Sehemu ya II
WAPINZANI NA AGENDA YA UFISADI
Kwa kuzingatia tuliyosema, wapinzani walijipambanua katika kupiga vita ufisadi. Hilo liliwapa nguvu kama agenda ya wananchi
Wapinzani wamejipambanua nalo na limewap ' political milage' katika kukabiliana na CCM
Mwelekeo ulikuwa wazi CCM kuondoka madarakani, au udhibiti wa mhimili kama bunge kupotea
Katika uzi huu, tumewaeleza wapinzani mambo mawili.
Ima wakazane kuchukua dola(Plan A1) na Bunge(Plan A2)
Uwezekano huo ulikuwepo, na CCM walisaidia sana uwepo wake
CCM WALIONA TATIZO
Kwa kutambua agenda umma, CCM iliwatosa makada wake nguli. Kishindo cha kushindwa kwa EL kinaeleza kila jambo.
Tukiri kuwa wanasayansi jamii wa CCM waliliona hilo , wakalifanyia kazi.
Ilikuwa ni kwa gharama kubwa kwa kutambua chama kitapoteza sana katika uchaguzi.
Hata hivyo, hiyo ilikuwa hatua mahususi kujibu hoja za wananchi
CCM wanatambua, mfumo uliopo unawatambua watu wake na kuwahudumia.
Hawakuona tatizo kwa mtu bali kwa wananchi. Walitambua, watuhumiwa wa ufisadi walitumia fedha nyingi ili ‘kununua' wapiga kura katika maamuzi vikao vyao Ukawekwa mkakati wa kuwaondoa(Rejea mabandiko ya nyuma)
LOWASSA
Ni mwanasiasa alijijenga ndani ya chama licha ya makando kando aliyo nayo.
Tulieleza katika nyuzi hii na nyingine, nguvu ya Lowassa haitokani na utashi wa jamii bali watu wanaoona ipo haja ya mheshimiwa kupata uongozi ili kulinda masilahi yao.
Wanaompigania si waumini wa sera au maono, kwamba mwisho watamwacha mwenyewe.
Tuliwaita ‘wafanyakazi' na kwamba kazi itakapokwisha , itategemea kama upo ushindi au la.
Kinyume chake watajiunga na makundi mengine. Kwao haikuwa siasa bali masilahi.
Ndivyo ilivyotokea. Tulisema pia, Lowassa hawezi kuhama na watu.
Atakaohama nao ni wale wale waliokuwa na masilahi na CCM itabaki kama ilivyo.
CCM KUPASUKA
Tulisema pia CCM haiwezi kupasuka kwasababu wanaoondoka si wanachama watiifu ni wanachama wenye masilahi.
Lowassa hawezi kuimega, wafuasi wake wanaitegemea CCM, haiwezi kupasuka isipokuwa upo uwezekano wa kudhoofika
KUUDHOFIKA
Katika kudhoofika, wapo wanachama watahama kwenda upinzani katika makundi matatu
- Waliochoshwa na utaratibu wa chama kushughulikia masuala ya kitaifa
- Walio na hasira za mgombe wao kupigwa chini
- Wanaoona ni wakati nchi kubadilika, hasa tukizingatia mijadala kama ya BMLK, Bunge la JMT n.k.
Kutokana na hilo, uwezekano wa wapinzani kutwaa dola(Plan A1 na Plan A2) ulikuwepo.
Hata kama ungekuwa ni kwa asilimia ndogo, kilichowazi ni kuwa Plan A2 ya kumiliki bunge ingefanikiwa.
Kumiliki ina maanisha CCM wasingekuwa na wingi 2/3 jambo ambalo lingewezesha wapinzani kupata nguvu ya kushughulikia mfumo mbaya mahala pa kuanzia
Mfano, serikali isingeweza kufanya kazi bila makubaliano na wapinzani.
Hapo pangewezekana kujenga mazingira ya mambo makubwa ya kitaifa kama Katiba, kubadilisha mifumo ya taasisi kama zile tume za uchaguzi na kuweka udhibiti wa vyombo kama Polisi ili vitoe haki.
Hadi hapo mfumo wa CCM ungeshaanza kudhoofika na pengine rungu lingefuata.
Lakini pia ingesaidia sana kuwajenga wapinzani mbele ya macho ya wananchi, tayari kushika dola .
Wangalikuwa mstari wa mbele kujenga hoja za kitaifa, ikiwemo kubadili mfumo taratibu kwa kuudhofisha kisha kuua kabisa
Inaendelea…