2013 chai day

Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Posts
5,329
Reaction score
5,024
Hi all,

Hii itakuwa ni mara yetu ya tatu mfululizo kufanya mkutano/kikao hiki pale Lunch Time Hotel, iliyopo along Mandela Road opposite na Mabibo Hostel.

Tunaita Chai day kwa sababu huwa tunakutana kujadiliana mambo muhimu tukiwa ktk kundi la watu wenye umri tofauti,ili kukipa kikao heshima huwa tunakunywa chai, kahawa,maji, juisi ktk muda wote tunaokata hoja. Tunaogopa maji ya Ilala kwa sababu wengine huwafanya wahame station.

Kundi hili linafanya uwekezaji kwa kuotesha miti ya mbao na boriti ( kilimotz@googlegroups.com),ni kundi la hiari na halina kiingilio, kiingilio ni nguvu zako. Agenda kuu ni kama zifuatazo; kundi/wadau kuingia ktk biashara ya hewa ya ukaa na nini cha kufanya;baada ya mafanikio yetu nini kinafuata;Changamoto za uwekezaji huu kwa sasa; Je ni wakati mwafaka sasa kwa kundi letu kuomba shavu la serikali?, AOb ni agenda ya mwisho.

Mkutano utafanyika February 2013, tarehe itafahamika mara baada ya kumpata mtalaamu toka SUA ili aje ashushe darasa kuhusiana na biashara ya hewa ya Ukaa. Kila mjumbe itabidi aje na Tsh 20,000/ kwa ajili ya ukumbi. Kwa wale ambao hawajawahi kuwekeza ktk kilimo hiki na wanataka kufanya hivyo mnakaribishwa siku hiyo.

Hili ni moja ya makundi yaliyofanikiwa kwa njia ya kuunganisha nguvu na hatimaye wengi wamefanikiwa kufikia malengo awamu ya kwanza.
 
..ASANTE SANA; mUNGU AKINIJALIA NAMI NITAFIKA
 
..ASANTE SANA; mUNGU AKINIJALIA NAMI NITAFIKA


Nimefanikiwa kumpata mtalaamu wa shughuli za hewa ya Ukaa toka SUA, ameahidi kuja kutoa maelezo/maujanja ya namna ya kuingia ktk biashara ya hewa ya ukaa. Kwa sasa naomba kuwajulisha wadau kuwa mkutano wetu utakuwa tarehe 09/02/2013 saa nane sharp mchana pale Lunch Time Hotel along Mandela Road opposite na mabibo Hostel.
 

Pamoja mkuu
 
Asante Mkuu Malila kwa mualiko!
Nitahudhuria kwa mara ya kwanza maana nilianza rasmi shughuli hizi za kilimo mwaka jana ktk wilaya ya Kilosa.
Japo nimelenga kilimo cha miembe na migomba ya kisasa (cavendish) kwa soko la dar, pia naendelea kutafuta maeneo mengine yenye ardhi inayofaa kwa kilimo cha miti ya mbao.

Kuh hii biashara ya carbon trade ambayo ni moja ya agenda katika kikao cha tarehe 9 feb 2013, ningeshauri wadau
wacheck hii website Plan Vivo › Improving livelihoods, conserving and restoring ecosystems ili kuona baadhi ya projects ambazo tayari zipo katika mpango huu. Pia vigezo na
project documents zimewekwa wazi kwa yeyote kuzi-study. This will put us in better position to understand whatever the invited expert will be explaining!
Kila la kheri wakuu!
 

Asante,

Tufanye hivi, kwa sababu mimi nayajua maeneo ya kuotesha miti, na nimekuwa ktk hii shughuli kwa miaka sasa, naomba nitumie uzoefu wangu kukusaidia ili upate urahisi wa kutekeleza nia yako hiyo. na wewe nitafutie eneo la kulima migomba/ndizi hapo Kilosa. Nipe na bei kwa eka kama unaweza kupata na mimi nitafanya hivyo hivyo.Maana Kilosa ni karibu zaidi kuliko Chita.
 
Sawa Mkuu Malila!
Kwa vile next month of Feb nitakuwepo Kilosa kwa muda mwingi(naandaa mashamba) nitafanya utafiti wa eneo zuri kwa migomba na upatikanaji wake. Maeneo mengiya kijiji hicho yanafaa kwa kilimo cha mazao mbali mbali, ila kwa migomba minilipendelea ardhi iliyoko mkabala namto ili niwe namwagilia wakati wa kiangazi na kuvuna ndizi wakati wote wamwaka. Ardhi ina rutuba sana!!!
Je, nikuangalizie uwezekano huo wa pembezoni na mto? Ni mtoWami ambao haukauki mwaka mzima una maji tele. Challenge ya hapa ni manyaniMkuu, ila wenyeji wananipa moyo eti manyani yatahama endapo watu wotewakiendeleza maeneo yao. Kweli baadhi wanafyeka na kulima hasa mipunga lakinibado sehemu kubwa ni matajiri wameshika halafu wako Dar hawaji kufyeka maporiyao.
Sheria ya kijiji ni miaka 4 hujafyeka unanyanganywa. Minilizembea 5 years sikuonekana, baada ya JF kunistua ndo nikarudi fastanikabembeleza viongozi ndo wakanipa ardhi nyingine huko mtoni kwenye manyani,ila nikaendelea kununua kwa wenyeji ambako manyani hayapo tena.
Kwa taarifa za hapo kijijini, kwa sasa ardhi ya kupewa nakijiji (30,000/-) kwa eka hawana tena ila ukikaa nao karibu, wao wanajua nieneo gani muda wa kuendeleza una expire na any time wanaligawa pori kwa mwingine.
Nitumie mobil No yako kwa Pm ili tuwasiliane zaidi.
 

Mkuu tafadhali pitia kule kwenye uzi wa Kilimo cha ndizi utupe Maujuzi yako ya kilimo cha hizo ndizi za kisasa
 

Mkuu Malila nategemea kuja kwenye chai day kwa sasahivi nipo Mbeya ila naweza funga safari kuja huko kwa ajili hiyo Je hili kundi linawezaje kunisaidia kuingia kwenye uwekezaji wa kilimo cha miti? Je linaweza kunisaidia kujua sehemu ya kupata ardhi? aina ya miti ya kupanda na ushauri mwingine wa kilimo cha Miti? Sina Maujanja kwenye hili eneo
 
Hili kundi litakusaidia yafuatayo bila malipo;Utapata shamba karibu na maeneo walipo wao ili iwe rahisi kwenye managementUtapata urahisi wa kuoteshewa miche ktk vitalu, kupandiwa na kutunziwaUtapata ushauri wa nbegu gani upande na nini faida zakena mbegu pia tunanunua kwa pamoja.Siri ya mafanikio yetu ni kila mtu kutimiza wajibu wake kwa siku yake anayopata nafasi na kutumia alicho nacho kwa faida ya wote. Wachoyo huwa tunawa-delete haraka sana. Kama uko Mby mjini, naweza kukupa simu ya member wetu moja yupo hapo soko matola anaweza kuwa bonge la link na group yetu.
 
Mkuu niombee kando ya mto huko kwenye manyani. Nakutumia kwa pm simu yangu ili tuongee vizuri.
 
Haya maelezo na kuhusu hicho kikao hasa upande wa kilimo cha kisasa kwa kweli nimevutiwa nayo saaana. Nitakuwepo kikaoni wadau nikaribisheni, sijawahi kulima ila nina ndoto za kuingia katika kilimo hivi karibuni.
Uliyeleta hii thread nakushukuru sana kwani nimepata pa kuanzia.
 

Ni Pm hiyo number mkuu ntashukuru sana pia ntakuwepo kwenye Chai Day ntajitahidi nije
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…