1981 Israel Raid on the Reactor: Jeshi la anga la Misri linaweza kufanya shambulizi la ghafla (Blitzkrieg) kwenye bwawa la umeme huko Ethiopia?

Sawa mkuu...
Mkuu mi ni msomi kidoogo wa war tactics.
Hii blitzkrieg ni offensive tactic iliyotumiwa sana na Hitler akitumia vikosi vyake maalum, yeye akiviita Storm Troopers.
Storm Trooperswalikuwa hatari, wakisaidiwa na mizinga, Air raids na Panzer Division(vifaru).

Tatizo kubwa ya tactic hii ni yale mafanikio yake!
Logistics zinaanza kuwa shida!
Risasi na supply lines zinakuwa nyuma sana.

Chini ya Generali Paulus aliyekuwa anaogopewa sana, Wajerumani walishambulia kwa kasi ya ajabu hadi Urusi.
Vi nchi vidogo kama Poland, Chzeckoslovakia, Hungary, vilipitiwa kama mswaki hadi nchini Urusi.

Huko Urusi wakakuta ukuta unawasubiri Stalingrad.
Na hiyo tactic ya blitzkrieg ndiyo ikawa mwisho wake, baada ya ushindi wa maelfu ya kilometa.

Hapo walimkuta mbabe wa Kisoviet, Marshal Zhukov, ambaye si tu aliwazuia, bali alitayarisha mshambulizi makali yaliyoangamiza kabisa nguvu za wajerumani.

Marshal Zhukov hakupumzika mashambulizi hadi ameiteka ngome ya Hitler , huko Berlin.
 
Ufafanuzi safi sana huu mkuu...
 
Asante Rais Magufuli kwa kutupeleka Tanzania katika uchumi wa kati, Mungu akupe afya uendelee kututumikia.
 
Mkuu, njia ipi sahihi itumike katika matumizi ya maji ya mto Nile ili uhusiano miongoni mwa nchi za Africa uendelee kuwa mwema na imara?
Kiufupi ni kwamba mkataba huu wa "kipumbavu" ulisainiwa kati ya Waingereza na Wafaransa kunako mwaka 1929 ambapo Waingereza (wakiwa watawala wa Kenya, Uganda na Tanzania kuliko na vyanzo vya mto) walitaka kuchepusha mto Nile na kuupeleka Uganda ili kuwakomoa Wafaransa ambao walikuwa na bifu nao wakati wa kugombea makoloni. Mkataba huu tata unaipa Misri haki kubwa ya matumizi ya maji ya mto Nile, na kuwaacha na bumbuwazi wale wanaotumia maji hayo upande wa juu (upstream Users) ambako ndiko maji yanakotoka. Kupitia taasisi iitwayo Nile Basin Initiative (NBI) utekelezaji wa masharti ya mkataba huu unaendelezwa. Watumiaji waliopo juu kwenye vyanzo ni :-
  1. Tanzania
  2. Rwanda
  3. Burundi
  4. Uganda
  5. Kenya
Watumiaji wengine ni Misri, Sudan zote mbili na Ethiopia ambako ni chanzo cha Nile ya bluu. Kwa miaka mingi mkataba hu umekuwa ukizipiga mkwara nchi hizo hapo juu pale zinapotaka kuendeleza miradi inayotumia maji ya mto Nile. Hata Tanzania tulipochota maji kutoka ziwa Victoria kupeleka Kahama na Nzega kulikuwa na mikwara sana, ila kwa kiburi tukachota maji hayo na kuwanyweshwa Watanzania wenye kiu. Hali kadhali ule mradi wa umeme wa Rusumo unaojengwa kwa uboa kati ya Rwanda na Tanzania unasimamiwa na taasisi tajwa hapo juu, ili kuhakikisha kwamba maji yanayochotwa hayaathiri watumiaji waliopo Sudan na Misri. Sasa Misri wanatumia mto Nile kama fimbo ya kuwachapia hawa walioko huku vyanzoni. Ila wanasahau kwamba tusipolinda mazingira sisi nchi 5 wao wanakufa.
Naamini kwenye huu mgogoro watamaliza salama kwa maelewano, kwa sababu vita haitakuwa na faida kwa yeyote kati yao. Kwa sababu Misri wakiamua kulivunja bwawa la Ethiopia Kibabe, Ethiopia wanaweza kutia sumu kwenye maji pale yanapoacha nchi yao kuelekea Misri ili kuwakomoa Wamisri. Naamini kila nchi imefanya calculated RISK ya vita hii kabla wajaliamsha dude.
Nawasilisha kile ninachofahamu
 
Safi sana mkuu...
 
Hilo bwawa wakilivunja kingo maafa yake si ni balaa!

Hayo maji yatatiririka kuelekea wapi na yasilete athari?

Wangelishambulia kabla halijaanza kujazwa maji.

Mikataba yote ya enzi za mkoloni inatakiwa ipitiwe upya na wadau wa pande zote ili iendane na mahitaji ya sasa.
 
Vp kuhusiana na mikataba inayohusu mipaka baina ya nchi moja na nyingine? Nayo pia inapaswa kupitiwa upya mkuu?
 
Bila shaka wewe ni afande
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…