Mwanakijiji,
Narudisha tena swali langu... naona tunayoyoma tu..
Nimeandika hivi:- inanipa shida kubwa sana kutambua vita hii itaelekeza majeshi wapi..Umesema kukiondoa chama CCM madarakani sii hoja haujali ni chama gani kitaingia madarakani..wakati namsoma Mwalimu Augustine Moshi akisisitiza ni wakati wa kukiondoa chama..Hii inanikumbusha uchaguzi wa Iran.. Hivi kweli lengo la wananchi ilikuwa kumwondoa Ahmadinajad au ilikuwa kukiondoa chama tawala. Kenya na Zimbabwe kote tumeona utata uliopo ktk kumwondoa kiongozi madarakani na itakuwa vizuri tukizungumzia zaidi majeshi yetu yaelekeze nguvu zake wapi, kwa maana fupi TATIZO LIKO WAPI?..
Tatizo la kufikiria kuwa kuondoa chama kimoja kutatua tatizo/matatizo tuliyonayo kwa kukiingiza chama kingine. CCM kama chama ni umwilisho wa utawala wa kifisadi ni wabebaji wa lawama zote za matatizo ya kifisadi kwani wao ndio waliounda serikali na ajenda yao ndio serikali inatekeleza. Kukiondoa madarakani basi kitamuondoa mtu wa kumlaumu. Wakati huo huo unapoingiza chama kingine na chenyewe kitapata tendencies zile zile za vyama tawala duniani (tumeona yaliyotokea Kenya, Zambia na kwingineko).
Sasa kuna njia ya haraka ya kuondoa tatizo nalo ni kuing'oa CCM madarakani. Lakini hiloo ni sawa na mtu ambaye mguu wake umevunjika na kwa haraka watu wanaamua kukata pale juu kwenye goti na kunyofoa ile seheu yenye madhara. Lakini watashughulikia vipi tatizo la uvujaji damu, uambukizwaji kwenye kigota?
Hapa ndipo linakuja suala zima la kuangalia hii vita kwa upana wake. Majeshi ya Marekani yalipoingia Iraq yaliingia kwa mbwembwe zote za kivita na ninakumbuka siku ile sanamu ya Saddam ilivyoanguka Baghdad na kuashiria "ushindi". Kutokana na hilo GWB akasimama juu ya meli ya kivita nyuma yake bango likitanza "Mission Accomplished". Miaka nane baadaye vita inaendelea na gharama kubwa imelipwa.
Ninachosema ni kuwa CCM ilivyo sasa haipaswi na haifai kuaminiwa utawala wa nchi yetu; lakini katika kufanya hivyo tunataka kiingie nini na nani na kwa nini?
Hapa linakuja suala la Ajenda.
Umesema hapo mwisho:
1. Je, kumwondoa JK Ikulu itaondoa uongozi mbaya.
Siyo lazima ni sawa na kumuondoa Kaunda na kumuingiza Chiluba. It has to be more than removing an individual.
2. Je, kukiondoa chama CCM madarakani (Ubunge) kutapunguza nguvu ya rais ktk kuchagua viongozi wabovu?..
Hapana kwani nguvu ya Rais kuchagua viongozi (wabovu au wazuri) haitegemei chama anachotaka; ni nguvu yake kikatiba.
3. Je, Kuondoka kwa vyote hivi viwili kutaleta Uhuru wa kweli? na Kivipi yaani..
Lengo siyo kuondoa ili visiwepo na badala yake kuingiza vingine vyenye mfanano huo huo. Lengo lazima liwe juu ya haya yote.
4. Je Huo Uongozi utakao kuja utakuwa na agenda zipi muhimu ktk kuhakikisha Uhuru wa kweli unapatikana. __________________
Huo uongozi hauwezi "kuja" na ajenda muhimu; uongozi huo unapaswa kuwa na ajenda hizo sasa. Bahati mbaya hadi hivi hakuna chama cha siasa nje ya CCM ambacho kina ajenda ya kueleweka (sizungumzii "ilani" ya uchaguzi). Mwakani ajenda ya uchaguzi itatoka kwa wananchi wenyewe. Lakini wananchi wawe na ajenda gani? Hapa ndipo ilikuwepo haja ya viongozi wa dini kwa mfano, kukaa pamoja (siyo kama walivyofanya Wakatoliki peke yao) na kutengeneza ajenda mpya ya taifa.
Siyo viongozi wa dini tu hata taasisi binafsi na makundi mbalimbali ya wananchi wanaweza kuwa na ajenda ambayo wanaweza kuipendekeza kuwa ni ajenda ya taifa. Hii JF inaweza ikatengeneza ajenda yake na kuiuza kuwa ni ajenda ya wananchi. Viongozi wanaotaka kutuongoza 2010 itapaswa wakubaliane kwa asilimia 100 na ajenda hiyo.