Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,892
- 16,476
1960s KGB CLOAK-AND-DAGGER SEXPIONAGE SPARROWS WITH LOVE FROM MOSCOW: Kisa cha Balozi Malaya wa Ufaransa na Majasusi wa Kike wa Russia (Femme Fatales)
Ninakushauri uanze kwa kusoma kwanza makala yangu hii ya zamani: K.G.B Espionage na Ujasusi kwa njia ya ngono kama silaha ya vita. Honey trap/Honeypot....Part One (1)
Larisa Kronberg enzi za ujana wake.
UTANGULIZI: Mnamo mwezi Aprili tarehe 24,mwaka 2017, vyombo vya habari vya Urusi viliripoti kwamba mwigizaji wa Soviet Larisa Kronberg alikufa huko Moscow akiwa na umri wa miaka 88. Alikuwa mhusika mkuu wa mwisho wa moja ya shughuli za kufanikiwa zaidi katika kazi za ujasusi wakati wa Vita Baridi.
Recruitment ya siri kwa balozi wa Ufaransa kwa Umoja wa Kisovieti (USSR), Maurice Dejean, kiongozi katika Upinzani wa Ufaransa wakati wa Vita vya Pili vya Dunia na rafiki wa karibu sana wa Rais wa Ufaransa kwa wakati huo bwana Charles De Gaulle.
BACK TO THE TOPIC: Ilikuwa ni mwaka wa 1964, miaka sita baada ya KGB kuweka moja ya mitego yake ya muda mrefu na yenye kina zaidi ya majasusi wa kike (honey traps/honey pot) huko Moscow dhidi ya mwanadiplomasia wa Magharibi. Operesheni hiyo ilihusisha maafisa zaidi ya 100 na maajenti wa KGB pamoja na mkuu wa Kurugenzi ya Pili, tawi linalohusika na uchunguzi na upelelezi wa ndani pamoja na ufuatiliaji wa wageni (foreign recruitment) katika Soviet Union.
Waandishi mashuhuri wa Kirusi, waigizaji, wachoraji, na wasomi, na makahaba wachache waliachukuliwa kwa jukumu hili lililojaa mikakati mingi na kabambe ambayo ipo midogo midogo pamoja na ile mikubwa mikubwa, ikihusisha mke wa Maurice Dejean na wake wa wengine. Hata Waziri Mkuu Nikita Khrushchev alichukua jukumu la kutega wale high value assets ambao yeye mwenyewe aliamuru wategwe kwa haraka sana.
Ulikuwa ni mkakati wa kutega ndoano ambao mara kwa mara ungeishia katika kutokufanikiwa, na kwa hakika KGB wasingefanikiwa kwa wakati huu lakini sio kwa huyu bwana Mfanansa anayependa sana ngono na wanawake. "Dejean alikuwa amehudumu kwa uaminifu sana na De Gaulle katika upinzani wakati wa Vita vya pili vya dunia kwanza huko chini Moroko na kisha London.
Maurice Dejean aliwahi kuwa balozi wa Ufaransa huko Prague Jamuhuri ya Czech na alifanya kazi kwa bidii ili kurejesha uhusiano wa Franco-Czech hadi mapinduzi ya kikomunisti ya mwaka 1948, ambayo Dejean alilaumi (moja kwa moja) juu ya kuhusika kwa Wasovieti. Aliongoza misheni ya Ufaransa huko Tokyo mnamo mwaka 1950; kisha alipelekwa Saigon Vietnam ambapo alitazama mapigano ya Dien Ben Phu na anguko lake kwa wapiganaji wa kikomunisti mnamo mwaka 1954 mwanzo wa mzozo ambao baadaye utaisababisha United States kuingia katika vita yake ya kwanza vya kujitakia.
Kila shirika la ujasusi hufuatilia udhaifu na mapungufu ya waajiriwa wao wa thamani na wa kiwango cha juu (potential high-level recruits.). Mara tu baada ya Dejean kufika Moscow mnamo 1955, KGB iligundua tama yake ya kupenda ngono na kufanya mapenzi na wanawake wadogo. Jenerali Oleg Gribanov, mkuu wa Kurugenzi ya Pili wa KGB (Second Chief Directorate) alikaa chini na alitengeneza mpango wa jinsi ya kutumia udhaifu wa Dejean dhidi yake na kwa maslahi ya sera za kigeni za USSR.
Mkuu wa muda mrefu wa kitengo cha kukabiliana na ujasusi (counterintelligence) wa CIA James Jesus Angleton alikuwa amemfikiria Gribanov kama mpinzani wake mkuu wa Soviet. Mahusiano yao yalionekana kuchukua kitu cha mapambano ya uwongo na kweli. Mwishowe, Angleton alifukuzwa kazi na uongozi wa CIA, ambao haukuwa na uvumilivu kwa mbinu zake za ujasusi ambazo nyingi ni za zamani na ngumu, na kushindwa kumdhibiti mpinzani wake bwana Gribanov.
Mpango wa Gribanov ulihusisha kutumia kile kinachojulikana kama "mtego wa asali" (Honey Trap) au "mtego wa kumeza" (Swallows) yaaani mwanamke mrembo ambaye angefanya ngono na Dejean kwa tishio la kufunuliwa kwa siri zake mbele ya umma, asingekuwa na njia nyingine zaidi ya kushirikiana na ajenda ya KGB. Inawezekana kwamba Larisa Kronberg alichaguliwa kwa sababu alikuwa mmoja wa waigizaji wazuri sana wa Soviet (Kama Wema Sepetu au Jokate Mwegelo) kwa wakati huo na alijulikana nchini Ufaransa pia kwa sababu alipokea tuzo katika Tamasha la Filamu ya Cannes kwa kazi aliyoifanya katika filamu ya Soviet ya 1954 iliyojulikana kwa jina la "A Big Family."
Yote yalianza mnamo mwaka wa 1956, mwaka wa Mapinduzi ya huko Hungar, katika Hoteli ya Moskva, na Colonel wa KGB bwana Leonid Kunavin akimuamuru mmoja wa wasaidizi wake kwamba Dejean alikuwa lengo kuu la recruitment, kutokana na ukaribu wake na Rais De Gaulle na uwezekano kwamba Maurice Dejean alikuwa njiani kuitawala Ufaransa.
Agizo lilikuwa linatoka juu sana. Nikita Sergeyevich [Khrushchev] mwenyewe alikuwa anataka akamatwe/ategwe. Matumizi ya Kronberg kama muwindaji yalikuwa ya kijanja na yenye busara, kutokana na uaminifu wake katika kazi na mfumo wa mazingira wa Soviet Moscow.
Mzaliwa wa Tbilisi, alikuwa mtoto wa mchoraji maarufu wa Georgia ambaye aliwahi kufanya picha ya Lavrenty Beria ambayo mkuu wa mwisho wa usalama wa Stalin alipendwa sana, alikuwa na nakala zilizotengenezwa na kuzungukwa makao makuu ya huduma ya usalama Lubyanka hadi, kwa kweli, Beria alitakaswa na Khrushchev kufuatia kifo cha Stalin.
Maurice Dejean na Kronberg walijuana na kutambulishwa kila mmoja na marafiki wa pande zote, Dejean na Kronberg walianza kutumia muda mwingi pamoja, na wakati, fulani mnamo mwaka 1958, mke wa Dejean alikuwa nje ya Urusi, Gribanov aliamua sasa kuwa ni wakati muafaka wa kufyatua mtego kwa kumshika Dejean na Kronberg wakiwa huko faragha wakifanya majamboz ya kikubwa.
Kulingana na maelezo ambayo yalipatikana inasemekana ya kwamba maafisa wawili wa KGB, mmoja akicheza sehemu ya mume wa Kronberg mwenye wivu kwa mkewe na mwingine sehemu ya shahidi, na wote kwa pamoja walivunja nyumba ambayo Dejean na Kronberg walikuwa wanafanya ngono na walifanya tukio hilo kwa hasira sana. Mume huyo fake alitishia kwamba atamshtaki Dejean kwa polisi wa Soviet, lakini, kulingana na hali ya kisiasa ya wakati ule, Dejean aliruhusiwa kutoroka kutoka huko ghorofani na kuelekea ubalozi wa Ufaransa.
Ilikuwa imepangwa pia ya kwamba jioni hiyo hiyo Dejean atakuwa na mkutano uliopangwa na Gribanov ambaye alitambulishwa kwake kama mshauri wa kiongozi wa Soviet Nikita Khruschev na ambaye, kwa kubashiri tu, aliomba msaada kutoka kwa Dejean. Mengine yaliyosalia, kwa kweli, yamebaki kuwa ni historia. Vyanzo vya Urusi vinadai kwamba wakati akiwa chini ya udhibiti wa KGB, Dejean alifanikiwa kutoa siri za namna Rais de Gaulle alivyokuwa na hasira dhidi ya NATO ambazo mwishowe zilisababisha Ufaransa kujiondoa kutoka NATO military command mnamo mwaka 1966 na kuondolewa kwa Makao makuu ya NATO kutoka Paris kwenda Brussels.
Taarifa sahihi zilipofahamika huko Ulaya ya Magharibi mnamo mwaka 1964, Dejean alijiuzulu wadhifa wake huko Moscow, lakini inaonekana hakupata vikwazo vyovyote vikubwa huko Ufaransa. Inawezekana pia kwamba kiwango cha usaliti wake kilichukuliwa kuwa ni cha kiwango kidogo sana, au tayari ilijulikana kwa mamlaka za Ufaransa hata kabla ya udhalilishaji huo kuanikwa hadharani.
Inafaa kukumbuka tu ya kwamba kutoroka kwa Major wa KGB bwana Anatoly Golytsin mnamo mwezi Desemba mwaka 1961 kulisababisha kuvumbuka kwa siri nyingi kuhusiana na harakati za kujipenyeza kwa KGB katika majeshi ya usalama ya nchi za Magharibi, na muundo wa kidiplomasia. Dejean angeweza kuwa moja ya vyanzo vya KGB vilivyofichuliwa na Major Golytsin. Mwishowe, hata baada ya kujiuzulu, Dejean hakujiondoa kutoka katika kundi la marafiki wa karibu sana wa de Gaulle na baadaye akapewa uongozi wa chama cha ushirikiano wa Ufaransa na Soviet (French-Soviet cooperation) hadi alipokufa mnamo mwaka wa 1982.
Kwa upande mwingine, haijulikani ni vipi Kronberg aliweza kufanya kazi na KGB na kwa nini alikubali kuchukua jukumu la "kuwa Swallow." Vyombo vya habari vya Urusi vinaripoti kwamba kama zawadi ya kufanikisha operesheni ya Dejean, alipokea saa ya Uswisi ya dhahabu na almasi (a golden Swiss watch with diamonds)
OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU NI JUKUMU LA KILA MMOJA WETU NA UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.