu zote na kukikemea kwa hasira zote.

Mbona mbeya hamuwashangai kwa kuchuna watu ngozi.?

Tatizo la mara limejengeka toka enzi na enzi, na limejengeka toka wakati wa mwalimu na tabia hii ilianza hasa wamasai wanapodai ng'ombe zote ni zao na kuja kuchukuwa( si kuiba )ng'ombe zao kutoka kwa watu wa mara na shinyanga wanyatunzu.

serikali zote zilishindwa kuchukuwa hatuwa yani kuanzia serikali ile ya mwalimu hadi leo, basi wananchi wakaunda umoja wa kwamba ng'ombe zinapoibiwa kijana kuanzia miaka 18 lazima aende kuzifuatilia.

Namnapowakuta wamasai wanang'ombe zenu unafikiri watawaachia kiraahisi? lazima mtapigana tu, kwa mapanga ,mikuki na hata silaha za motto.

Sasa ikaja kuonekana kuwa wamasai ni strong na wana tactic za mapigano ya namna hiyo na ikafika wakati kuwa ukiweza kumuuwa mmsai mmoja basi wewe ni kidume wanakufanyia hata tafrija.

Tabia hiyo ikaendelea kwa mwizi mmoja wa ng'ombe kumuuwa ,unaonekana kidume na unafanyiwa sherehe, sasa tabia inapotumika siku nyingi inakuwa tamaduni.

Kinachotokea leo kuuwa koo nzima ni moja ya mbinu ya wizi kuchukuwa ng'ombe kirahisi yani ya kwamba wizi wanapokuja kutoka ngambo fulani wanapovamia kijiji ni kabla hamjajiandaa wanauwa kwanza ili mshindwe kuji organize kuwafuatilia na kuwapa wakati mgumu pindi wanapoondoka na ng'ombe.

Hii tabia ya kuuwa jamii nzima kabla ya kupora mifugo imeanzia huko kenya rift valley na ethiopia.
Hivyo wanaouwa namna hiyo mara nyingi ni majirani ya wanatoka nchi jirani.kwa hiyo msiwalaumu tu watu wa mara yawezekana kabisa wauwaji ni wafugaji wezi kutoka kenya.
 
Haya, watu wameguswa pabaya. Wachagga wakishambuliwa humu hamna wa kuwatetea...mkuki kwa nguruwe...
 
Inasikitisha yaani hata kufikiria hili tukio tu mtu unahuzunika.Kama tukio hili limefanywa ili kulipiza kisasi, je na upande huu wakitaka kujibu mashambulizi?!Tunaenda wapi lakini?..Wapumzike wanapostahili!!
Ila muhimu ni kujua kuwa samaki mmoja akiharibika siyo wote!..Kuna watu wenye roho nzuri na huruma+upendo huko Mara,siyo kua wote ni watu wa hasira, chuki,ugomvi, mauaji na visasi!..
 

Kaka kama unatoke huo mkoa kataa kubali ila ukweli utabaki pale pale kwamba binaadamu wa mkoa wenu ni vichaa kabisa, binaadamu gani ambae hajali uhai wa binaadam mwenzake?? Nyinyi kwenu kuua mtu sio ishu kabisa ni kama kuua kuku tu, then unataka kufananisha na Mbeya kuchuna ngozi, kwani walichunwa watu wangapi na kwa mara ngapi, we ni mtu wa ajabu sana kutetea haya mauaji, shame on you...Umeniboa sana na hiyo post yako....WAKURYA NI BINADAMU WAKATILI tena zaidi ya hata magaidi.... Shame on you WAKURYA WOTE HUMU NDANI..I MEAN IT.
 

Hawa jamaa ni wababe sana, we acha tu. Ukiishi huko utashuhudia mengi. Kuna mkurya mmoja aliwahi kushtakiwa mahakamani kwa kumkata mtu sime kiunoni akajitetea tena bila aibu eti alikuwa anai'test' sime yake... hiki ni kisa cha kweli kabisa. Ila haya mauaji nadhani hayakutokea ukuryani .. ni maeneo ya musoma ambako wenyeji ni mchanganyiko wakwaya/wajita kwa wingi
 
nafuu cynic umesema, kwa buhare ni musoma mjini, sio rahisi ikawa kwamba ni mauaji kuhusiana na wezi wa mifugo, kwanza wajita sio wafugaji, wengi wa maeneo hayo ni wavuvi. hasa wa maeneo ya musoma, haya ni mauaji ya kigaidi tu! nafuu polis wangefanya kazi ya ziada kuwakamata hawa majambazi, inaweza kuwa ni wale maaskari/majambazi waliofanya mambo ukerewe wanalipiza kisasi! polis wachunguze kama kati ya familia hizo kuna wenye connection na mauaji ya ukerewe! ni hatari na huzuni sana raia kupotea namna hii, kuteketeza familia yote hadi watoto! sidhani kama kuna wakurya wenye roho mbaya kiasi hicho, hawa watakuwa polis/majambazi.
 
Basi kahamie Kenya!
 
Ina maana hao waliopoteza ndugu zao na wenyewe sasa wanajipanga kulipiza kisasi..
 
Sijui kwa nini lakini sioni kama serikali inalipa uzito unaostahili suala hili. Sijasikia Rais au PM wakitoa tamko na kutueleza hatua wanazochukua! Kupoteza roho za watu 17 kwa sababu yoyote ile haikubaliki.
 

Pole sana,

tatizo lako umechanganya damu ya kitanzania na ya kichina, ingawa hukupenda iwe hivyo ni wazazi wako ndio walipenda iwe hivyo.

Kabla ya kuutoa mkopo mkoa wetu kitu ambacho hakitatokea abadani, tutakutoa bure wewe kwa wachina.
 
Ni mauaji ya visasi sio ya ukoo jamani. Ni mauaji mabaya sana na hayajawahi kutokea sio tu Musoma bali hata Tanzania. Nimesikia majina kama Kawawa na familia yake yote ya watu wanane wameuawa. Tusubiri uchunguzi wa polisi utasemaje. Serikali kuanzia zile za vitongoji, mitaa/vijiji, kata, tarafa, wilaya,mikoa na hata Taifa zote zimelala. Mambo kama haya yanazuilika.
 

Matatizo yako yameanzia mbali sana,
Kamuone Dr. Ndodi akusaidie brain activater, ili kichwa yako ifanye kazi vizuri.
 
jumla ya vifo vya raia wasio na hatia ndani ya miezi miwili ni 30.
16 - Musoma, 14 Ukerewe.
hapo bado wale walioitwa majambazi - polisi wakiuwa watu wanawaita majambazi.

RIP raia mliyofikwa na mauti.
Jumlisha wale waliouawa kule Ruvuma na na wale wa mburahati.
 
Hawa watu huwa siwaelewi bse to me kama mwakaa pamoja ni ndugu.Naona kuna haja madhehebu ya dini kuongeza nguvu uko bse ata police hawatasidia bse this is deeply rooted in their hearts ie hatrage and anger
 
lakini huu ugomvi wa koo utaisha lini katika jamii zetu
mambo ya kulipizana kisasi kisa waliua ng'ombe wetu na mengineyo
tutaendelea nayo mpaka lini
inatisha na kusikitisha
 
Idiot! Go kill yourself!
 


Utaskia "MARA IWE KANDA MAALUM"

Hakuna preventation till happened!!!
 
Bahati mbaya niliwahi kukaa huo mkoa maisha ya kule yanasikitisha na kutisha watu wanakosa amani kipindi kile ikifika usiku ni hofu kwa Raia ..vifo vingi kwao si Maralia wala Huu ugonjwa wetu wao wanaongoza kwa kukatana mapanga ..wenyewe wanaita "kugechana "
damu yao imeshakuwa na sprit za kulipizana visasi toka enzi na enzi ..nini kifanyike kubadilisha haya kwa sababu yanaumiza jamii nzima ya Watanzania sio Raia wa Mara pekee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…