2019 Africa Cup of Nations Special Thread

2019 Africa Cup of Nations Special Thread

Mkitaka mnenepe Africa shangilieni warabu team zote za Africa magharibi wanaelewa fitina zao wanakupiga nje ya uwanja na ndani wanakugonga chuma mmoja tu
 
View attachment 1130345

View attachment 1130346

Michuano ya kombe la mataifa ya Afrika inatazamiwa kuanza kutimua vumbi ijumaa tarehe 21/06/2019 kwa mechi kati ya wenyeji Egypt dhidi ya Zimbabwe

Michuano hiyo itahusisha mataifa 24 ambayo yamegawanywa katika makundi 6, kila kundi likiwa na timu 4

Tanzania imefanikiwa kufuzu kwenye mashindano hayo kwa mara ya pili katika historia yake, mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1980 na imepangwa katika kundi C

Mara ya mwisho mashindano haya yalifanyika 2017 nchini Gabon ambapo Cameroon walifanikiwa kuchukua kombe baada ya kuifunga Egypt kwa magoli 2 -1 katika mechi ya fainali

Je nchi gani unaipa nafasi ya kuchukua kombe hilo?

Nini matumaini ya Tanzania kwenye mashindano hayo?

Tutakuwa tunatumia mada hii kuhabarishana tukielekea kwenye ufunguzi wa mashindano hayo, yanayojiri wakati wa mechi, matokeo na matukio yote yanayohusiana na mashindano hayo

UPDATES

Ratiba 21/06/2019: Egypt vs Zimbabwe

Matokeo: Egypt 1 - 0 Zimbabwe

Ratiba 22/06/2019: Congo vs Uganda | Nigeria vs Burundi | Guinea vs Madagascar

Matokeo: Congo 0 - 2 Uganda

Nigeria 1 - 0 Burundi

Guinea 2 - 2 Madagascar

Ratiba 23/06/2019: Morocco vs Namibia | Tanzania vs Senegal | Kenya vs Algeria

Matokeo: Morocco 1 - 0 Namibia | Tanzania 0 - 2 Senegal | Kenya 0 - 2 Algeria

Ratiba 24/06/2019: Ivory Coast vs South Africa | Tunisia vs Angola | Mali vs Mauritania

Matokeo: Ivory Coast 1 - 0 South Africa | Tunisia 1 - 1 Angola | Mali 4 - 1 Mauritania

Ratiba 25/06/2019: Cameroon vs Guinea Bissau | Ghana vs Benin

Matokeo: Cameroon 2 - 0 Guinea Bissau | Ghana 2 - 2 Benin

Ratiba 26/06/2019: Nigeria vs Guinea | Uganda vs Zimbabwe | Egypt vs Congo

Matokeo: Nigeria 1 - 0 Guinea | Uganda 1 - 1 Zimbabwe | Egypt 2 - 0 Congo

Ratiba 27/06/2019: Madagascar vs Burundi | Senegal vs Algeria | Tanzania vs Kenya

Matokeo: Madagascar 1 - 0 Burundi | Senegal 0 - 1 Algeria | Tanzania 2 - 3 Kenya
Naona dalili za Uganda na Kenya kuvuka... yani tunashika nafasi ya juu kwa kutokea chini 😕😕😕
 
Halafu mwana siku yuko press hakuwa na tabasamu ni kama kuna msongo wa mawazo ni kama kuna kitu kinamsumbua. naunganisha dot tu ila sina uhakika. JWTZ ile press meeting kuna watu wamepigwa madongo na watatajwa isije kuwa ndio anatafutiwa njia ya kutolewa kafara katika wale waliomba watu wao wapate kazi. maana ile press ni kama wanaambiwa hatujali vyeo vyao wala nini na hii haijawahi kutokea katika history ya jeshi, kuna watu wameingia 18. just my thoughts nothing more
 
Baada ya kupata burudani kabambe kutoka kwa Harambee Stars hapo jana usiku, nililala usingizi mzigo fofofoooo hatimaye nikachelewa kuamka kwenda safari yangu niliyoipanga.

Ahsanteni Harambee Stars

Fantastic
😄😄😄😄
 
Halafu mwana siku yuko press hakuwa na tabasamu ni kama kuna msongo wa mawazo ni kama kuna kitu kinamsumbua. naunganisha dot tu ila sina uhakika. JWTZ ile press meeting kuna watu wamepigwa madongo na watatajwa isije kuwa ndio anatafutiwa njia ya kutolewa kafara katika wale waliomba watu wao wapate kazi. maana ile press ni kama wanaambiwa hatujali vyeo vyao wala nini na hii haijawahi kutokea katika history ya jeshi, kuna watu wameingia 18. just my thoughts nothing more


Funguka mkuu
 
hongera sana harambee stars Kwa ushindi poleni taifa stars sijategemea mlicheza mpira ya kiwango cha juu kuliko mechi ya algeria. what a very tyt east African derby.
kumradhi ,i mean mechi ya Senegal
 
Back
Top Bottom