Dressing codes tunamaanisha nini? Aina za nguo (mishono) na vipimo vyake? Rangi? Aina za vitambaa (labda wengine wasije wakaja kazini wamevaa vyandalua!) Na zimepangwa kwa jinsia zote au ni kinamama tu wanaandamwa na sketi zao? Mie nikienda kazini na mgolole sawa? (Mzee Kawawa ndiyo ilikuwa fasheni yake miaka ya mwanzo ya uhuru).
Serikali inazungumza kuhusu mtumishi kuvaa decently, lakini imeacha hiyo term ikabakia kama relative term. Ni tofauti na dressing codes za watawa wa kike wa kikatoliki ambao wameeleza wazi katika sheria zao kuwa gauni litakuwa na urefu gani toka kwenye kiwiko cha mguu, mkanda utakuwa katikati kabisa ya kitovu na tip ya mfupa wa kati ya kifua, viatu vitakuwa vya kufunika vyenye soli ya unene gani, head scarf itapita usawa upi wa masikio na kushukia nyuma katikati ya shoulder blades na kuishia usawa wa hizo shoulder blades, nk. Askari wa majeshi yetu wako makini hadi kwenye ukubwa wa sleeves (kama ni shati short sleeve), kama ni wakati wa kukunja mikono ya shati kuna utaratibu ni mikunjo mingapi ya upana gani, na shati lililokunjwa mikono liishie usawa gani.
Huko bungeni kuna official dressing code ambayo inasimamiwa na kanuni zao, na kuna wakati nilishaona mheshimiwa spika akiwatoa nje wabunge ambao hawakuvaa ipasavyo.
Na wengine tunaotembea hapa na pale tunafahamu majina ya dress codes, ambayo ukitajiwa tu unaelewa wamesema uvaeje. Tukialikwa kwenye tafrija ama shughuli wengine huwa wanatuandikia kwenye kadi dress code, labda: "Formal", "Informal", "Business-Standard", "business-casual-corporate", "Business-Casual-Relaxed", "Smart Casual" au "casual". Na hizi zote, kila moja uvaaji wake unategemea na nchi husika, hali ya hewa ya siku hiyo, muda wa siku (smart casual ya jioni ni tofauti na smart casual ya mchana, vivyo hivyo kwa formal, relaxed etc), na jinsia ya mvaaji. Hata walioko kwenye uniformed services (majeshi, mahospitalini), wana dress code kuendana na matukio, japo wao flexibility yao si kubwa kama ya other civillian dress codes.
Kama hizo dress codes za serikalini zimepangwa kwa category kama hizi, ni vigumu kumpangia mtu avae nini. Mtu anakuwa na uhuru wa kuchagua vazi mradi liendane na dress code ya wakati na mahali. Na katika hizo nilizotaja juu ambazo zote zinakubalika, suruali na skirt kwa kinamama zipo. Labda swali, hivi skirt ya ikifika urefu wa magotini (si chini ya magoti), ni ndefu au ni fupi? Sasa suti ya kike yenye skirt hiyo, ambayo mvaaji akikaa anabana mapaja au anachora 4, katika nchi za commonwealth iko kwenye dress code ya "business standard". Na hizi kwa kinamama zina mapozi yake, huwezi tu kukaa unajichanulisha! Sasa executive wa kike akivaa hivi, na akiketi na kutembea kama inavyopaswa kwa uvaaji huo, ameharibu nini? Au sisi tuna dress code tofauti na nchi nyingine za commonwealth?