Wachezaji wanajeshi wawili wa kikosi cha Zambia AFCON 2012 kinachoshiriki michuano hiyo huko Guinea ya Ikweta na Gabon, nahodha Chris Katongo na Nathan Sinkala, wamepandishwa vyeo jeshini na Amiri jeshi mkuu wa nchi hiyo, rais Michael Chilufya Sata kutokana na mchango wao katika timu ya taifa. Katongo amekuwa Warrant Officer Class One ambapo kabla ya hapo alikuwa Warrant Officer Class Two. Sinkala (angalia avator yangu) amepandishwa kuwa Sergeant ambapo kabla ya hapo alikuwa Corporal.
Itakumbukwa kuwa hii ni mara ya tatu kwa Katongo kupandishwa cheo bila ya kuwepo kambini, kwani muda wote anacheza soka ya kulipwa China. Alipandishwa kutoka koplo hadi sajent mwaka 2007 kwa kupiga hat trick (mabao matatu peke yake) katika ushindi wa Zambia wa 3-1 dhidi ya South Africa mjini J'burg na kuiwezesha timu yake kufuzu AFCON 2008. Akiwa huko Ghana AFCON 2008, alipandishwa tena cheo kwa kuisaidia timu vyema na akawa staff sergeant.
Aliruhusiwa kutoka kambini kwenda kucheza soka ya kulipwa nje ya mipaka ya nchi yake, ambapo kwa hapa Tanzania, mwanajeshi akihama timu yake anafukuzwa kazi !