18% nini maana yake kwa watumishi wa umma wanaokopa kwenye bank za NMB na CRDB?

18% nini maana yake kwa watumishi wa umma wanaokopa kwenye bank za NMB na CRDB?

Mkuu nimesema hivyo kwa sababu sera za mabenki kuhusiana na riba, loan to value ratio, masharti pia yanatofautiana. Kwa hiyo each case in utofauti.

Kwa mfano mikopo ya ujenzi wa nyumba huweza kuchukua hata miaka 20 au 15 na ina masharti tofauti. Maana yake ni kwamba ukikosea kuchagua una kazi nzito kwa miaka 15 mpaka 20 ijayo.

Hata hivyo kama ni Mfanyabiashara au unakopa lufanyia biashara ni vema kuhakikisha kwamba faida uipatayo kwenye biashara inaweza kulipia ile pesa unayolipa kila mwezi. Kinyume na hapo mkopo utaogharimu biashara yako.

Pia ni vema kutembelea bank zinazokuzunguka ili kujua riba wanazotoza. Usikimbilie NMB kwa kuwa wewe ni mteja huko nenda hata FNB. Hakikisha una taarifa za msingi za mabenki yote kuhusu riba na masharti ya kila bank ili mwishoni uangalie unafuu uko wapi (hili lina umuhimu usikope kwa mazoea unaweza kuta bank ambayo huijui riba ni 16%)

Cha mwisho kama una kipato interms of Dollars kakope kwa dollar bank kwa kuwa ni cheaper sana kuliko kukopa in Tshs.
Ulishawai kukopa kwa America dollars. Au wamekusimulia kwamba ni rahisi
 
vipi unaweza kujua Islamic banking inakopeshaje? Halafu umenishauri ni ku- pm, nmeona wengi wanahitaji maarifa haya. Mie nafikiri kukopa mwakani,nataka nijifunze kwa huyu jamaa yangu aliyekopa nione namna atakavyo invest, nataka nione knowledge gap

Kwa upande wa Islamic banking sijui mfumo wao wa kukopeshana ukoje na criteria zipo vipi.
 
hapa nimekuelewa kumbe wanakokotoa kwa namna hiyo , je saccos zinaweza kumkopesha mtu hata kama si mwanachama wao?
Hapana huwezi kopeshwa.Lazima uwe mwanachama na Mkopo utapata kulingana na akiba uliyo nayo
 
20 parcent kwa mwaka mmoja...

ambayo kwa mwezi ni kama 1.7% ya principal amount uliyoikopa...

so miaka minne maana yake ni 20 *4 ambayo inaleta 80%

sema kwa sababu riba inapungua kwa jinsi principal amount inavyopungia ndio maana unaona gharama zinapungua..

ushauri mkuu kwa watu wote.. usipende kukopa bank huwa wanajali faida yao tu na riba kubwa sana bali nenda kakope saccoss
Wengine wengi wanakupa hiyo interest kwa flat rate ambayo haipungui kulingana na kupungua kwa mkopo.....kama unahitaji sana kukopa pia uliza kama hiyo interest ni flat rate au redusing balance yani inapungua jinsi unavyozidi kurudisha mkopo
 
Riba inalipwa kwa muda lets say hiyo 20% ni riba ya 20% kwa mwaka. Hesabu ziko hivi kama utakopa 10m kwa miaka miwili ila unalipa 300000 kila mwezi. Riba kwa mwezi itakuwa 20%/12 (kupata riba ya mwezi) halafu unazidisha na kiasi unachodaiwa kwenye pesa uliyokopa.

Kaa mfano huo riba itakuwa hivi:
Mwezi wa kwanza.
(20%/12) * 10m= 166,667

Mwezi wa pili.
(20%/12)* (10-makato ya mwezi wa kwanza)
0.1667 *( 10m - 133333)= 164,445

Kwa maana nyingine miezi ya kwanza utakuwa unalipa zaidi riba kuliko mkopo wenyewe. Na mikopo hii ina hssara moja ukikopa kwa muda mrefu na pesa za riba huongezeka zaidi.

Unaweza kutumia excel spread sheets kujua mkopo utakugharimu tsh ngapi jumla na kueavaluate options nafuu zaidi.
Very true niliwahi kopa NMB 6.5M nikajalipa 9M na pesa kwa muda wa miezi 60.

So muda unavyokuwa mwingi ndivyo unalipa more!
 
USHAURI MZURI KULIKO YOTE...USIKOPE KAMA HUNA BIASHARA YA KWENDA KUFANYA. UKIDHANI UTAKOPA UKANUNUE TV, SMART FONI NA SABUFA UJUWE RIBA UTAIONA KUBWA NA KUZIDI KUCHANGANYIKIWA HATA UKINYWA SUPU.
Kukopa kwa ajili ya ujenzi ni viable kiuchumi?
 
Back
Top Bottom