Uzalendo wa wananchi wa nchi yoyote kwenye kitu chochote haulazimishwi ila unatakiwa kuja wenyewe...
Watanzania wengi hupenda mchezo wa soccer (mpira wa miguu) na hii ingetosha kuwapa mitisha, mapenzi na uzalendo wa hali ya juu kuissuport timu ya taifa, ila vitu vichache (vya aibu ) vimetoa uzalendo kwa watanzania hawa...
Kabla timu haijacheza match dhidi ya Uganda tuliunganishwa ila maada ya matokeo kua mazuri kuna watu waliona timu ni yao na imefanikiwa kwa jitihada zao. mfano " ilan ya chama inatekelezwa kwa vitendo" , "Awamu ya tano imefanya tumekua na timu nzur ya taifa" nk
Juzi kuna mtu kasema yeye akienda timu itashinda wakati huo hana hata ujuzi wa mpira ( tena inawezekana hata sodo hajacheza), huku ni kuchanganya siasa na mpira kitu ambacho ni sumu kwa michezo yetu, ningetegemea kuona watu wenye uwezo wa mpira ( Mkwasa, na walimu wengne wa ndani pamoja na wataalamu wa psychology wanaenda kuwaweka sawa wachezaji wetu).
ukiuliza CV ya kocha wa timu ya taifa utaambiwa ashawahi kucheza Barcelona ( hiv kusoma na wanafunzi bora kunakufanya uwe mwalimu bora?? ) hii ni aibu, José morinho ashawahi kucheza wapi?
katika umri wangu sijawahi kuona stars ambayo watanzania hawakuipenda kama hii japo ilikua na vipaji vingi.
Tuacheni kuchanganya Siasa na michezo ili tufanikiwe.