Sijui unamaanisha kwenye ngazi ipi? Kwenye Urais hilo halina shaka ni kweli CCM watashinda. Kwenye ubunge mh??? Udiwani atleast huko viti vitapatikana maana wengi watakosa nafasi za kugombea kwenye chama chao watakwenda kugombea kwa upinzani. Binafsi naona upinzani unazidi kuwa dhaifu kadiri siku zinavyoenda. Nakumbuka wakati nipo shule tulifundishwa law of diminishing returns, yaani km ni prodn au scale of performance basi inaongezeka kwa increasing rate, then ina increase kwa decreasing na constant. Lakini kwa upinzani sasa hivi ni declining moment. Yaani wanadecrease kwa increasing rate (inatisha kidogo).
Kiujumla mafanikio ya upinzani Tanzania nayaona ni ndoto. Maana ni mfumo ambao hauna fair play na sometime naamini tumeiga demokrasia ya kimagharabi ambayo si lazima ifanye kazi katika nchi zetu. Tungeiachia nature na sio kureplicate mifumo ya watu. Binafsi naamini katika institutions imara katika nchi yetu excluding politics. Maana tunamiaka takribani 15 ya vyama vingi. Tujiulize nini mafanikio ya mifumo hii?