2019 FIFA Women's World Cup

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Timu ya ya wanawake ya Ufaransa inaelekea kuja kuwa tishio kubwa kwa marekani, kwani watoto hao nililiwaona wana ball controll ya hali ya juu sana. Ingawa wachina wamefungwa na ujerumani, ni dhahiri kuwa walikuwa na resistance kubwa na ujerumani ilicheza mchezo wa hali ya chini sana.

Dada zetu wa Banyana Banyana wa South Africa walianza vizuri na kuwapa wakati mgtumu Spain lakini wamekuwa wakielemea sana kadri muda unavyokwenda na dakika hihi hihii wamefungwa goli la pili; sijui kama watakata tamaa.


Ratiba kamili ya michezo yote iko hapa Paris France

Updates: Banyana Banyana wameishiwa sana pumzi dakika za mwisho na kuishia kufungwa 3-1
 
Kombe la Dunia la wanawake halina mvuto sana, walipe promo bana lisikike vizuri
Kama uliangalia timu ya wanawake ya Ufaransa jana, wasichana wale walicheza kandanda la hali ya juu sana; si ajabu wakazifunga timu zetu zote za daraja la kwanza wakipambanishwa. Timu ya wanawake ya Marekani imekuwa kwa miaka mingi ikicheza vizuri sana na kuwa mabingwa wa dunia mara kadhaa, sijui mwaka huu wakafikia wapi kwa vile wachezaji wake wengi maarufu wameshazaa na wengine kustaafu.
 
Marekani ishajiimarisha kwa kila kitu, michezo yote inayo exist Marekani wanaicheza.

Mwaka huu kama hawajajiandaa vizuri, kombe linaenda kwa wengine
 
Nigeria wamelambwa haraka haraka sana na Norway!
 
Cameroun wamefungwa na Canada bao 1-0 ila akina dada wa cemeorun walionyesha mchezo wa nguvu sana kuliko timu zote za Afrika zilizokwisha shiriki (Nigeria na South Africa).

Mpaka sasa kuna timu mbili za kuangaliwa sana; Japan na France, ingawa Canada nayo inawakaribia. Nyingine zote zinacheza lakini kuna hili na lile. Ingawa Argentina imetoka sare na Japan, ila katika dakika tisini zote ilikuwa imeelemewa sana; kuna makosa madogomadogo ya upande wa ufungaji wa Japan ndiyo yaliyosababisha sare hiyo. Nadhani Japan watajipanga upya tena kunoa safu yao ya ufungaji kwani mashambulizi yao mengi yalikuwa yanakosa goli kwa "sentimita moja" tu. Mchezo wa England na Scotland nao haukuwa na ufundi wa kusisimua, wakati Brazil na Jamaica nao ilikuwa vile vile. Ngoja tusubiri timu ya USA tuone kama bado ni imara kama ile ya zamani.

Kwa mbali kidogo naiona China nayo kama timu ya kuwekewa jicho; wana spidi kubwa sana kiasi kuwa kila mara wanakaba watatu watatu; na defense yao inonekana kuwa ukuta wa mawe. Ujerumani iliwafunga kwa bahati bahati tu.
 
Katika michezo ya leo, Team USA imefanya mauaji dhidi ya Thailand kwa kuwafunga magoli 13-0 katika mchezo mmoja tu. Ingawa hapa kwangu mvua ilivyesha ikanikatia satellite langu kwa muda kama dakika 20 hivi, kwa hiyo kuna sehemu sikuiangalia, ila kwa jumla watoto wa Thailand walielemewa sana kwani kwa takribani asilimia 80 ya muda wote mpira ilikuwa uko kwenye lango lao. Baadhi ya maveterani wa Team USA walikuwamo, kwa mfano Morgan (aliyefunga mabao matano), O'Hara, Rapinoe, Carli Lloyd na wengineo; lakini hata wale wapya walionyesha uwezo wa hali juu sana.


Mchezo baina ya New Zealand na Uholanzi ulikuwa mzuri huku team ya Uholanzi ikimudu sana mchezo huo lakini walihangaika sana kupata mabao wakaishia bao moja tu kwenye dakika za majeruhi.

Mchezo kati ya Sweden na Chile haukuwa mzuri; huenda kwa vile walikuwa wakinyeshewa sana mvua ikabidi mpira usimame kwa dakika kama 25 hivi kipindi cha pili. Baada ya kurudi kumalizia muda uliokuwa umebaki ndipo Sweden ikapata bao moja la harakaharaka baada ya kuanza tu, na baadaye wakaongeza jingine katika dakika za majeruhi na kutoka na ushindi wa 2-0.


Michezo ya kesho Jumatano ni kama ifuatavyo:
 
Mchezo wa kwanza leo umekwisha na Nigeria imewararua Korea mabao 2-0. Mchezo ulikuwa mkali sana; bao la kwanza la Nigeria lilikuwa na utata kidogo kwani ilionekana kama yule mfungaji alisukuma mpira kwa mkono baada ya kuwa deflected na defender wa Korea. VAR ikaonyesha kuwa haikuwa hivyo, na goli la kwanza kwa Nigeria likwa limeandikwa. Baada ya hapo Korea walifanya mashambulizi makali sana lakini defense ya Nigeria nayo ikawa imara sana. Korea walikuwa na kiu sana ya magoli kiasi kuwa waligeuza formation kuwa 2-3-5 kusudi wawe na washambuliaji wengi kusaka magoli. Kosa hilo lilisababisha Nigeria iwafunge bao la pili kirahisi sana baada ya mshambuliaji wa na Nigeria kupata mpira akiwa katikati ya uwanja na kuupeleka golini kwa Korea ambako hakukuwa na walinzi wa kutosha. Nusura Nigera ipate goli la tatu kwa njia hiyo hiyo ila yule mshambuliaji alisogeza mpira mbele mbali zaidi ya spidi yake ukaweza kukamatwa na kipa wa Korea kabla yeye mwenye hajafika kutungua goli alilokuwa akipania.

That all for now folks: nitawaletea updates nyingine baadaye.
 
Haya tena; mchezo wa pili kwa leo nao umekwisha na Ujerumani imeibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Uhispania. Mchezo huu ulikuwa mzuri sana wenye upinzani mkubwa sana huku timu ya Uhispania ikitawala mchezo mzima. Ila kwa kwa kosa dogo walilofanya Uhispania katika kipindi cha kwa kwanza na kusababisha kufungwa bao moja, iliwafanya wajerumani wajijenge kwenye ulinzi zaidi ili kulinda goli hilo na hivyo mwishoni kufanya ujerumani wawe washindi ingawa uhispania ilionyesha mchezo na ufundi wa hali ya juu sana.

 
Kama unaijua olympique Lyon ya wanawake ambayo imechukua UCL ya wanawake kwa kuifunga barca ya wana wake ambayo ni Kali sana, basi huwez kushangaa uwezo na ubora wa France ya wanawake maana wengi wao wanatoka olympique lyon,

Natabiri watakaochukua hili kombe ni France ,Spain au USA
 
Haya tena; mchezo wa mwisho kwa leo ndio umekwisha hivyo na Ufaransa imeibuka kidedea kwa maogli 2-1. Mchezo huu ulikuwa wa kusisismua kuliko michezo yote iliyotangulia. Pande zote mbili zilicheza kwa kujiamini na kwa nguvu sana. Ufaransa ilipata goli la kwanza kwa mchezo mzuri sana, ila baadaye wakafanya makosa ya kujifunga wenyewe na hivyo kurudisha ngoma kuwa droo. Baadaye Norway nayo ikafanya makosa ya papara na kusababisha penalty iliyowapa ufaransa ushindi. Mchezo huu ulikuwa na burudani sana.

 
Mademu wanapiga mpira kama wanaume. Mimi nawaangalia na nina furahia.
Mimi napenda kuliangalia lile kipa la Brazil Barbara Ana mzigooo.
Usiangalie maumbile yao; angalia jinsi wanavyomudu mchezo. Kipa wa Jamaica alieweza kuzuia penalty na kipa wa Chile aliyepangua mashambulizi zaidi ya kumi golini kwake ni makipa wazuri sana.

Hebu mwangalie golikipa Christiane Endler wa Chile akiwa kazini


Halafu mwangalie golikipa Sydney Schneider wa Jamaica alivyopangua penalty ya Brazil

 

Nigeria v Korea Republic - FIFA Women’s World Cup France 2019
 
Mchezo wa kwanza leo uliohusisha Australia na Brazil umekwisha na Australia wameibuka kidedea baada ya kuwafunga Brazil 3-2. Mchezo ulikuwa wa kusisimua sana kwani pande zote mbili zilicheza kwa ufundi wa hali ya juu na kwa nguvu sana. Brazili ndiyo iliyoanza kupata goli kwa njia ya penalti iliyopigwa na Marta. Baadaye Chrstiane akafunga bao la kichwa, kwa hiyo hadi dakika 45 kipindi cha kwanza Brazil ilikuwa inaongoza kwa bao 2-0; hata hivyo katika dakika za majeruni za kipindi hicho Australia iliweza kupata bao moja lililofungwa kiufundi sana na Caitlin. Kwenye kipindi cha pili timu zote zilifanya jitahiada sana za kupata magoli lakini Australia ilionekana kuwazidi Brazil kwa kete na hivyo kujikuta imeongeza mabao mawili kiasi kuwa hadi kipenga cha Mwisho Australia ilikuwa inaongoza 3-2. Ikumbukwe kuwa timu hizi za Australia na Brazil zina visasi vya muda mrefu kuanzia world cup ya mwaka 2015 ambapo Australia illifunga Brazil 1-0 na matokeo yake timu ya Brazil ikakataa kushikana mikono na timu ya Australia baada ya mchezo huo. Hata juzi wakati Australia ilipofungwa na Italy iliapa kuwa lazima itaifunga Brazili ili kuweza kuendelea na mashindano hayo.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…