200 Mil biashara gani ya kunilipa fasta

200 Mil biashara gani ya kunilipa fasta

Sasa mkuu hapa tunadanganyana asee haiwezekani bank wakupe mil200tsh bila makablasha wala biashara ya vipi utarejesha mkopo.
Otherwise hii ni story ya kupikwa tena imetoka jikoni kijiweni kwenu...
Hakunaga hii kitu ndg make benki hawaangalii tu thamani wala uzuri wa kajumba kako bali ni namna gani umejiandaa na sababu ya kukopa kwako.
Na uwe makini mkuu isijekuwa kuna mtu ndani ya hiyo benki katamani hicho kijumba akupokonye kiaina! Shaulilo....

Mbona mgumu kuelewa? Nimesema dhamana ninayo bank wamekagua na wamesema wanaweza nipa hadi mil 200 sasa ninachofanya sasahivi ni kufanya upembuzi yakinifu ni biashara ipi naweza kufanya ili niweze rudisha mkopo ambayo nikiandika proposal itawleweka
 
Kwa jinsi kila mtu anavyotoa ideas zake inaonesha bongo biashara nyingi zialipa. Ila rate ya kushindwa kulipa mikopo benki ni kubwa sana sijui kwa nini? Mtoa mada mkopo unasaidia sana kujenga au kuimarisha biashara iliokuwa up and running,yaani una biashara na ushajua inakwendaje then unaiimarisha kwa mkopo. Ila kukopa then ukaanzishe biashara hizi zetu ndog ndogo, nyumba itaenda enda hio. Kuwa makini sana na biashara uayotaka kufanya.

Biashara zenyewe ngumu, profit kidogo sasa ukijumlisha na interest ya mkopo hali itazidi kuwa mbaya.
 
Ah we unasema nini bana..

Bongo mambo safi mno.
 
Mbona mgumu kuelewa? Nimesema dhamana ninayo bank wamekagua na wamesema wanaweza nipa hadi mil 200 sasa ninachofanya sasahivi ni kufanya upembuzi yakinifu ni biashara ipi naweza kufanya ili niweze rudisha mkopo ambayo nikiandika proposal itawleweka
Mkuu bank wamekupa uhakika wa kupata m200 kulingana na thamani ya nyumba yako lakini kamwe hawatakugrant huo mkopo ikiwa utaonesha kuteteleka/mashaka jinsi ya kurejesha pesa yao.
Hapa ugumu upo kwako, namna ya kupata mradi wa biashara yenye uhakika wa kukulipa na wakati huohuo urejeshe mkopo. Ukikurupuka kuna uwezekano mkubwa ukajikuta unatumikia mkopo au kufail kabisa.
Bado bank watahitaji kujiridhisha kama una uzoefu na biashara unatakayofanya au la watapima uwezekano wa hiyo biashara kujiendesha mpaka ukomo wa mkopo.

Labda umpate mtu aliye na biashara tayari, jiridhishe mwenyewe vyakutosha then ungana nae mkachukue mkopo huo kuliko kuanza mwenyewe biashara uliyo na ugeni nayo kabisa!

Uwe makini...
 
ulipaswa kupanga kabla hujaenda
now nafikiri uweke ukumbi wa muziki ..kama bendi hivi..
angalau hutakosa milioni kumi kila mwezi

Huo ukumbi inaTegemea na Location. Sehem itakayo mlipa ni Maeneo ya Mjini.

Je atalazimika kununua Eneo ndio ajenge ukumbi!? Au atalazimika kukodisha sehem na kuiendesha!?

Tufafanulie vizuri Mkuuu.
 
Nina nyumba ambayo bank wamekubali kunikopesha million 200, je ni biashara gani itakayo nilipa fasta yaani zaidi ya mil 10 kwa mwezi!
unaenda kukopa bila kujua biashara gani ..lol tayari ushsafeli hapo jihesabie umwewauzia bank nyumba kwa m 200
 
Mkuu mimi naona ungekopa kiasi kidogo kama 20m au 30m then inapokua iyo biashara utakayofanya ndio ukope hiyo hela biashara za nje zipo ambazo zinaweza kulipa iyo hela ila kwa ugeni wako mimi sikushauri ukope kiasi kikubwa ndio uanze...maana iyo mikopo ukipewa tuu baada ya mwezi unatakiwa uanze kuwalipa utaanza kutoa izo izo ulizokopa na kulipa wakati biashara haipo ok..
 
Huo ukumbi inaTegemea na Location. Sehem itakayo mlipa ni Maeneo ya Mjini.

Je atalazimika kununua Eneo ndio ajenge ukumbi!? Au atalazimika kukodisha sehem na kuiendesha!?

Tufafanulie vizuri Mkuuu.

Anaanza kwa kukodisha later ananunua
 
Biashara inayoweza kumtoa mtu ni kwenye manufacturing of goods...cha msingi ni kuangalia una manufacture kitu ambacho ni necessity sio luxury badala ya kukomaa na uchuuuzi wa kupata faida kwwnye kitu i.e. 1500 au 2000 kitu kinachouzwa kwa 5000 muuzaji wa jumla anaweza uza 6500 au 6000 lakini anaepiga hela hapo ni manufacturer...
 
200mil ni parefu sana kama huna biashara tayari. Ungeanzia angalau nusu yake (100mil) na ukiirudisha kwa ufanisi unafanya top up kidogo kidogo. Ningekushauri uiweke kwenye kilimo ila kiwe cha kisasa na uajiri mtaalamu. Binafsi niliwahi kukopa 80mil na zilinipeleka race sana ila namshukuru Mungu baada ya kupoteza karibu robo yake, niliweza kutuliza kichwa na kuwekeza sehemu ambapo ilinizalishia wastani wa 5.5mil kwa mwezi na nikiweza kurudisha wote ndani ya muda wa marejesho. Chamsingi uwaze kwanza pakuiwekeza na hasa investiment utakayoweza kuimudu. Siri nyingine ya mkopo mkubwa ni kwamba usiwekeze wote. Tumia japo 70% na 30% iweke kama emergency kwani lolote laweza kutokea hivyo hiyo 30% itakunyanyua pindi ukianguka. Kila la kheri mkuu.
 
Hv bongo kuna nyumba ya mil 200 kweli? Maana naona gharama zimepanda sana
 
Nondo zinamwagwa humu ndani hadi raha., ngoja mimi niwe msikilizaji
 
Mimi nimeweka hela kama hizo fixed deposit nakula kwa ulaini sana. Kwa mwaka sikosi 30m.
 
mtu unaenda kukopa milioni 200 huna hata biashara ambayo unafanya, benki wanakukopeshaje? hii ina maana hujui hata changamoto za biashara na discipline anayotakiwa kuwa nayo mfanyabiashara, halafu unachukua stake kubwa hivi?
ushauri wangu chukua milioni 10 kwanza ufanye kama pilot then uta expand kadri uzoefu wako na biashara yako itakavyokuwa, usije kulia na kuanza kusema mikopo inahusiana na freemason
 
200mil ni parefu sana kama huna biashara tayari. Ungeanzia angalau nusu yake (100mil) na ukiirudisha kwa ufanisi unafanya top up kidogo kidogo. Ningekushauri uiweke kwenye kilimo ila kiwe cha kisasa na uajiri mtaalamu. Binafsi niliwahi kukopa 80mil na zilinipeleka race sana ila namshukuru Mungu baada ya kupoteza karibu robo yake, niliweza kutuliza kichwa na kuwekeza sehemu ambapo ilinizalishia wastani wa 5.5mil kwa mwezi na nikiweza kurudisha wote ndani ya muda wa marejesho. Chamsingi uwaze kwanza pakuiwekeza na hasa investiment utakayoweza kuimudu. Siri nyingine ya mkopo mkubwa ni kwamba usiwekeze wote. Tumia japo 70% na 30% iweke kama emergency kwani lolote laweza kutokea hivyo hiyo 30% itakunyanyua pindi ukianguka. Kila la kheri mkuu.

Mkuu ni biashara gani hiyo ulifanya? Maana wengine tunazo hizo hela na wala sio za mkopo ili tujaribu. Nipm ukipenda
 
Back
Top Bottom