Fantastic Beast
Member
- Feb 18, 2019
- 53
- 539
Historia huwa ni mwalimu mzuri sana. Na hii hii historia unaweza kuitumia kujua nini kinafuata.
2000 ya Mkapa ilikuwa rahisi sana sababu kwa miaka 5 yake watu walishamuelewa na kumkubali zaidi.
2010 ya Kikwete ilikuwa mtelezo sana sababu raia walishamuelewa sana, hata wale waliokuwa hawamkubali walisharudisha imani kwake.
Kwenye chaguzi za hiyo miaka CCM walishinda kirahisi sana sababu marais walijenga chemistry nzuri na raia wao. Hata ukisikiliza kampeni zao unaona kabisa walistahili kupewa miaka mingine 5 wamalizie yale waliyoyaanzisha.
2020 ya Magufuli tayari ina dosari lukuki:
1. Sheria kandamizi kwa vyama vya upinzani. Nyingi ya hizi zimetungwa ndani ya utawala wake.
2. Sheria kandamizi kwa raia hasa sheria ya maudhui ya mtandaoni.
3. Chaguzi zisizo na haki hasa uchaguzi wa serikali za mitaa. Uhuni uliotumika huko umeonekana kuendelezwa hata kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
4. Kuzuia mikutano ya vyama pinzani. Hii imewakosesha raia haki yao ya kuinteract na vyama vyao. Hii imefanya raia mtaani kuwa na njaa ya hii mikutano sana. Kama huamini subiri kampeni zianze ujionee.
5. Kuchanganya mambo ya kitaifa na mambo ya chama tawala. Yani wanajiona kama wao ndio wenye hati miliki ya kila kitu cha nchi. Kumbukeni hata wakati wa chama kimoja kulikuwa kuna kura ya ndio & hapana na hapana zilokuwepo nyingi tuu.
Mambo ni mengi sana lkn hayo ni kwa uchache tuu.
NB: Polepole ni aibu kwa katibu mwenezi kama wewe kupanda jukwaani na kutuimbia ngojera za chama x kutokuwa na ofisi kwa miaka 25. Usisahau hata sisi huku mitaani tumezaliwa kwenye nyumba za kupanga, tumekulia kwenye nyumba za kupanga na sasa tumezeeka bado tumo kwenye hizihizi nyumba za kupanga.
Kwanza hawa waliopanga ndio wanajua maisha yetu yalivyo kuliko nyie mliozoea maghorofa yenu.
Usirudie tenaa kutuletea habari za kimbea mbea kwenye mambo ya serious. Tuambieni kwa miaka 5 mmetufanyia nini na kwa nini tuwape miama mingine mitano, fullstop.