2019 Africa Cup of Nations Special Thread

2019 Africa Cup of Nations Special Thread

😂😂😂😂😂😂😂

Algeria wameifunga Senegal 1 - 0 na hivyo kuifanya Taifa stars ambayo itaifunga Harambee Stars ya Kenya muda mfupi ujao kuwa katika nafasi nzuri ya kusonga mbele.

Nitarudi baadae kuweka msimamo wa kundi letu.

Hakika Cairo kumenoga.........Amunike hoyeee!


Maendeleo hayana vyama!
 
Ww unaona ni sawa kusema timu inatimza ilan ya ccm
Hapana hayuko sahihi kabisa sababu huwezi changanya mpira na siasa...but not everyone is after politics... Wengine tunashabikia coz ni timu yetu ya taifa hayo mengine hatujui...MTU unachukizwa na magoli ya msuva na samatta really??? Kuna watu wa ajabu sana dunia hii...Africa>politics kuna shida kubwa hapa..
 
Uzalendo wa wananchi wa nchi yoyote kwenye kitu chochote haulazimishwi ila unatakiwa kuja wenyewe...
Watanzania wengi hupenda mchezo wa soccer (mpira wa miguu) na hii ingetosha kuwapa mitisha, mapenzi na uzalendo wa hali ya juu kuissuport timu ya taifa, ila vitu vichache (vya aibu ) vimetoa uzalendo kwa watanzania hawa...

Kabla timu haijacheza match dhidi ya Uganda tuliunganishwa ila maada ya matokeo kua mazuri kuna watu waliona timu ni yao na imefanikiwa kwa jitihada zao. mfano " ilan ya chama inatekelezwa kwa vitendo" , "Awamu ya tano imefanya tumekua na timu nzur ya taifa" nk

Juzi kuna mtu kasema yeye akienda timu itashinda wakati huo hana hata ujuzi wa mpira ( tena inawezekana hata sodo hajacheza), huku ni kuchanganya siasa na mpira kitu ambacho ni sumu kwa michezo yetu, ningetegemea kuona watu wenye uwezo wa mpira ( Mkwasa, na walimu wengne wa ndani pamoja na wataalamu wa psychology wanaenda kuwaweka sawa wachezaji wetu).

ukiuliza CV ya kocha wa timu ya taifa utaambiwa ashawahi kucheza Barcelona ( hiv kusoma na wanafunzi bora kunakufanya uwe mwalimu bora?? ) hii ni aibu, José morinho ashawahi kucheza wapi?

katika umri wangu sijawahi kuona stars ambayo watanzania hawakuipenda kama hii japo ilikua na vipaji vingi.
Tuacheni kuchanganya Siasa na michezo ili tufanikiwe.
 
pamoja na kwamba timu yangu ya harambee star imeshinda ila niwapongeze taifa star wamejitahidi sana,mpira ulikua mzuri na magoli yote pande zote mbili yamefungwa kwa ustadi mkubwa,mimi sio shabiki wa mpira sana ila nimeweza kuungalia hadi mwisho ,wamejitahidi kwakweli
 
Nikiwa kama mtanzania mzalendo harisi nimefurahi sanaa kipigo cha 3-2 tulicho kipata kutoka kenya... Maana team yetu ya taifa inatumika kama ngazi kisiasa...

Kuna bwana mmoja ambaye hajielewi alisikika akisema watashinda kama wanavyo shinda chaguzi za CCM kwakua taifa stars ni CCM... Nikiwa kama mzalendo hiyo kauli sikuipenda...

Na kingine yule bwana kujinasibu kwamba yeye akienda basi taifa stars itashinda yeye ni nani kwenye soccer...

Tukumbuke kua soccer haihitaji janja janja mpira ni mchezo wa wazi unao hitaji ujuzi.. kwakweli magoal ya msuva na samatta yaliniuma sanaa na kunisononesha moyo...

Mpira ni moja kati ya michezo inayo kutanisha watu na kujenga umoja na udugu ndio maana sisi watu wa mpira tunapinga ubaguzi wa aina yoyote...

TAIFA STARS NI YA WATANZANIA WOTE NA SIO YA CCM PEKEE NDIO MAANA MNAOMBA MICHANGO KWETU SISI WANANCHI...

yule bwana ni kweli hajielewi
Huyo bwana yuko sahihi, sema huko Misri hawakumuweka mchakachuaji
 
Back
Top Bottom