Wakuu, amani ya Bwana iwe nanyi. Kwa heshima zenu hasa wale waliojibu uzi huu nilipouleta kwa mara ya kwanza takribani mwaka mmoja uliopita, nimeona ni vyema hata kwa mukhtasari tu nikawaletea mrejesho wa unabii huu niliounena juu ya maisha yangu.
Mwaka 2018 umekuwa mwaka bora katika maisha yangu yoooote. Nasema hivyo kwa dhati kabisa ya moyo wangu!!! Kauli nilizozisema zimetimia, zinaendelea kutiimia na zitaendelea kutimia kwa kuwa Mungu amedhihirisha pasipo na shaka kuwa yu nami.
Nimekutana na kufanya kazi na watu, mashirika na makampuni ambayo ni ya kushangaza sana. Na hayo yote yamekuja kwa njia ambayo pasipo na shaka ni mkono wa Mungu umetenda. Ndiyo maana nimeona ni wajibu wangu kuwaletea mrejesho ili labda umsaidie yoyote yule anayetetereka na imani yake.
Mshikilie Bwana usimuache na kwa wakati wake atakutendea yale unayoyaomba. Kumbuka maneno yake katika Yeremia 29:11-13.
Mwaka huu pia nimehudhuria mafundisho ya Mchungaji Mwakasege kwa mara ya kwanza kabisa. Pia nimemjua Mchugaji Kimaro wa KKKT Kijitonyama na kuyafuatilia mafundisho yake ambayo kwa kweli nayo yamenibariki sana.
Najua kuna mengi zaidi ningeweza kufanya na kwa hilo naomba Mwenyezi Mungu anisamehe kwa yote ambayo sikufanya kwa uzembe wangu.
Mapambano ya huyu adui umasikini yako pale pale na mwaka 2019 ndiyo kabisa naenda kummaliza huyu mshenzi. Nadhani na yeye anajua hilo ndiyo maana anaendelea na mapambano yake. Mwezi huu tu karibia na Christmas mara mbili tofauti nimekuwa kwenye gari zilizopata ajali, ya pili ikiwa Christmas yenyewe. Last time nimepata ajali na yenyewe ilikuwa ni siku kama mbili kufikia Christmas miaka kadhaa iliyopita na ilikuwa ni ajali mbaya sana ambayo ilikuwa ni miujiza kutoka hai ukiachilia mbali kutoka bila ukilema.
Yote kwa yote namshukuru sana Muumba wangu kwa yote. Nitamtukuza yeye daima na kunena ukuu wake bila aibu wala woga.
Mwaka 2019 utakuwa hata bora zaidi na mipango yangu ni hii na natamka haya na yatakwenda kutokea na kufanyika kwa Jina la Yesu Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai:
1. Naenda kuwajengea nyumba wazazi wangu.
2. Naenda kujenga nyumba yangu na kuishi maisha yale niliyoyatazamia na kuyapanga kwa muda mrefu.
3. Naenda kukarabati sehemu ya watoto kusali katika kanisa langu.
4. Naenda kukuza zaidi biashara zangu kwa level ya juu kabisa. Na nitakakikisha biashara zangu zinakuwa baraka kwa wengine pia. Ndiyo tafsiri yangu ya maneno ya Mungu anaposema sisi ni chumvi ya dunia.
5. Naenda kuanzisha familia yangu. Na nitahakikisha ni familia yenye kumjua na kumtukuza Mungu kama alivyotuamuru katika Kumbukumbu ya Torati 6:4-9.
6. Kuna mengine pia nimeyanena kwake na yeye ameyanena kwangu nayo pia nitahakikisha nayafanyia kazi. Nayo nitawaletea mrejesho nitakapoanza kuyafanyia kazi.
Nawatakia mwaka mpya mwema wenye heri na baraka tele. Mtumainie Mungu pekee naye hatakuangusha kamwe.