2019 Africa Cup of Nations Special Thread


Nigeria vs Burundi ( 1 — 0 ) AFCON 2019 Highlights
 
Naangalia mechi ya Uganda vs DR Congo, licha ya matokeo ya Uganda kuongoza 2-0 lakini dominance, determination, organisation, vigor ipo juu sana. Sishawishiki kama tuliwafunga 3-0 hapa Taifa bila wao kuweka uzalendo wa Afrika Mashariki.
Niliwahi kuandika humu JF, huenda Uganda walipewa kitu au walikuja kutalii sasa acha tujipakulie minyama kuwa sisi wababe wao eti tumepata droo kwao na tukawafunga.

Wakati Uganda kaenda Cape Verde kampiga sisi tukafa, kaenda Lesotho kambomoa sisi tulichezea, kwakweli ili kuondoa fedheha kesho nitakuwa shabiki wa Senegal uzalendo namwachia Nyerere
 
Africa jamani , hivi kwanini hii afcon isiweke promotion za nauli timu zipate washabiki wake!!

Aliye ona mechi ya kongo na uganda uwanjani atakuwa shahidi,

washabiki walikua nadhani ni 100, hamsini kongo hamsini uganda!!

Emu kaangalieni copa america jamani, watu wana jaa, hivi ni nini kinakosekana huku afcon team kupata mashabiki wake wa nchi husika lwa wingi??
 
hahaa maisha magumu bana
 
kivip mkuu
Madagascar wanamtukuza Ahmad Ahmad kuwa kawaletea neema kaingia madarakani tu CAF na nchi yake inaenda AFCON.

Wakati kiuhalisia ni afadhali hata ya timu ya Bongo, sasa amekutana na watu wanaopiga chenga hadi golikipa ndio wafunge.

Guinea wamefunga goli la dharau sana, ingekuwa ni mimi na kisirani changu ngumi zishawaka
 
Habari Za Muda huu Wa jamii, Sisi watanzania Kwa hamu kubwa Siku Ya kesho Muda Wa Saa Mbili Usiku tutakuwa tukitupa kalata Yetu ya Kwanza Katika Mashindano ya Africa cup of Nations dhidi ya Senegal Ni Matumaini Yangu kesho tunashida Kwani Nia Na Uwezo tunao japo kwenye mpira Wa Miguu Kuna Matokeo ya aina Tatu Ila Sisi ushindi Muhimu.
 
Kwa uandishi wa hivi tayari hiyo Taifa Stars imeshafungwa.
 
Ndio maana kuna jukwaa la timu mbali mbali kijana, hili ni jukwaa la mpira thread ya AFCON hakuna thread ya kila timu
Kila mtu mwenye dukuduku lake na timu anasema humu ndani ya thread hii
Sawa mzee napenda kutambua uwepo wako kesho kwa senegal...
 
MNATUPA kalata yenu.....
mtapigwa mchakae zaidi ya mbwa koko.... UGANDA YANGU NAITAKIA MEMA TU SIYO HII
ccm stars.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…