Car4Sale 1996 Toyota Hilux a.k.a Mkongwe yuko sokoni

Car4Sale 1996 Toyota Hilux a.k.a Mkongwe yuko sokoni

Sema sio kosa lao TRA wanaumiza wananchi kwenye kuingiza gari ukitaka kuleta gari kama hiyo utaambiwa kodi zaidi ya 22m ndio maana Tanzania magari chakavu yanaendelea kuuzwa bei kubwa sana kuliko thamani halisi ya gari lenyewe sasa hivi hata minada yao gari zipo bei juu..
Duh kazi kweli mkuu, an ukiiona gari ya 2020 Kuja juu unaona mmiliki ni Tajiri Sana,, hizi kodi zinakanda Sana na kufanya watu kununua mikweche loh!
 
Muwe mnawashauri maboss, gari imetengenezwa 1996, imeingia nchini 2008 ikiwa na miaka 12 ya kuendeshwa Japan/Europe namba AQW,nina uhakika kununua na kuitoa bandarini wakati huo haikuzidi milioni 20, imeendeshwa hapa nchini karibia miaka 18 hadi leo 2026, Ina mileage ya kilometer 180,000. Bado mnataka muiuze milioni 32!???, kwasababu ni Hilux Ina sports rims au!?, hata kama ni dalali sio kila bidhaa unapost, nyingine unaacha tu boss ajipambanie wateja wasikukariri vibaya kwamba una tamaa.
Wala Sina Tamaa Kiongozi Ila Iyo Gari Imesukwa Vizuri Sana Ukija Hata Kufanya Test Drive Hakika Utaelewa Kwanini Inauzwa Bei Iyo

Kingine Kinachofanya Ipande Bei Ni Investment Kubwa Iliyotumika Katika Kuiweka Sawa Ndio Maana Leo Hii Kuna Land Rover Za Mwaka 1990 Zinasukwa Na Kuuza Hadi Milioni 50

Sababu Nyingine Hizi Gari Kwa Sasa Ni Adimu Na Isitoshe Ni Mkataba Yaani ROHO Ya PAKA Na Kuzipata Ni Changamoto Sana Hata Huko Japan
 
Hapo ukipata wa kumkamata ni 15m.... ! Narudia tena wa kumkamata !

Madalali wapuuzi sana, mnajiongezea tu hela, huenda boss kataka hela ya kawaida nyie mnadabo kwa tamaa ! Fair play hio ni 10m
Hahahahaaaaaaa Imenibidi Kwanza Nicheke Aisee, Iyo Gari Hata Engine Yake Ukisema Uzunguke Ilala Kwaiyo 15 Milioni Huwezi Kupata Mzee Alafu Kitu Kama Hujui Ni Vyema Ukauliza Na Sio Kutoa Mapovu
 
Mkuu hayo maelezo ume Copy & Paste au umeandika mwenyewe!

Hio gari kwenye hizo picha Transmission yake ni AUTOMATIC kweli?

Kigezo gani umetumia kupata hio bei ya kuuzia.
Ni Kweli Kiongozi Ni Typing Error Kwa Sababu Huwa Tuna-Post Magari Mengi Per Day

Kigezo Cha Kwanza:

Investment Kubwa Iliyofanyika Katika Kurudisha Katika Hali Yake Ya Awali Ya Kuwa Kama Mpya Vile

Kigezo Cha Pili:

Demand Yake Kuwa Kubwa Na Isitoshe Hizo Gari Ni Adimu Na Kwa Wenye Kazi Zao Wanazitafuta Kwelikweli Ni Gari Ya Kazi

Kigezo Cha Tatu:

Ni Uimara Wake Kwa Ujumla Na Kudumu Sambamba Kabisa Na Uvumilivu Yaani Zina Shukrani
 
Ukiwa dalali uwe smart asee usiwe falafala kabisa,hivi mtu kama wewe hata ukitangaza kitu Cha maana nani atakuamini?
Jitathimini
Nimekuja Kugundua Baadhi Ya Watu Huku JF Wamekariri Haya Magari Ya Kisasa Ya Siku Hizi Lakini Kwa Sisi Tuliopo Jikoni Tunajua Ukweli Thamani Halisi Za Bei Za Magari

Sio Kosa Lako Kutukana Na Nimekusamehe Ila Wakati Mwingine Ni Vyema Ukauliza Wala Hutoonekana Mjinga
 
Sema sio kosa lao TRA wanaumiza wananchi kwenye kuingiza gari ukitaka kuleta gari kama hiyo utaambiwa kodi zaidi ya 22m ndio maana Tanzania magari chakavu yanaendelea kuuzwa bei kubwa sana kuliko thamani halisi ya gari lenyewe sasa hivi hata minada yao gari zipo bei juu..
Uko Sahihi Kabisa Ndio Maana Leo Toyota Premio Ya Mwaka 1998 Inauzwa TSH 26.8 Pamoja Na Usajili

Watu Ukija Hapa Kuwaeleza Wanaishia Kutukana Na Kutoa Mapovu Badala Ya Kuuliza
 
Hapo ukipata wa kumkamata ni 15m.... ! Narudia tena wa kumkamata !

Madalali wapuuzi sana, mnajiongezea tu hela, huenda boss kataka hela ya kawaida nyie mnadabo kwa tamaa ! Fair play hio ni 10m
Gari imetumika miaka 18 bongo iwe mln 10
 
Uko Sahihi Kabisa Ndio Maana Leo Toyota Premio Ya Mwaka 1998 Inauzwa TSH 26.8 Pamoja Na Usajili

Watu Ukija Hapa Kuwaeleza Wanaishia Kutukana Na Kutoa Mapovu Badala Ya Kuuliza
Magari yana kodi kubwa Tanzania kuliko Nchi nyingi Afrika na hata hauelewei wanafanya hivyo kwa malengo gani watu wapo busy na IST sijui paso ukiangalia gharama yake ya kuingia Tanzania kwa Nchi zingine unapata gari ya juu juu nzuri kabisa..
 
Back
Top Bottom