- Tu-support uwezo wa uongozi ushahidi upo wazi wa wanaoweza na wasioweza, kuna vijana hawafai na kuna wazee wasiofaa, JF tujiepushe na ideology za ujana na uzee maana ushahidi tunao tena mkubwa sana kwamba sio tija, kuna vijana wametuangusha na kuna wazee wametuangusha,
- Binafsi siwezi kushauri kuudwa sheria moja ya kuwazuia wazee wa CCM, na nyingine ya kuwaruhusu wazee wa Chadema, ninasema itakwua ni a National nightmare kuwakosa wazee kama Dr. Slaa na Ndesamburo bungeni kwa sababu ya hizi ideology za ujana na uzee, cha muhimu JF tukachukue fomu za kugombea, tuelimishe wananchi kuhusu viongozi wanaofaa na wasiofaa na sababu, sio maneno ya ujana na uzee!
- Hii kioo cha jamii kinapaswa kuwa bigger than hizi ideology za uzee na ujana, maana hazina nafasi katika jamii yoyote duniani inayotaka kuendelea mbele, na pia it is about time sasa taifa letu likaanza kufikiria mikakati ya kuwapatia wazee wenye elimu za juu nafasi za kuendelea kutumia elimu zao na experience zao za kazi kwa taifa, kama majuzi tumeona jinsi Mzee Kaunda alivyopewa kazi kule Boston ya kufundisha University miaka miwili na malipo mazito sana,
- Halafu pia tatizo lingine kubwa ni namna ya kuwajengea hoja nzito za kuwafanya wakubali, badala ya kutumia matusi na kejeli, na huwezi kusema mzee Slaaa, abaki lakini wazee wengine waondoke haya hayawezi kuwa mawazo ya Great Thinkers!
JF tuende kuchukua fomu za kugombea uongozi ndio dawa peke yake ya kuwajibu wazee tusiowataka!
Respect.
FMEs!