Common Folk
JF-Expert Member
- Nov 8, 2023
- 909
- 4,050
Mpina mwenyewe kapata nafasi ya kugombea urais ACT kwa magumashi.Kimsingi toka kuanzishwa chaguzi za mfumo wa vyama vingi mwaka 1995, CCM wamekuwa wakipitisha wagombea Urais kwa turufu za ubora wa wahusika.
Mwaka 1995 walimpitisha Mkapa, ila sote tunajua Kikwete alikuwa anaongoza kura za maoni. Busara za Nyerere zikasikilizwa Mkapa akagombea. Hiyo ndiyo ilikuwa turufu yao.
Mwaka 2005 Kikwete hakuwa na mpinzani. He was a clean sheet Presidential Material. Na ndiyo uchaguzi pekee CCM walipata kura nyingi za ushindi kwa uhalali.
Mwaka 2015 sote tunajua wajumbe wengi na raia kwa ujumla walikuwa wanamtaka Lowasa. Ila kwa sababu za kisiasa na michezo yao michafu ya nyuma ya pazia wakamkata. Turufu akawa Magufuli, mtu ambaye hakuwa anategemewa kabisa kabisa.
Hatimaye tuko 2025, mwaka ambao ndani ya CCM mgombea amepatikana kwa kuvunja zile taratibu za mwaka 1995, 2005 na 2015. Tukiuface uhalisia, ndani ya CCM na nje huku hakuna anayeelewa imekuwakuwaje, mambo yalienda ghafla bin vuup tukashangaa mgombea tayari.
Lakini tukiongea ule ukweli, mgombea wa mwaka huu siyo turufu kwa CCM. Ni mgombea ambaye hauziki ndani ya chama na hata nje ya chama.
Laiti uchaguzi ungekuwa ni wa haki na huru, Mpina wa ACT alikuwa anatosha kabisa kumshinda mbali sana. Wakitaka wathibitishe hili basi wamuachie Mpina agombee kisha kusifanyike uchakachuzi wowote, watajionea maajabu.
Kitendawili kilichobaki ni mwaka huu 2025, turufu atakuwa nani???
View attachment 3454370
View attachment 3454371
View attachment 3454372
Ya ACT tuwaachie wao, ila CCM mwaka huu wamekosa turufu kabisa.Mpina mwenyewe kapata nafasi ya kugombea urais ACT kwa magumashi.
Kanuni za ACT zinamtaka mgombea uraia awe mwanachama wao angalau mwezi mmoja kabla ya mchakato kuanza.
Mpina kawa mwanachama wa ACT August 2025.
Mchakato wa kugombea urais umetangazwa April 2025.
Mpina akikatwa na Msajili kwa sababu hakufuata kanuni za ACT utamlaumu Msajili hapo?
Hapo ndipo mnapokosea.Ya ACT tuwaachie wao, ila CCM mwaka huu wamekosa turufu kabisa.
Safari hii turufu atakuwa kiaziKimsingi toka kuanzishwa chaguzi za mfumo wa vyama vingi mwaka 1995, CCM wamekuwa wakipitisha wagombea Urais kwa turufu za ubora wa wahusika.