2018 natangaza vita kali na adui umasikini

2018 natangaza vita kali na adui umasikini

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
2,428
Reaction score
3,937
Natangaza vita na huyu adui popote pale nitakapomuona. Na nimejipanga kwelikweli! Nimejitathmini na kugundua sipendi kuona mtu yoyote akitaabika kwa umasikini. Ukiweza kuushinda umasikini, mambo mengi sana yanakuwa rahisi zaidi kuyakabili na unakuwa mtu bora zaidi.

Hii ndiyo mipango yangu kwa 2018 na jinsi nitakavyomkabili huyu adui (namwambia kabisa mipango yangu, hii inaonyesha jinsi nilivyojipanga!):

  • Nitamtanguliza Mungu mbele zaidi
  • Nitasaidia wengine walioonyesha nia thabiti na juhudi za kupambana na umasikini (either kwa kuinvest katika biashara zao au kuwapa msaada kama grants/donations katika biashara zao, hata kama ni 10,000/=).
  • sitapoteza muda wangu kwa mtu yeyote au jambo lolote lile lisilonisaidia katika mapambano haya. Yeyote atakayenipotezea muda au hela yangu kizembe, nitamwambia wazi na sitamuonea aibu na atalipa kwa kosa hilo kwa njia moja ama nyingine.
  • nitajitoa kabisa katika mijadala yote ya kisiasa. Nitarudi kuwa msikilizaji kama ambavyo nimefanya kwa muda mrefu tu. Itakapofika December 2018, naweza hata nisijue Waziri Mkuu ni nani lakini investment zangu zitakapokuwa zinaingiza pesa ya kutosha tu, mbona itapendeza zaidi!
  • nitakemea mawazo, kauli au fikra za kimasikini kwa nguvu zangu zote popote pale nitakapozisikia. Hii nitafanya bila woga au kumung'unya maneno. Itafika wakati, umasikini ukiniona tu naingia sehemu ulipo, unakimbia wenyewe! Yes, it's that serious!
  • nitafuata kwa nidhamu kubwa dira na muelekeo ninaojiwekea wiki hii ya kwanza ya January 2018. Nitakuwa flexible kiasi katika execution kwa jinsi itakavyobidi lakini nitajitahidi dira na malengo yawe yale yale.
  • nitakuwa najikumbusha thamani yangu na kuisimamia kwa nguvu zangu zote kila nitakapokuwa na kila nitakachokuwa nafanya (na kuwafunza wengine pia wajue thamani zao).
  • nitatenga muda kuwa nawafundisha wengine na kushare ninachokijua. Hii imekuwa ni passion yangu siku zote ingawa sijaitumia ipasavyo kwa muda sasa.
Nayasema haya wazi ili universe na mbinguni wasikie na inipe msaada wote ninaohitaji katika hili. Natamka pia afya njema ya akili na mwili na amani katika moyo wangu ili nipigane vita hii kwa ujasiri na ushindi wa kishindo.

I DECLARE WAR. UWEZO NINAO, SABABU NINAZO, NIA NINAYO!

Nitarudi December 30, 2018 kuja kutoa testimony itakayotoa watu machozi.

My motto in 2018: 'Everybody around me is rich, or will be'

Happy New Year to you all.
 
Safi sana. Nyongeza hapo. soma na tafuta mbinu za kukwepa kodi kihalali/kisheria kwa kutumia loop holes zilizopo kwenye sheria za kodi. Inasikitisha sana unapojituma sana kufanya kazi ya serikali (kuleta maendeleo) halafu ukailipa serikali, ni ujinga
 
Maneno ya busara sana haya, nitayazingatia!
 
Everybody by me baby, Be Millionaire.

Nakuomba Mkuu usihache kabisa Kufatilia Posts za Mange Kimambi na kutembelea jukwaa la siasa hata kama hucomment chochote. Itakujenga uzalendo na Nchi yako. [ Jokes ]
Pia nakuomba usome vitabu vya kukujenga zaidi. Na mwisho zaidi kumbuka kutoa fungu la 10.
 
usitumie nguvu nyingi sana, jiunge na forex

Sitaki kumwambia sana huyu adui silaha zangu, si unajua unahitaji element of surprise kwenye vita ila hilo linaweza kuwa kombora langu la masafa marefu!

Lakini ushauri nimepata, it's all about working smart not hard.
 
Wenzangu mnajipanga halafu mimi kichwa changu kinasema

Sex

Sex

Sex

And more sex
 
Mambo ya New Year resolutions, safi sana Munyazi Mungu akusaidie, me hizi NY resolutions zishanishinda nikipanga Jan ikifika Feb nshatoka nje ya reli.

Unaweza mkuu ukiamua. Mipango huwa haitekelezeki kwa sababu kwanza mtu anajipa muda mfupi sana. Matokeo yake ukipata changamoto ndogo tu, unakata tamaa. Nilikuwa namwambia mtu juzijuzi, hakuna kitu ambacho ukikiwekea malengo ya kukifikia, mfano in 10 years, utashindwa, HAKUNA!
 
Everybody by me baby, Be Millionaire.

Nakuomba Mkuu usihache kabisa Kufatilia Posts za Mange Kimambi na kutembelea jukwaa la siasa hata kama hucomment chochote. Itakujenga uzalendo na Nchi yako. [ Jokes ]
Pia nakuomba usome vitabu vya kukujenga zaidi. Na mwisho zaidi kumbuka kutoa fungu la 10.

Ushauri mzuri, nitauzingatia. Mange Kimambi sijawahi kumfuatilia, sipo active IG.
 
Yatendee kazi hayo mkuu.usiishie kuandika tu hapa jukwaan.

Unaweza kujifunza kutoka kwangu,binafsi nimeorodhesha mipango yote ambayo napaswa kukamilisha kufikia 2020.ambapo kila jambo lina time yake ambayo iko fixed.na utekelezaji wake niliuanza mwaka jana 2016
 
Mkuu mpango kazi wako unaweza kutudokezea hapa?
 
Back
Top Bottom