Mkuu Mkandara
Ni tofautiane nawe kuhusu kuwalaumu wananchi kwa yanayotokea. Ninaamini kabisa, badala ya kuwalaumu wanasiasa na vyama vya upinzani, wananachi wanapaswa kuchukua lawama hizo.
Hakuna mahali katika dunia hii nguvu ya dola iliwahi kushinda umma. Dola ni zao la nguvu ya umma na si kinyume chake
Kwa dunia ya wenzetu, wanasiasa huwatumikia wananchi na si wananchi kuwatumikia wao.
Mambo yekienda kombo, jukumu la kuweka sawa ni la wananchi si la vyama vya siasa.
Vyama vya siasa hubeba agenda ya wananchi kwavile wana platform. Hufanya hivyo wakijua agenda ya wananchi ndio muongozo na si kinyume chake
Kama tutakubaliana wananchi hawana sababu ya kubeba lawama, tukubaliane hawana sababu za kulaumu wanasiasa
Muhimbili wananchi wakilala sakafuni, akina mama wakipanga foleni ya kwenda kwenye chumba cha kujifungulia hilo si tatizo la wanasiasa wanaotibiwa chunusi Appolo au Joberg. Na wala hakuna mwanasiasa atakayesimama kuzungumzia matatizo hayo kwasababu hayamhusu.
Kwa nchi za wenzetu, wananchi wanachukua jukumu mikononi mwao, iwe kwa njia ya sanduku la kura au nyingine
Ni makosa kuwapumbuza wananchi tukitumaini kuwa ipo siku malaika watataremka kulinusuru taifa. Tumejaribu miaka 50, je tusubiri hadi karne nyingine? Wale wenzetu wanaochukua hatua dhidi ya 'malaika' wamepungukiwa nini ?
Ni wananchi wa Tanzania peke yao wanaosubiri miujiza na si wao kuchukua hatma ya taifa lao
Wanasiasa wamefikia mahali wanadhani wao ndio nchi. Sababu kubwa ni wananchi walioshindwa kuwaambia wao ni waajiriwa. Mwajiri anaposhindwa kuchukua hatua dhidi ya mwajiriwa hilo ni tatizo lake, si la mtu au taasisi nyingine
Mkuu wangu tuendelee kutokubaliana katika hoja hizi maana mitazamo ipo mingi na tutafikia mahala tutaelewana kwa kutokubaliana..
Unajua kwamba wananchi sio wanaochagua viongozi bali huletewa majina na kuchagua kati yao. Unakumbuka ule ubishi wa Dr.Slaa kupata kura za wananchi wa karatu? haikuwa hivyo, na umeona ya CCM majuzi na ndivyo tunavyoendelea kuletewa wagombea au watia nia!. Sio wananchi wanaowaambia wagombea wachukue fomu bali wagombea huamua wenyewe na kwa sababu zao binafsi na hivyo wanapojitangaza ama kutangazwa ni mwanzo mpya wa wananchi wenyewe kumfahamu mgombea.
Licha ya hapo Mfumo wa nchi yetu ulivyo, mwananchi hana nafasi kabisa ya kudai ama kusema jambo na likawa. Kama wazazi wanalala chini Muhimbili unadhani wanannchi wafanye lipi tofauti? kuchagua chama kingine? Hivyo vyama vyenyewe umeona wanashindania nafasi za Uongozi hadi kutoana macho, na sii wamekubaliana nini juu ya maslahi ya wananchi!.
Ebu fikiria kidogo hapo, kwa nini vyama vyote nchini ugonvi wao mkubwa ni madaraka ndani ya vyama! Kuna nini haswa ukiwa kiongozi kiasi kwamba uko radhi kupoteza wanachama ubakie pake yako..Watu ndani ya vyama hawazidiani hoja zao kwa sera, dira ama idea mpya isipokuwa nani awe nani na roho ya KWA NINI..Na ukija kwenye uongozi wa Kitaifa jambo lolote linalowanufaisha wao hufukia vichwa vyao mchangani kama mbuni. Chukulia mfano wa mishahara ya wabunge, posho VX na hivi viiunua mgongo na nkadhalika, hao wananchi wafanye nini ikiwa hawakubaliani na miwang vilivyowekwa?
Mbunge mmoja anakula mshahara wa millioni 11 kwa mwenzi au Mil. 132 kwa mwaka na anaruhusiw akuwa na biashara zake, wapo wabunge 340 ni ngapi hizo - Tril. 44,880 kwa mwaka je miaka mitano?. Wanakula Posho at least mil 50 kila mmoja kwa mwaka mara 340, tril. 17 kwa haraka haraka kuna trillioni 61 kwa mwaka zinachezewa na hao hao unaosema tuwachague watatuletea maendeleo kumbe ndicho kinacho walepeleka Dodoma. Hapo hatujui Mishahara ya rais na ofisi zake, Makamu na ofisi zake, waziri mkuu na ofisi zake! taasisi za seirkali na kadhalika. Unafiiri ni kiasi gani tunachoma kwa matumizi ya kawaida tu..
Unataka mwananchi afanye nini kwenye sanduku la kura kupinga matumizi haya yasokuwa na huruma, ikiwa wagonjwa wanalala chini! Unapojiandikisha Ubunge unaondoa Huruma yote kwa sababu unajua unaenda chuma sio kumhudumia mwananchi. Uzalendo mgumo kaka sii swala la wananchi tena. Hakuna mgombea hata mmoja anayeingia Chimwaga atayezungumzia kuwa haya ni matumizi mabaya ya serikali ndani ya bunge hakuna..
Akitokea mgombea kesho akitangaza nia ya kukata matumizi ya kawaida ya serikali KUBWA na akaweka mfumo bora zaidi wa utekelezaji na uwajibikaji basi ndio nitaweza wapima wananchi kwa sababu adui wa maskini ni Umaskini wenyewe. tazama maskini wa watu wanavyosumbuka na Lowassa, wanamlilia kwa sababu kawaahidi pepo (kuondosha Umaskini) yale yale ya Mtikila 1995, wakidhani kwamba maadam Lowassa ni tajiri basi atakuwa na njia za kutajirisha watu wote wakati Lowassa huyo huyo ana ndugu zake wa damu na maskini..
Haya leo tunaambia tujiandikishe tupige kura ni haki yetu lakini tuloletewa ni Magufuli, Lipumba na Lowassa ambao wote wataahidi mambo yale yale isipokuwa wewe mwananchi unamuona nani zimwi likujualo! Kwa mfano CCM imeshatoa ILANI yake je umesikia Ilani ya UKAWA ama niseme CUF, NCCR au Chadema? hakuna zaidi ya ahadi ahadi ahadi za mgombea.
Haya wananchi wakifanya mgomo wanapigwa tena wanaitwa waleta fujo na kupoteza AMANI, huu ni mtazamoa wa viongozi na nguvu ya dola sio wananchi weloshika mpini. Kuna habari za mujini zinasema kwamba TISS wote wamerudi kambini hawatagombea Uchaguzi huu kwa sababu kuna hali ya hatari Kiusalama, na watu wote wanaoendesha vijimambo vya kuvuruga AMANI na UTULIVU watashughulikiwa! hapo sii swala la demokrasia tena, ila Usalama wa Taifa, sasa wewe na mimi ukishasikia hayo utaweza hata kuhema!..
Kifupi sisi tukubali KUTAWALIWA na hawa ndugu na jamaa zetu rangi moja, lugha moja.. Kufa hatufi, lakini cha moto twakiona!