2018 FIFA World Cup: Yaliyojiri upangaji wa makundi ya Kombe la Dunia

2018 FIFA World Cup: Yaliyojiri upangaji wa makundi ya Kombe la Dunia

Argentina vs Nigeria. Hawa jamaa huwa wanakutana sana. Juzi kwenye friend match Argentina kachezea 4-2. Sasa wanakitana tena.

Tutawapiga nyau hao hata 10 kumbuka hii ni w/c. Na ile ilikuwa ni friendly match,,,,so Argentina alikuwa anapasha tu. Na record yao inaonyesha Nigeria hajawai kuifunga Argentina kwenye world cup/michwano muhimu.
 
Nimemsikia mchambuaji mmoja wa mpira amesema katika mara 6 Nigeria walizoshiriki kombe la dunia mara 5 kakutana na Argentina.... Ajabu kweli
1994 kule marekani Diego Maradona alipigwa viatu na wanigeria. Maradona akiojiwa na waandishi wa habari akasema waafrika ni mbwa. Game iliyofuata Nigeria vs Saudi Arabia Finidi George anafunga bonge la goli baada ya kuwapangua mabekia kibao wa saudi arabia. Anakimbia mpaka kwenye kibendera cha kona kisha anatembea kama mbwa anafanya kama mbwa dume anavyokojoa.

Dah Nigeria ya wakati ule ilikuwa kiboko aisee. Kina Rasheed Yekini...
 
Hivi mbona ulaya kuna timu nyingi sana, kuliko mabara mengine?
 
Kundi...B D F G ndio makundi ya wanaume. Waliobakia mfano brazil miaka yote anapangwa na vibonde. France nae anabahati hakuna timu pale,,atavuka kiulaini tu
 
cd76b29ba353820500b1be161f37d43c.jpg



b6b45d15f7dab038e5f8ab1275d7b0eb.jpg
 
Kwa mzungu kuhusiana hujuma ya kupanga linawezekana kuna wakati walikuwa wanachanganya vipira vya baridi kwenye vile vyungu.

Au unajuaje vile vipira labda vina sensor na yule mchagua naye amevaa sensor hivyo akishika kipira sensor inavibrate kwenye saa aliyovaa.


Mpira huu una fedha siyo mchezo na kuna baadhi ya timu kama Brazil hawawezi wakavumilia zitoke mapema.

Brazil kuwa kundi E na Germany kundi F inaweza isiwe bahati mbaya. Maana kila mtu akishinda kwenye kundi lake kukutana ni FAINALI KUU.
 
Sijajua kwa nini spain mabingwa wa 2010 wawekwe pot no 2. Poland aakae pot no 1. Kama ni kumaliza mshindi wa kwanza kwenye kundi spain alimaliza wa kwanza juu ya Italia.

Kama ni fifa ranking sidhani kama poland atakuwa juu ya Spain. Kigezo gani kimetumika?
Mkuu vinachanganywa ka uefa
 
Back
Top Bottom