Mkuu
Nguruvi3 uliongea ni kweli kuhusu wananchi wa vijijini kuamini kuwa bila CCM maisha yao hayaendi.. Matatizo kwao imekuwa ni sehemu ya maisha yao hivyo hawaoni kero, kwao muhimu ni mvua zinyeshe walime, wavune, washerekea mavuno basi kwao wanakuwa wameridhika.
Hawa watu hawaelewi kuwa ni haki yao kupata maji, umeme, mashule, kujenga barabara, serikali kutengeneza vyanzo vya ajira kwa ajiri ya watoto wao, ni wajibu wa serikali kuhakikisha hakuna mtu anayekosa matibabu na nk. Hawa watu wanaamini kabisa kuwa kukosa dawa hospitali ni kawaida, watoto kurundikwa madarasani ni kawaida, shule kukosa waalimu ni kosa la waalimu, kukosa maji ni adhabu kutoka kwa mwenyezi Mungu na nk.
Hawa watu wanahitaji elimu ya uraia hii elimu kwa bahati mbaya au nzuri hawezi kutolewa na serikali maana serikali kuwapa elimu ya haki zao ni kama kujichongea.. Elimu hii inabidi itolewa na vyama vya siasa, wapenda mabadiliko, wanaharakati na nk.Lakini kwa bahati mbaya kutokana na ukosefu wa pesa, vikwazo mbali mbali kutoka serikalini inakuwa ni vigumu kutoa elimu hii. Hivyo basi kujikuta watu wengi waishio vijijini kuendelea kuichagua ccm pamoja na umasikini mkubwa walionao.
Tatizo lingine linalokumba siasa yetu za Tanzania au za Afrika kwa ujumla ni ubinafsi wa viongozi, viongozi wetu wa vyama vya siasa ni wabinafsi anapokuwa kiongozi malengo yake si kukuza hicho chama bali malengo yake ni yeye kama yeye kufaidka kwa namna moja au nyingine na uongozi wa hicho chama.
Tukiangalia baadhi ya vyama vya siasa vimekuwa vikifanya vibaya mwaka hadi mwaka lakini huoni uwajibikaji wa uongozi pale wanapopoteza kura/wanapopata kura chache kulingana na chaguzi zilizopita. Utakuta kiongozi tena msomi kabisa chama chake kinadidimia kila mwaka lakini hashutuki na kuachia ngazi bali atang´angánia mpaka chama kife au kisahaulke kabisa, sasa mtu unajiuliza hivi hawa viongozi akili zao huwa ziko sawa kweli? huyu mtu anaweza ana mapenzi mema na chama chake kweli?
Alinda , CCM haiwezi kutoa elimu ya Uraia. Wanafahamu huo unaweza kuwa ndio mwisho wao. Wanachokifanya ni kwenda kula na wananchi au kubeba matofali mawili ili wananchi waone hiyo ndiyo haki zao.
Wanabeba matofali mawili kujenga zahanati, wakati gharama za matibabu kwa mmoja tu ni sawa na gharama za zahanati tatu au nne. Kuna waziri mmoja alipelekwa India na kukaa miezi 6 huko akitibiwa.
Tunamsikia akisema CCM imeleta maendeleo, wananchi hawajiulizi yapi hayo? Ya yeye kuishi hotelini India au
Tatizo la vijijini si kukosa pesa za kuwafikia wananchi tu, ni kubwa zaidi ya hapo. Kuna watu muhimu sana katika jamii wanaoishi huko( Walimu). Sasa kama wao wameridhika kupata mafao kila miaka 10 kama walivyoahidiwa Ngurufoto, tutegemee wanakijiji wachote wapi elimu?
Kundi lingine ni la vijana na hasa wasomi. Wakirudi vijijini hakuna anyewasaidia wananchi kutambua kuwa huduma ya afya, maji na elimu ni haki yake. Kazi yao ni kutafuta kazi za upambe. Mwisho wa siku kazi ya upambe inakwisha wanarudi mjini kulalamika mambo si mazuri
Nasi huku mitandaoni tuna 'share' yetu. Tunajadili mambo yasisyowagusa wananchi kabisa. Mfano, topic inayohusu gari la Obama kuwasili Nairobi. Nyuzi hiyo inachangiwa vema sana na hata kujiuliza, gari hilo ujio wake unamsaidiaje mwananchi wa kawaida wa Kenya au Tanzania?
Pengine tubadilike na kujadili matatizo yao, si wote lakini wachache wanaweza kukota kitu na muda unavyosonga mbele kasi ikashika.
Kuhusu viongozi kutowajibika, hili nalo neno. Ni tatizo linalotokana na sisi wananchi kuacha mambo yakielewa. Uchaguzi unapokwisha mwingine unaanza. Ni lazima kuwe na post mortem ya kujua kwanini imetokea hivi na si vile
Tatizo ni sisi tusio wawajibisha, si wao wanaotaka kutowajibishwa
Tatizo la watanzania ni ile hali ya ' baasi waache tu au tutafanyaje au kazi ya mungu hiyo'
Ndio maana unakutana nao wakienda muhimbili, ukiwauliza , mambo? Utasikia poa tu. Yaania anakwenda Muhimu kwenye hukumu ya maisha yake, akijua hakuna dawa, atalala chini na pengine asimuone Dr bado anasema mambo poa tu!
Akitoka muhimbili na kusawajika kwa maradhi anasima na kusema CCM itamleta nani kugombea? Tunataka mtu wa kutuletea maendeleo.
Lazima tubadilike, tuangalie taifa kwanza. Tuache mambo ya vyama, kama kiongozi kacheza fyongo anaambiwa kaa pembeni. Hatuna upungufu wa viongozi, tuna upungufu wa maadili na wingi wa ubinafsi.
Tusiwaonee haya, tuwaambie sasa inatosha