2010: Pamoja Tunaweza

IJUMAA iliyopita, Rais Jakaya Kikwete aliandaa hafla maalumu ya kukaribisha Mwaka Mpya kwa mabalozi wanaowakilisha nchi zao Tanzania, iliyofanyika Ikulu ya Dar es Salaam na ambayo huifanya kila mwaka kama ada.

Akizungumza na mabalozi hao katika salamu zake za Mwaka Mpya kwao, pamoja na mambo mengine, Rais alisisitiza wawakilishi hao wa nchi hizo kuzingatia kuwa mwaka huu ni wa uchaguzi nchini, na asingetarajia kuwaona wakijiegemeza katika vyama vya siasa au wagombea.

Bila kutafuna maneno, Rais aliwaambia mabalozi hao kuwa watanzania hawataki kuchaguliwa viongozi, ila wana uamuzi wao wenyewe na ridhaa ya kuona ni chama gani au kiongozi yupi anastahili kuwaongoza katika kipindi kingine cha miaka mitano.

Aliwaonya kuwa atakayekiuka dhima yake ya uwakilishi wa nchi yake, atakuwa anajihalalishia kufukuzwa nchini na atakuwa pia amemdhalilisha aliyemtuma kumwakilisha, kwani kufanya hivyo ni kukiuka kazi yake ya uanadiplomasia.

Tunampongeza Rais na kuungana naye katika kuwafahamisha mabalozi hao kuwa Tanzania ina wenyewe na kuwakaribisha kuziwakilisha nchi zao si hati ya kuwaruhusu kuingilia mambo ya ndani ya nchi kama vile wanataka kuitawala.

Diplomasia si ukoloni, hivyo balozi anapokuwa ameteuliwa na nchi yake kuiwakilisha katika nchi nyingine, atambue kuwa anakwenda huko si kuiamrisha, kuiagiza au kuielekeza kufanya hiki au kile, la hasha, jukumu lake ni kujenga na kuimarisha uhusiano uliopo.

Kazi na wajibu wa balozi ni kupatanisha au kusuluhisha kama kuna mgogoro na kusababisha mambo yafanikiwe katika nchi yake au nchi aliyomo; hivyo hana haki ya kuikemea, kuigombanisha au kuikosanisha nchi anayoiwakilisha na nchi mwenyeji au kuwafarakanisha wananchi wa nchi hiyo.

Kwa kuwa huo ndiyo wajibu wake, kama alivyowaambia Rais Kikwete, basi waendelee kusaidia ili hatimaye uchaguzi nchini uwe huru na wa haki na kila upande utakaoshiriki uridhike na matokeo na kuendelea kuijenga nchi kwa pamoja.

Ilishakuwa kama kawaida kwa baadhi ya mabalozi kujisahau na kujikuta wakifanya siasa badala ya uwakilishi, na matokeo yake huegemea katika baadhi ya vyama vya siasa na hatimaye kuchangia kujenga chuki miongoni mwa wananchi.

Yawezekana misaada yao ndiyo inayowapa ‘kichwa’ cha kudhani kuwa wanaweza kuifanyia lolote nchi na kutishia kuinyima misaada kama haitatii amri, kama hiyo ndiyo imani na welewa wa baadhi ya mabalozi, basi wajue Tanzania ni 'masikini jeuri' asiyetaka kuyumbishwa.

Watanzania na hasa viongozi wa vyama vya siasa wanaodhani kuwa mambo hayaendi bila ufadhili, walisahau hilo na badala yake walinde uhuru wao wa kujiamulia mambo yao wenyewe kwa maslahi yao na kuhakikisha wanaondokana na fikra za utumwa.

Tunasema balozi ye yote atakayekiuka mwito wa Rais Kikwete, aoneshwe njia na awaache watanzania wajiamulie mambo yao ya kidemokrasia kwa kupingana bila kupigana na kuchaguana kwa uhuru na haki kama wanavyoona na kujipangia wao.

SOURCE: http://www.habarileo.co.tz/tahariri/?n=5189&cat=tahariri

SWALI: HIVI TANZANIA KUNA UCHAGUZI AU UTEUZI?

Mhariri anazungumzia demokrasia ipi? Ya kura kwa kubadilishana na khanga, wali, pombe na fulana?
 
Thank you man, we are together.
 
hakuna kulala watanzania wenzangu mpaka kieleweke, Daima mbele nyuma mwiko , pamoja tutawang'oa na kuwaondoa hawa watawala wakizazi cha ufisadi, na MUNGU atutie nguvu
 
Mnyika,
Kagombee nyumbani unakotoka. Majimbo ya Dar yanahitaji mtaji mkubwa ambao naamini huna kwa kuwa wewe sio fisadi na hauna mtandao wa kifisadi.
 
Mnyika,
Kagombee nyumbani unakotoka. Majimbo ya Dar yanahitaji mtaji mkubwa ambao naamini huna kwa kuwa wewe sio fisadi na hauna mtandao wa kifisadi.

WildCard

Asante kwa maoni yako.

Kuhusu suala la ninapotoka, wengine sisi ni machotara wa asili nyingi kwa kweli jambo ambalo nalo linachangamoto zake.

Kuhusu majimbo ya DSM kuhitaji mtaji mkubwa; je unachomaanisha ni kwamba majimbo ya DSM waachiwe matajiri ama mafisadi?

Hoja hii imebeba kwa kweli dhima ya makala yangu hapo juu; hoja yangu kubwa katika makala hiyo ni kuwa uchaguzi usichukuliwe suala la mtu binafsi. Ukisema kwamba matajiri pekee ndio wagombee, mantiki ya hoja yako ni kwamba mgombea atumie fedha zake kwenye kampeni.

Hoja ninayoijenga hapa ni kwamba kwa kuwa uongozi huu ni wa umma, lazima umma ushiriki kumweka kiongozi madarakani. Kule Marekani, Obama angetumia fedha zake binafsi asingefika pale alipofika kwa njia aliyofikia.

Sasa je, hatuwezi kuzibadili siasa za Dar es salaam zisiwe za matajiri na mafisadi pekee bali zikatazama uwezo wa kisiasa na kiuongozi wa wagombea na masuala ya gharama za kampeni yakawa ni jukumu la pamoja?

Tuendelee kujadili.


JJ
 
Mnyika,
Mazingira ya sasa kuliko wakati mwingine wowote majimbo ya Dar hayakamatiki sio tu kwa ninyi wa Upinzani bali hata kwa wanaCCM masikini kama "rafiki" yako Nape. Hakuna namna ya kuibadili hali hii kwa sasa. Ingekuwa rahisi kidogo kama ungekuwa unatoka Kilimanjaro na hasa Uchagani. Majimbo ya Ubungo na Kawe Uchaga unasaidia.
 
Mnyika,
Mazingira ya sasa kuliko wakati mwingine wowote majimbo ya Dar hayakamatiki sio tu kwa ninyi wa Upinzani bali hata kwa wanaCCM masikini kama "rafiki" yako Nape. Hakuna namna ya kuibadili hali hii kwa sasa. .

Wildcard,

Umasikini mbaya zaidi ni umasikini wa mawazo. Mwaka 2005 jimbo la Ubungo likuwa na wapiga kura laki tatu na elfu 10. Sasa watakuwa wameongezeka zaidi.

Tuchukulie kwa ajili ya mjadala kwamba jimbo lina wapiga kura laki tatu.

Kati yao, asilimia 10 ya wapiga kura ikaamua kukuunga mkono kwa hali na mali kama mtaji wa kisiasa wa kuanzia. Huu ni utajiri mkubwa wa ushindi.

Watu 30,000 kila mmoja akitoa elfu 1 tu kuwezesha kampeni ni sawa na shilingi 1,000 zidisha kwa 30,000= 30,000,000(Soma milioni 30).

Pamoja na umasikini wa baadhi ya watanzania wanaoishi mathalani Manzese Uwanja wa Fisi hapa jimboni Ubungo. Unadhani kati yao hakuna wenye kuweza kutoa buku moja? Kwa kipindi cha miezi takribani ya kampeni ni sawa na wao kuamua kutoa mia tatu tu kwa mwezi sawa na shilingi kumi kwa siku!.

Lakini kumbuka pia kuna watu wa 'tabaka la kati'(kwa viwango vya bongo) walioko mathalani pale Sinza jimboni Ubungo. Hawa hawawezi kutoa zaidi ya elfu moja kwa mwezi?

Msingi wa makala yangu ni kutaka watanzania wabadili mtizamo kuhusu wagombea, kampeni na uchaguzi kwa ujumla. Siku mapinduzi hayo ya fikra yakitokea kutatokea vuguvugu kubwa la mabadiliko ambalo halitaweza kuzuilika.

Hawa watanzania wanaoitwa masikini, wakiwekeza senti zao kwenye uchaguzi hawatakubali kirahisi kuhongwa na watashiriki kwa hali na mali kulinda kura. Pamoja Tutashinda kwa falsafa ya Nguvu ya umma.

Tuendelee kujadili na tuupekeke mjadala huu huko vijiweni waliko wananchi wa kawaida kabisa ambao hawawezi kutembelea kwenye mtandao.

JJ
 
Mnyika,
Nimekuwa muwazi kwako kwa kuwa naamini unao uwezo wa kuwa kiongozi katika ngazi hiyo ya Ubunge. Naamini pia yapo uliyoyaona mwaka 2005 ulipogombea na Mzee Keenja. Unaweza usiyaseme yote lakini unajua wazi kwamba yapo. Wapiga kura wetu wengi hawako hivyo unavyojaribu kueleza hapo juu. Hatuna utamaduni wa kumchangia mgombea badala yake tunamtarajia yeye atumwagie pesa, vitenge, pilau.....
Masuala ya "kabila letu" hasa kwenye ngazi hii ya Ubunge yana nafasi kubwa tu.
 

Wildcard,

Nakushukuru kwa kuwa muwazi. Hayo unayoyasema ni kweli yanasemwa na baadhi ya watu pia. Kwa hiyo ni muhimu tukayajadili, tukayatafakari na kuyazingatia kama changamoto.

Hoja ya ukabila huwa inajitokeza, na kwa kweli ni hoja ya kukemewa. Ni ubaguzi ambao Mwalimu Nyerere aliwahi kuuita ni sawa na kula nyama ya mtu. Ndugu wa karibu wa ukabila ni udini, nao huwa unasema semwa. 2005 niligombea na Keenja, ni mchagga. Mimi ni chotara wa kiafrika- baba yangu msukuma wa mwanza, mama yangu ni mpare wa same. Kwa hiyo wakati huo nilipochukua fomu, wapo walioniasa kwamba usigombee kwa kuwa wewe sio mchagga, kwa hiyo wachagga wa ubungo hawatakuunga mkono. Kama ningesikiliza sauti hizo wakati huo, hata ule ushindani wa 2005 ambao mpaka leo umebaki kuwa sehemu muhimu ya historia usingekuwepo. Nikaingia, na kwa kweli ni nikaungwa mkono na watanzania, wa makabila mbalimbali wanaoishi ubungo; wakiwemo wachagga. Sasa tuendelee na mjadala wazi kwa kweli, hiyo ilikuwa 2005; je, 2010 hali imebadilika na kwamba sasa jimbo la Ubungo lina ukabila wa hali ya juu na kwamba makabila mengine yasigombee jimbo hilo ndani ya Mkoa wa Dar es salaam?

Nakubaliana nawe kuwa nilijifunza mengi kwenye uchaguzi wa mwaka 2005, yapo mengi kiasi kwamba yanaweza hata kuandikiwa kitabu.

Nilipoanza kampeni 2005 kweli umma kwa kiasi kikubwa sana ulikuwa na mtazamo huo kuwa wagombea ni kugawa fedha na vitu, kwa kuwa wamezoeshwa hivyo kuwa na utamaduni wa takrima na rushwa.

Kwa hiyo changamoto kuu niliokuwa nayo kama mgombea wakati huo ilikuwa si tu kuwaeleza sera zangu nakusudia kufanya nini bali pia kuwabadili mtizamo(mindset/perception) kwamba mgombea hapaswi kugawa fedha. Na kwa kweli mwanzoni ilikuwa ngumu sana, lakini niliamua kabisa kampeni zangu msingi wake mkuu uwe ni kufanya siasa safi na kutoa elimu ya uraia.

Unaweza kuona namna ambavyo vuguvugu hili likuja kukubali; na kwa kweli wakati huo tuliweza kushindana na chama dola, na mgombea aliyekuwa waziri wakati huo akichangiwa na wafanyabiashara wakubwa akigombea kwenye chama chenye tuhuma ya kuchota fedha kifisadi na kuchangiwa na mafisadi.

Unaweza kujiuliza sasa tuliwezaje kupata fedha za kuendesha kampeni zote zile wakati huo nikiwa na miaka 24? Ni kwa watu mbalimbali walioguswa na kampeni zile(narudia kuwashukuru kama watasoma ujumbe huu hapa). Lakini, somo kubwa nililojifunza kuhusu katika hili ni kwamba kuwa na mtandao wa wachangiaji wachache pekee hakutoshi, kwa maana ya kuwa na rasilimali za kutosha na kwa maana ya kuuamsha umma kushiriki kulinda ushindi na kuwabana majirani zao wasikubali kuhongwa!

Ndio maana hoja ya mfumo huu nilioupendekeza kwenye makala ni kutaka twende hatua moja mbele kutoka pale tulioishia mwaka 2005(si lazima mgombea niwe mimi, kama wananchi wataona sistahili kugombea basi huyo watayemtaka); tuanzishe vuguvugu la kufanya wananchi wenyewe waunge mkono kwa hali na mali kampeni za wagombea badala ya kuwaomba wagombea mali. Wananchi waelewe kwamba tunaowachagua ni viongozi wa umma, wakiingia kwa nguvu ya umma; watautumikia umma; wakiingia kwa nguvu binafsi, watajitumikia binafsi.

Kwa hiyo mimi nauna mjadala huu ni wa muhimu sana, nataka kwa kweli kusikia na kusikiliza sauti za watu ili niweze kufanya maamuzi sahihi. Na ningependa mjadala huu usihusu jimbo la Ubungo pekee, uhuru pia majimbo mengine, ili watanzania wafanye maamuzi sahihi.

Hoja yangu kuu ndani ya makala yangu; je uamuzi wa kugombea au kutogombea kwa mgombea ambaye tayari anafahamika mbele ya umma nguvu na udhaifu wake; je uwe suala lake binafsi au uhusishe pia maoni ya umma?

Tuendelee na mjadala

JJ
 
Mnyika wahamasisheni vijana wajiandikishe kwa wingi ili wapate fursa ya kupiga kura vinginevyo tutakuwa tunaendelea na hadithi zile zile naamini wapiga kura wengi ni kina mama na watu wenye umri mkubwa ambao wengi wao wamemezwa na CCM.
 
Mnyika wahamasisheni vijana wajiandikishe kwa wingi ili wapate fursa ya kupiga kura vinginevyo tutakuwa tunaendelea na hadithi zile zile naamini wapiga kura wengi ni kina mama na watu wenye umri mkubwa ambao wengi wao wamemezwa na CCM.

Fidel80,

Nakubaliana nawe, wapiga kura wapya hususani vijana huwa wanapigia kura mabadiliko. Uandikishaji unaendelea sasa hivi kanda ya kaskazini. Utakuja Dar es salaam Februari/Machi. Ni muhimu sana kufanya jukumu la kuhamasisha watu kujiandikisha, lakini halipaswi kuwa letu peke yetu. Kila mmoja atimize wajibu wake ama kwa kuwaambia wengine au kwa kuchangia rasilimali zitakazowezesha kutolewa kwa matangazo ya uhamasishaji na kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya kuhamasisha umma kutimiza wajibu wao.

Hata hivyo, kwenye suala la wakina mama, tunapaswa kwenda hatua moja mbele zaidi. Hatuwezi kuliacha kundi hili na kuona tu kwamba kundi hili halikubali mabadiliko na kwamba linaunga mkono chama kilichopo madarakani. Ni lazima tujiulize kwanini wakati ndio kundi lenye kuathirika zaidi na hali duni ya maisha inayotokana na uongozi mbovu? Lazima tujiulize, ni mbinu gani zitumike kulifikia kundi hili ambalo kwa kawaida haliji kwenye mikutano ya hadhara ya upinzani kwa wingi kama vijana? Kwanini wanawake hawako mstari wa mbele kwenye uongozi hususani katika upinzani? Je; hatuna wanawake wa kuwa mstari wa mbele kuwabadili wanawake wenzao? Maswali haya yatatusaidia kutafakari masuala ya kuingiza kwenye mikakati. Kwa hiyo mjadala uendelee, mpaka kieleweke

JJ
 
Fidel80,

Nakubaliana nawe, wapiga kura wapya hususani vijana huwa wanapigia kura mabadiliko. Uandikishaji unaendelea sasa hivi kanda ya kaskazini. Utakuja Dar es salaam Februari/Machi.

Mmeweka mikakati gani ya kuwasukuma wananchi hususani vijana wajiandikishe kwa wingi? Maana naona mnafanya kazi ile ile ya kuwaeleza wananchi kuhusu ufisadi n.k kinacho takiwa hapa ni kupiga kampeni watu wajitokeze kwa wingi wajiandikishe ili wawe na vitambulisho vya kupigia kura maana navyo ona wengi wa watu wanao jiandikisha ni kina mama na hawa wazee sasa hawa idadi kubwa ni CCM toeni elimu kwa wananchi wa huko umuhimu wa kujiandikisha wakisha jiandikisha kwa wingi nendeni sasa mkawape ni wapi chama tawala wameshindwa na kwa nn wameshindwa na nyie mtawezaje kufanikiwa?
 
Mnyika, Wildcard,

Nimesoma majadiliano yenu na labda niwape uzoefu ambao mimi ninao wa huko wilayani kwetu.

Tusahau ya USA au UK au Europe ambako watu wako tayari kuchangia demokrasia kwa faida ya maendeleo yao, kwa Tanzania na Watanzania nafikiri ni ngumu sana na walio wengi hawaoni kabisa umuhimu wake.

Wananchi wengi wanafikiri wakati wa uchaguzi ni muda wa wao kuchuma na wala sio kinyume chake. Imefika mahali TZ hata kuonyesha kwamba wewe huna pesa inakuwa kama ni sawa na kuwaambia wananchi huna uwezo wa kuwaongoza.

Hiyo ndio reality iliyoko nyumbani na ndio maana watu wenye lengo la kujitajirisha kupitia siasa, wako tayari kufanya lolote kukusanya pesa na kisha wakipata uongozi basi hawana muda wa kuwatumikia wananchi tena na inageuka kuwa kipindi cha kuchuma. Hata uji wa mgonjwa inakuwa halali yao kuunywa.

Tanzania ya leo ni ngumu sana kwa maskini kugombea uongozi wa siasa na sio kwamba haiwezekani ila kuna ugumu na sababu kubwa ni kwamba wananchi wameonyeshwa pesa na wanasiasa na sasa na wao wanataka mgawo wao maana wanajua hakuna la maana ambalo wanasiasa wanaweza kuwafanyia.

Inasikitisha lakini huo ndio ukweli wenyewe. Kuja kubadili trend hiyo itakuwa ngumu sana. Muhimu ni kufanya yale ambayo mtu unaamini ni sawa. Ni bora ukishindwa ukitetea mambo unayoyaamini kuliko kushinda kwa njia zozote zile.
 

Mtanzania,

Wakati nakubaliana na hali uliyoisema, sikubaliani nawe kwamba kuibadili trend hiyo ni ngumu sana. Inaweza kuwa ngumu ndani ya CCM, kwa sababu mfumo wa chama umeelemewa na utamaduni wa namna hiyo wa ufisadi lakini si ngumu sana kwa umma.

Ukweli ni kuwa wananchi wanaonyesha ugumu kwa sababu ya kukatishwa tamaa na wanasiasa, wanaweka matumaini kwao halafu baada ya kuchaguliwa wanawaangusha. Kwa hiyo wanaona siasa ni mchezo mchafu na ni kazi ya nipe nikupe.

Lakini nimekwenda vijiji kwenye chaguzi Tarime, Mbeya Vijijini, Busanda na Biharamulo; nimekwenda chini kabisa na kuishi na watu. Watanzania wanaweza kabisa kubadilika wakiona tumaini jipya.

Pamoja na umasikini wao wanaweza kubadili mtizamo, na wanaweza pia kuwa na msimamo. Na kwa kweli hao wanaoitwa masikini na wanaoitwa hawana elimu ya uraia, hao watu wa vijijini wakichukua mwelekeo mbadala wanauwezo wa kufanya maamuzi magumu yaliyo mazuri.

Ikawa hayo yanawezekana kwa wananchi wa kijijini kama ilivyokuwa Tarime, ni aibu yakishindakana kwa wananchi wa mjini kama Ubungo ambao wanaitwa kuwa wanauelewa kuliko wenzao wa vijijini.

Suala la kujiuliza, ni mikakati gani itumike katika kubadili hali hiyo? Nini wajibu wa kila mmoja wetu katika kufikia azma hiyo?

JJ
 


kijana,
ni vizuri ujibu na hivi vijiswali,ni vya kizushi lakini vina uzito.All the best mkuu...mi nilikupigia 2005,sasa hivi nilishahama ubungo.pambana tuko nyuma yako.
 
kijana,
ni vizuri ujibu na hivi vijiswali,ni vya kizushi lakini vina uzito.All the best mkuu...mi nilikupigia 2005,sasa hivi nilishahama ubungo.pambana tuko nyuma yako.

Rugas

Kwa jina uliloliita viswali hivyo, ni muhimu kutovipa uzito mkubwa tusije tukatoka nje ya mjadala. Lakini kimsingi, ni muhimu maswali yote yakajibiwa- mahali muafaka na wakati muafaka.

Nakushukuru sana kwa kunipigia kura mwaka 2005, na nashukuru kwa kuendelea kuunga mkono. Pamoja Tutashinda


JJ
 
kijana,
ni vizuri ujibu na hivi vijiswali,ni vya kizushi lakini vina uzito.All the best mkuu...mi nilikupigia 2005,sasa hivi nilishahama ubungo.pambana tuko nyuma yako.

Bora Mnyika avipotezee hivyo viswali kwa vile kama kumbukumbu yangu iko sawa kipindi hicho alikuwa anamalizia degree yake ya biashara UDSM au alikuwa amemaliza. Sa sijui huyo mleta swali anafahamu zaidi anachokiuliza au nikuyumbisha trend ya kujibu hizo hoja.
 
kuna haja ya kuwa na wagombea binafsi

Dada,

Hilo ndilo lilikuwa tegemeo la wengine kwamba ile hukumu kwenye case ya Mtikila ingetekelezwa, na kuwapa nafasi watu wengi ambao hawako interested na hii minyororo ya vyama, kuweza kutimiza malengo yao kisiasa bila kulazimika kujiunga na vyama.

Naona vyama karibu vyote haviungi mkono hili labda kwasababu wanaogopa wananachama kuwakimbia.

Tatizo kubwa kwa TZ kwa maoni yangu ni sisi watu. Ukiunganisha Watanzania wawili pamoja utagundua matatizo baada ya muda mfupi tu.

Pamoja na vijembe vya kisiasa, tatizo letu la utendaji mbovu linabaki kuwa pale pale bila kujali ni chama gani au kampuni gani au familia gani.

Bila kuwajibika na kujituma katika kazi, tusitegemee maendeleo yoyote ya maana. Tunaongea sana, lakini ukitupeleka kwenye utekelezaji, hakuna kinachoonekana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…